Tyson alikuwa anabebwa, overrated

Tyson alikuwa anabebwa, overrated

Castr,
Natamani nikuazime kitabu cha Mike Iron Tyson ili ujue ukweli.

Cus D'Amato hakumuokota Tyson mitaani. Alipelekwa kwake na mtu mwingine aliyemwona Tyson kwenye gereza la watoto na akaona talent yake.

Kwenye hicho kitabu anaeleza vizuri jinsi alivyopigwa Japan.

Kifupi kama Tyson haji kutokea kirahisi.
 
Mtoa Mada, unaweza kuwa una vijihoja lakini Mtizamo wa Chuki Umekujaa sana na hilo ni tatizo lililodhalilisha bandiko lako
Hahaha boss namheshimu Tyson kwa mchango wake wa kuizindua Tanzania juu ya ubondia. Ila nilichosema ni ukweli kwa kadri ukweli ulivyo.

Pinga kwa hoja.
 
Natamani nikuazime kitabu cha Mike Iron Tyson ili ujue ukweli.

Cus D'Amato hakumuokota Tyson mitaani. Alipelekwa kwake na mtu mwingine aliyemwona Tyson kwenye gereza la watoto na akaona talent yake.

Kwenye hicho kitabu anaeleza vizuri jinsi alivyopigwa Japan.

Kifupi kama Tyson haji kutokea kirahisi.
Mkuu sasa unaandika kitabu halafu unajikandia si utakua wa ajabu.

Haji kutokea kama Tyson?

AJ na Wilder unawajua lakini?

Alichokifanya Tyson chooote isipokua kua bingwa na miaka 22 watu walishakifanya. Na wanafanya.

Sababu ya yeye utoto kumkuta ulingo wa heavyweight ni hakupitia wenzake walipopitia mfano utakuta mabondia wengi umri huo bado wapo kwenye mashindano ya olympic au bado mapromota wanamzungusha.
 
Mkuu sasa unaandika kitabu halafu unajikandia si utakua wa ajabu.

Haji kutokea kama Tyson?

Muhammad Ali unamjua lakini?
Mkuu, sijasema naandika kitabu. Nina kitabu nilichonunua.
Baada ya Cassius Clay, ndiyo Tyson. Na kabla ya Clay walikuwepo akina Sunny Liston na wengine.
 
Castr,

Unachokisema wewe leo ndicho ninachokisema kila siku hata jana kuna mtu humu nilimwambia Tyson ni bondia wa kawaida sana anakuzwa tu, kwanza hana pumzi pia hawezi kuvumilia makonde.
 
Upo sahihi kabisa. Sahivi mapambano heavyweight ya kichovu kinoma. Watu wanaviziana viziana na kukumbatiana tu, hakuna burudani yoyote, unaona tu pambano limeisha.

Iron alikua anafata kama nyuki. Hata kama kapigwa bado utaona raha ya pambano.
Pambano lipi hilo la heavyweight walikuwa wanakimbiana?.
 
Unachokisema wewe leo ndicho ninachokisema kila siku hata jana kuna mtu humu nilimwambia Tyson ni bondia wa kawaida sana anakuzwa tu, kwanza hana pumzi pia hawezi kuvumilia makonde
Na kila unayemwambia kuhusu hili atakwambia juu ya skills za kuchezesha kichwa. Kuna mmoja nikamuuliza hivi unajua kwanini Matumla anaitwa Snake Boy? Akajibu hapana, nikamwambia ni anajua kukwepa ngumi kwa kichwa kwa haraka.

Uwezo wake huo muweke level moja na Ali. Akajibu mi nilidhani anaitwa Snake kwakua anatisha ulingoni. Nikajua kumbe nilikua naongea na mtu ngumi hajui historia yake.
 
Naona umesapoti nilichoandika.
Yah! Sipo kukupinga, wewe ukisema overrated ni sawa ni mawazo yako, ie sijali opponents wake, mie nasema nilikuwa naenjoy vile alivyokuwa anapigana ni moja kati ya wachezaji ndondi bora niliopata kuwatizama, kujilinda, kushambulia n.k n.k

Na ndio maana comment yangu ya kwanza sikuanza kumpinga mleta mada, alivyoongea vingine vina ukweli ndani yake, kiuchezaji kwangu alikuwa bondia bora.
 
"..boxing ability is not a natural gift to black men as many people think.."

