Tyla wa Afrika Kusini amechukua tena tuzo ya Grammy

Tyla wa Afrika Kusini amechukua tena tuzo ya Grammy

McLaren

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2025
Posts
1,170
Reaction score
3,743
Wakuu,

Mwimbaji wa Afrika Kusini, Tyla, amewashinda Davido, Burna Boy, Ayra Starr na Eddy Kenzo na kushinda tuzo ya Best African Music Performance katika Tuzo za GRAMMY za 68.

Wimbo wa Tyla, “Push To Start”, ulikuwa umeingia kwenye kipengele hicho sambamba na “Love” wa Burna Boy, “With You” wa Burna Boy na Davido akishirikiana na Omah Lay, “Hope & Love” wa Eddy Kenzo na Mehran Matin, pamoja na “Gimme Dat” wa Ayra Starr akimshirikisha Wizkid.

Hii ilikuwa ni tuzo ya pili ya GRAMMY kwa Tyla, baada ya wimbo wake uliovuma sana “Water” kushinda tuzo hiyo hiyo katika GRAMMY za 66 mwaka 2024

photo_2026-02-02_09-21-00.jpg
 
Chibu akuje kutolea ufafanuzi imekuwaje ameshindwa kuleta hicho kidubwasha nchini!
 
CCM imewamaliza wasanii wote....huwezi julikana huko duniani kama nchini kwako hautambuliwi...

Sasa hivi Samia anataka kuwamaliza Content Creators
Ili afaidike na nini? Nieleweshen anataka kuwafanyaje haswa
 
Back
Top Bottom