January 26, 2019
Nairobi, Kenya
Two people have been injured in an explosion at Nairobi's Latema Road-Tom Mboya Street junction.
Reports say a man hired a trolley pusher to carry a box. It is suspected the box contained an Improvised Explosive Device which exploded.
According to Nairobi Police boss Philip Ndolo, the man who hired the trolley pusher ran away immediately after the explosion. Ndolo has asked the public to be on high alert and report any suspected terror activities.
Source : KTN news Kenya
=====
Shambulizi la bomu limetokea katikati ya jiji la Nairobi usiku huu na kujeruhi watu wawili, polisi wathibitisha.
Mlio mkubwa ulisikika katika eneo la Odeon, moja ya viunga vyenye shughuli nyingi na mikusanyiko ya watu wengi katikati ya jiji la Nairobi.
Bomu hilo lilikuwa limefichwa ndani ya begi na kusukumwa kwa mkokoteni.
Mkuu wa polisi wa jiji la Nairobi Philip Ndolo amewaambia wanahabari kuwa, bwana mmoja mwenye asili ya Kisomali alikodi mkokoteni na kupakia begi lake, na walipofika eneo la tukio, kwenye makutano ya barabara za Tom Mboya na Latema mmiliki huyo wa begi alitoweka.
"Alimhadaa mwenye mkokoteni kwa kumwambia amsubiri akafuate kitambulisho chake ambacho alikisahau...hakurudi na baada ya muda mfupi kilipuzi kilichokuwamo ndani ya begi hilo kililipuka,"amesema bwana Ndolo.
Mlipuko huo umewajeruhi mwendesha mkokoteni na mfanyabiashara ndogondogo aliyekuwepo karibu na mkokoteni. Mlio mkubwa wa bomu hilo ulizua taharuki kubwa kwenye eneo hilo lenye stendi nyingi za mabasi ya abiria.
Shambulio hilo linakuja siku chache toka viunga vya hoteli ya kifahari ya DusitD2 kushambuliwa na kupelekea vifo vya watu 21.
Tayari eneo hilo limefungwa na polisi na vikosi vya kutegua mabomu vimeshawasili eneo la tukio.