''you've got to work bloodly hard 4 it.."
Legendary
 
Yah! Sipo kukupinga, wewe ukisema overrated ni sawa ni mawazo yako,ie sijali opponents wake, mie nasema nilikuwa naenjoy vile alivyokuwa anapigana ni moja kati ya wachezaji ndondi bora niliopata kuwatizama, kujilinda, kushambulia n.k n.k

Na ndio maana comment yangu ya kwanza sikuanza kumpinga mleta mada, alivyoongea vingine vina ukweli ndani yake, kiuchezaji kwangu alikuwa bondia bora.
Sawa ila kama unataka burudani ulingoni kwa Tyson ulikua unapotea kamcheki Dwight Muhammadi Qawi, Sugar Ray, Muhammad Ali, Chris Eubank (Baba), Chris Eubank jr (mtoto) na Drunken master.

Utaenjoy mno.
 
"..boxing ability is not a natural gift to black men as many people think.."

''you've got to work bloodly hard 4 it.." Legendary
Tell that to Sugar Ray, Joe Frazier, Muhammad Ali, Dwight Qawi
 
Hahaha boss namheshimu Tyson kwa mchango wake wa kuizindua Tanzania juu ya ubondia. Ila nilichosema ni ukweli kwa kadri ukweli ulivyo.

Pinga kwa hoja.
Mkuu nimesoma hoja na baadhi ya comments zako, na maoni yangu ni haya:

1. Kipindi cha kina Tyson, kilikuwa ni shifting era toka kwenye boxing kama burudani (more of an entertainment) kuja kwenye biashara (more of a business). Ukifatilia vizuri kwenye hizi zama mbili, utagundua kuwa kwny era ya kwanza boxing iliongozwa/endeshwa na passions,techniques na legacy (political/social) wakati kwenye era ya pili economic factors zilikuwa most influencial na hivyo kufifiza passions na techniques ambazo zilileta real fights in the boxing ring.

2. Kutokana na sababu hiyo hapo juu, Promoters na Promotion companies zilikuwa na sauti zaidi ya bondia na technical team yake. Hivyo issue kama kupigana na opponent gani, kwa wakati gani na kwa gharama gani vilikuwa chini ya wadhamini na si bondia.

3. Sababu ya 1 na ya 2, zikapelekea changes in boxers' mindset (Tyson in particular) from entertainment to business as well.

4. Mabondia wengine (pamoja na uliowaorodhesha) kwa zama hizo walipambana na target fights zao zilikuwa kupata match against Tyson ambaye alikuwa the most rated boxer hivyo ukipata pambano na Tyson hata ukipigwa unaweka mpunga mrefu mfukoni (hii ni domino effect ya sababu ya 1 hapo juu) kuwa 'pigana upate pesa'.

5. Ukiwa kwenye situation namba 4 hapo juu with plenty of options around, hata kama ni wewe utachagua pambano linaloguarantee ushindi(kwa nn uchanganye pilau yako na mlenda?). Hata CCM jana walichagua kupambana na TLP na UDP et all na sio CHADEMA.

5. Kuhusu issue ya hofu, hiyo ni kawaida unapokuwa ume-invest kwny jambo fulani lazima uwe na fear. Tyson na promoter wake walikuwa sahihi. Hii hata Mayweather Jr ameitumia sana ingawa tofauti na Tyson, Mayweather Jr alihakikisha anakuwa na muda mzuri wa kujiandaa na kumsoma mpinzani ambayeni tishio kabla ya kumvaa. Naye pia alikataa mapambano mengi ya wababe na alipigana when he felt the time was right for him.

6. Kwa kumtaza Tyson akipigana,nikiri kuwa the talent was there, he had the passion to fight and he was a natural warrior.

Angeweza kuwa-defeat hao uliowataja kama angetumia technique ya Mayweather, huyu jamaa ni genius wa mipango. Pamoja na watu kumtuhumu kubebwa baadhi ya mapambano kwny points, hakuna bondia aliyewahi kuondoa huo utata kwa kumpiga kwa KO/TKO, I think this was what Tyson lacked in his days.
 
Kweli kabisa, Tyson alikuwa anapiga mabondia wabovu, akina Mcneely, Botha, alipokutana na real boxers Evander, Lennox akakwama, alibebwa sana na media na promoter wake Don King.
 
Castr, Mawazo yako ni kama yangu, watu wanampenda Tyson, mim nikiwemo ila wanashindwa gundua madhaifu mengi aliyonayo
Hakua na pumzi
Starehe ilikua kipaumbele
Si mvumilivu wa makonde
Ndio maana alipokutana na manunda kama Evander, Lewis alikarishwa kirahisi hakaishia kuuma meno
 
Back
Top Bottom