Binafsi nazifahamu hizi
Defensive Mids
Hawa siku hizi wanacheza kama mabeki au mabeki wanacheza kama viungo wakabaji kwa timu zinazomiliki mpira sana. Mabeki viungo wanajulikana kama ball playing defenders (David Luiz, Pique, Ramos etc). Then kuna viungo wakabaji ambao pia huwa wanatumika kama mabeki wa kati kulingana na mchezo unavyokwenda, ila ni viungo (Luiz Gustavo akiwa na Brazil, Busquets, Xabi).
Destroyers
Hawa ni viungo ambao primary role yao ni kuharibu tu, kama Coquelin wa Arsenal, Tiago wa Atleti n.k.
Deep Lying Midfielders
Hawa primary role yao ni kuchezesha team ila kutokea kwenye half yao zaidi, kina Toni Kroos Madrid, Pirlo Juve, Verratti PSG n.k.
Creative/Attacking Midfielders
Simply wazee wa assists, primary role yao ni kufungua ngome za wapinzani na kutoa pasi za mwisho. Iniesta, Gotze, Coutinho n.k.
Box to box Midfielders
Hawa wanafanya kila kitu, wanatakiwa kuwepo popote mpira ulipo. Isco na Modric chini ya Ancelotti, Yaya Toure mara nyingi Man City, Rakitic Barca, Matuidi PSG n.k.
Offensive Midfielders/strikers
Hawa ni washambuliaji ila pia ni wachezeshaji, kina Benzema, Messi at times, Welbeck, Rooney at times n.k.
Unazifahamu aina ngapi?
Huo ni mtazamo wangu tu, ruksa kunisahihisha nilipochemka pia.