U JUHA WA AJIBU NI WA KIWANGO CHA FLYOVER

U JUHA WA AJIBU NI WA KIWANGO CHA FLYOVER

Watu wanakimbilia kumlaumu ajibu bila kuangalia upande wa pili. Wana uhakika gani kama alifanikiwa majaribio? Hata kama walionesha interest lakini wanaweza kubadilika baada ya kugundua kitu ambacho hawakukijua awali
Amezingua wakala wake kwenye mazungumzo.... Hakuitwa kwa majaribio alitakiwa mazimamazima.... Anaenda Simba nakwambia ....
 
Wachezaji wetu wanahitaji sana kupata elimu ya mikataba. Pili ni wakati muafaka sasa TFF iwekeze kwenye kuandaa mawakala wadogo wadogo ili kuwasimamia wachezaji wetu. Tatu TFF na SPUTANZA ziwe zinandaa semina kwa ajili ya wachezaji wetu wawe wanaweza kupambana na kuwa wavumilivu na sio kusubiri kesi za wachezaji kuvunjiwa mikataba.

Pia tuiombe wizara ya michezo/vijana iangalie kwa jicho la tatu suala la elimu ya mikataba, ukakamavu, upambanaji na kutokutaa tamaa kwa wachezaji wetu wa michezo yote kwani michezo ni ajira. Unapokuwa na wanamichezo takribani 10,000 wa michezo mbali mbali kama ngumi, mpira wa miguu, riadha, kuogelea n.k. wa kimataifa kwanza tayari wanakuwa na ajira, pili mapato watakayopata yatakuja kusaidia nchi na wao wataajiri pia watu wa kuwasaidia.

Mimi ni shabiki wa Simba, lakini kama ni kweli Ajibu ametema dili la Mazembe kwa ajili ya Simba hapo kachemka. Hata Simba wenyewe watakuwa wamechemka kwa sababu kiasili Ajibu ni mchezaji mvivu mvivu, hajitambui kabisa kipaji chake. Angekuwa makini yeye ndiye angekuwa anafuata njia ya Samata kabla hata ya Msuva.

Mpira ni mchezo wa muda maalum umri ukipita ndio basi tena. Leo hii wapo wapi Gerson Tegete, Haruna Moshi na Halfan Ngasa. Siasa za Simba na Yanga zimeharibu kabisa maisha yao ya baadae.

Ajibu alipaswa ajifunze moyo wa kupambana kama Samatta. Sijui wachezaji wa Tanzania wanakwama wapi. Ukipata historia za wachezaji wengi wa Afrika Magharibi wanavyokwenda Ulaya njia wanazopitia ni za hatari sana lakini hatimaye wanafanikiwa. Lakini hawa wa kwetu hata kupita njia halali hawawezi sijui tumelogwa na nani.
Wajinga ndiyo waliwao hama kweli. Wacha akachome mahindi maana ndicho alichochagua na muda na bahati aliyochezea atajutia baada ya 2yrs.
 
Usimlaumu Ajibu kaka,kuna kitu kinaitwa personal terms kama hakijafikiwa vizuri mambo hayawezi kwenda.Hata ukifuatilia personal terms za ajibu hazikufikiwa ndo maana mambo hayjaenda sawa,ebu tulicheki na hilo sio tunalaumu bure
 
Write your reply...Shida ni tamaa za Viongozi wa klabu na wakala wa mchezaji . Tp walijua kua Ajibu yupo huru ndio maana wali mtaka na wakala wa ajibu alishindwa kutoa maelezo moja kwa moja kuwa Ajibu kua teyari amesha saini mkataba na timu nyinge na pesa ya advance ameshachukua.

Na simba nao tamaa zime waponza baada ya kusikia ishu ya Mazembe wa kaona ndio muda wa kupiga pesa wakajitokeza wao ndio wenye haki na ajibu na wa kataka 220m na 20% ya hela endapo mazembe wata muuza ajibu kwa timu nyingine.

ukweli masharti walio taka simba ni tofauti na mchezaji husika na Bado tutaendelea kusema simba na Yanga ndio timu zinazo ua vipaji vya soka la Bongo
 
Ajibu katemaje dili la Mazembe?

Kabla Mazembe hawajaanza kumfukuzia alikuwa tayari amesaini mkataba wa awali Simba,TP Mazembe hawakuwa na taarifa hizo,Simba ndo wamewaambia Mazembe Ajibu ni wetu na si mchezaji huru na kama mnamtaka njooni kwa meza ya maongezi,wakaweka mambo mengiiiiiiiiiiii ikiwamo dola 100,000 ili mazembe wamchukue,jamaa wamechomoa wenyewe siyo Ajibu .

Ajibu ni kapeto atabaki kuwa wa hapa hapa tu,hajitambui,atazunguka Msimbazi,Jangwani na kurudi tena Msimbazi,wachezaji wetu wamerogwa,hawajitambui na aliyewaroga alishakufa
Sasa umeshaandika Mazembe wameshindwana na Simba sio Ajib then unaandika hajitambui au ulitaka Ajib azitoe yeye hizo dola 100,000 avunje mkataba na simba aende mazembe?
 
Samatta angekua Simba leo angekua Genk? Simba inatamani kuwa kama Mazembe lkn bado haiwezi kufikia level za Mazembe mwaka leo wala kesho.
1. Kumiliki uwanja
2. Kuwa timu yenye ushindani CCL.
3. Kutwaa ubingwa wa CCL.
4. Kuuza jezi online
na vingine kibao
Alf Moise Karudi Congo Ajib analaana anapishana na gari la mshahara kila mwaka.
nilichogundua wabongo tunatabia ya kuridhika mapema ukisoma soma stori za wachezaji weusi waliotoboa mbele unakuta walipitia mengi sijui kaenda ulaya kwa meli ya kudandia kapita italy ubaguzi ukamshinda kaenda ufaransa kalala barabarani kwenye baraza ndio anakuja kutoboa lkn huku kwetu mtu akicheza Simba Yanga kazi imeisha
Hata kama hujui radha ya kutoboa ulaya...inamana samata hamuoni?.
Jamaa anapokelewa na mawaziri kuliko Hata mabalozi wa nchi
Mchezaj ambae hata team ya taifa anastruggle kupata no ndo umsajil then ukapambane na Esperance, waydad, eto, al ahaly , zesco nk alaf Eti anagoma ! kweli mapimbi hawataisha duniani
Je unajua alikuwa anaenda kulipwa mshahara kiasi gani pale TP Mazembe?
Ajib huwezi mlinganisha na Samata, Samata alikuwa bado kijana mdogo Ajib umri umeenda ana miaka kama mi4 tu ya kucheza kwa kiwango cha juu.
 
Back
Top Bottom