U-Simba na Yanga unaua Timu yetu ya Taifa

U-Simba na Yanga unaua Timu yetu ya Taifa

Kichwa Kichafu

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2017
Posts
44,855
Reaction score
189,385
Habari!

Timu ya Taifa bado hali ni tete na itaendelea kuwa tete kila kuchika.

Huu U-Simba na Yanga unadumaza sana timu ya taifa isisonge mbele na kunajikuta tunarudi nyuma kila siku.

Kocha ni kama amepewa idadi ya wachezaji wa Simba/Yanga ibaki vile vile ndani ya uwanja bila kujali timu imezidi.

Kama wachezaji wa Simba/Yanga ni sita ndani ya uwanja basi watabaki hivyo hivyo hadi mwisho wa mchezo.

Kwa hali hii ya kuogopa kutoa wachezaji wa Simba/Yanga kuogopa mabwenyenye hali itaendelea kuwa hivi hivi na vipigo vitazidi zaidi na zaidi.

Natoa rahi weka pembeni U-simba na Yanga ujenge timu kama ni mchezaji wa Simba/Yanga piga chini weka mchezaji atakaye-deriver kitu bora.

Hawa wachezaji wa Simba/Yanga wanabebwa sana wa wageni ndio maana wakibaki wenyewe wanacheza makiriri tu!
 
Umeongea ukweli, timu ya Taifa imecheza hovyo kabsa yani hata kuvuka tu half yao nishida sembuse kushambulia. Tatizo sio kocha ila ni wachezaji wenyewe.
 
Tatizo ni makocha wa bei cheee! we unazani kwa makocha wetu kama hawa anatoka azam anakua kocha mkuu wa timu ya taifa. ulitegemea tuifunge tunisia kwa mpira gani ambaao wapo makini kwenye usajili wa makocha..

ACHA NIJIFUNZE KUNYAMAZA
 
Kocha mkuu ndagar nini sijui, kocha msaidizi matola&mwenine huyu kibonge wa coastal sijui. Ulitaka maajabu gani mkuu? Sometimes tufikirie. Mtu upo ugenini unatumia holding mildfilder 2. Maybe alitaka tushinde kuanzia matatu kwenda mbele
 
Lazima tukubali kuwa Tunisia wametuzidi mbali sana kisoka.

Lakini pia ni muhimu tutambue kuwa uwezo wa wachezaji wetu ni mdogo mno ila wanabebwa na wageni na wanapambwa na magazeti.

Kumlaumu Kocha tunakosea mno, angalia wachezaji wetu hata kupiga pasi sahihi wanakosea unataka kocha afundishe wachezaji kupiga pasi?
 
Mkuuu unakosea, Wamekuja makocha wa bei mbaya kama Poulsen, Maximo, Amunike nk nk nk. Yaaani hata aje Pochettinooooo au Zidane kwa aina ya Wachezaji wetu Wadumavu, Lishe Duni, Wasiofundishika, Waliobweteka na Vimafanikio kiduuuchu hutokuja kuona Maaajabu kwa hawa andunje wetu mkuu, tuache kuwalaumu makocha.
 
Wachezaji waandaliwe toka utotoni hapa bongo hivi kuna academy yeyote?
Umeongea ukweli, timu ya Taifa imecheza hovyo kabsa yani hata kuvuka tu half yao nishida sembuse kushambulia. Tatizo sio kocha ila ni wachezaji wenyewe.
 
[emoji23][emoji23][emoji23]

Kocha mkuu ndagar nini sijui, kocha msaidizi matola&mwenine huyu kibonge wa coastal sijui. Ulitaka maajabu gani mkuu? Sometimes tufikirie. Mtu upo ugenini unatumia holding mildfilder 2. Maybe alitaka tushinde kuanzia matatu kwenda mbele
 
Mkuu uliangalia mpira vizuri kweli?

Tunisia unawaita bora kwa mpira waliocheza jana ule?
Lazima tukubali kuwa Tunisia wametuzidi mbali sana kisoka.

Lakini pia ni muhimu tutambue kuwa uwezo wa wachezaji wetu ni mdogo mno ila wanabebwa na wageni na wanapambwa na magazeti.

Kumlaumu Kocha tunakosea mno, angalia wachezaji wetu hata kupiga pasi sahihi wanakosea unataka kocha afundishe wachezaji kupiga pasi?
 
Mbona Nigeria Jana pamoja na kuwa na kocha bora na wachezaji professionals wametoa safe 4-4 na Lone Stars,miye Jana tatizo nililoliona ni wachezaji wetu kutotekeleza vizuri majukumu ya game za away kwa kupoteza Pasi na kushindwa kumiliki mpira,mitandaoni tupo wajuaji wengi sana,miye naamini kwa Mkapa hao Tunisia tutawakataa,stars watabadilika na utashindwa kuamini,mbona equatorial guinea waligongwa na timu na wachezaji hao hao!!? Timu zingine Burundi,Kenya, Sudan
 
Mm niliangalia mechi yote...kwa kweli timu yetu ya taifa ina hali mbaya sana....pongezi kwa nyingi kwa Aishi Manula...ukitoa golikipa wengine wote walicheza kiwango cha chini sana....hiki ndicho nilichokiona....wachezaji wetu wengi hawana uwezo wa kulinda mpira adui asimpokonye....pasi nyingi zinapotea kabla ya kumfikia mlengwa.....stamina hafifu....Mkude....Himidi....na sure boy....kwa mm walicheza hovyo kabisa...Ingawa Tunisi nao hawakuwa vizuri sana....ila walituzidi....tusipokuwa makini mechi ya marudio pia watatufunga.....naunga mkono hoja ya kuwa na Academy za kutosha....bila hivyo tutasubiri Sana.
 
Tatizo sio Academy...vipaji vingi vinazuiliwa na wazazi wanaona hakuna future kwenye mpira..kwanza ifanyike kazi kubwa ya kuwabadilisha wazazi fikra zao hawa wanaocheza VPL huko utotoni walikuwa hawapati namba kwenye timu zao....
 
Kwanza mshukuru mungu mmefungwa kamoja tunisia sio levo yetu kabisa, lingine kocha hana kosa michezaji ya bongo inaibuka tu kutoka kusiko julikana alfu unategemea umfunge tunisia kweli?

Tuache utani
 
Back
Top Bottom