Tyson Fury na Terence Crawford ni mabondia uchwara.

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2016
Posts
20,137
Reaction score
26,189
Hawa jamaa Tyson na mwenzake Crawford si chochote si lolote kwa kifupi ni waoga kupindukia.

Hawa wote wawili wana mkanda mmoja mmoja , Tyson ana WBC Super belt, na Crawford ana WBO lakini wapinzani wao wanaotaka kupigana nao wana mikanda mitatu lakini cha ajabu hivi vijamaa vinakwepa kwepa mixer visingizio kibao.

Tyson Fury ilibidi apambane na Oleksandr Usyk 19 April Wembley Stadium kuunganisha belts nne maana Usyk ana WBA,IBF na WBO ili apatikane Undisputed Champion(Champion mwenye belts zote nne kubwa za kidunia) na Lineal Champion maana kwa Sasa Lineal Champion ni Fury alioupata kutoka kwa Vladimir Klitschko. Tyson anamuogopa sana USYK ,anaogopa atadhalilika kama alivyodhalilika Anthony Joshua kwa kupigwa mara 2 na bondia aliye mpandia uzito πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚.

Wanasema Styles makes fight ,nikimuangalia Tyson Fury naona kabisa hatoboi kwa Usyk ,Anthony Bellew swahiba mkubwa wa Anthony Joshua licha na uwezo wake mkubwa sana wa boxing ila alipigwa K.O moja mbaya sana na Usyk kitu ambacho kinazidi kumuogopesha Gyps King (Tyson Fury).

Tukiachana na Fury ,turudi kwa huyu Terence Crawford (Role model wa Hassan Mwakinyo 🀣🀣🀣🀣) haka kajamaa nako taarabu nyingi ila maajabu hakana .

Ilibidi naye mwaka huu apambane na Errol Spence ila mchizi kachana nyavu kakimbia πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ maana Errol Spence alisema anatamani wapambane hata round 20 mpaka mmoja wao asalimu amri kama sio kufia ulingoni kabisa ,Crawford aliposikia hivyo akaona daah hapa nimedandia mtumbwi wa vimbwengo akachapa lapa fastaaaa


Kwa kifupi Crawford na Fury wanatunyima uhondo wapenzi wa ndondi kushuhudia Undisputed Champion kwa uoga wao wa kipumbavu .Hawafai , kazi Yao kupigana na vitoga tu πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚Hapo Fury angeambiwa apigane na Dillian Whyte au Deontay chapu angekubali ila kwa Usyk kakimbia
 
Majamaa kama majibwa koko takataka kabisa
 
haya erol kachezea kichapo fungua uzi mpya sasa
 
Ngumi si lelemama, unadhani wanapenda kupigana ndondi ni njaa.Wewe unawalaumu wakati wenzio kila siku sura zao zinakuwa kama sakafu ya zamani sana.
 
Wadau wa makonde (boxing na ufc) tumekuwa wanyonge sana humu JF.

Masimba na mayanga yametawala mwanzo mwisho humu, uzi kila baada ya dkk 1
 
Mods ingependeza mngeweka jukwaa la masimba na mayanga, lijitegemee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…