Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Mwaka huu umeweka alama nyingine muhimu kwa muziki wa Afrika baada ya Tyla kushinda tuzo ya "Best Afrobeats" kupitia wimbo wake maarufu "Water." Tyla, wa Afrika Kusini ameshinda tuzo hiyo katika kipengele cha Best Afrobeats katika tuzo za MTV Video Music Awards (VMAs) za mwaka 2024 na kuwabwaga Chris Brown, Burna Boy, Usher na Tems.
Mbali na ushindi huo, Tyla pia alikuwa anawania tuzo nyingine ya "Best New Artist" na "Best RnB," akiendelea kung'ara katika tasnia ya muziki wa kimataifa. Tyla alishukuru, nakusisitiza utofauti wa muziki wa Kiafrika, huku akijivunia kuiwakilisha Afrika Kusini na mtindo wa muziki wa Amapiano.
Soma: Tyla Awabwaga Davido Na Burna Boy Kwenye Tuzo Za Grammy