U-Simba na Yanga unaua Timu yetu ya Taifa

U-Simba na Yanga unaua Timu yetu ya Taifa

Kuna watu mnajua tu kulaumu yaani timu ya taifa itoke tu huko ikamfunge Tunisia nyumbani hivi hujui hiyo kufungwa moja na Tunisia away ni improvement ya hali ya juu inapaswa uwapongeze wachezaji waliocheza hiyo mechi
Tusitake mafanikio ya haraka haraka tu starz haijafika kwenye ubora wowote wa kuilaumu eti kwanini ifungwe na Tunisia
 
Ishu sio usimba na uyanga, ishu ni serikalu yetu kutotoa kipaumbele kwenye michezo, serikali haitoi uthamani na haijui kuwa michezo ni suluhu tosha kwenye ishu ya unemployment!! Serikali inapaswa kuwekeza kwenye mpira na sio kuleta masiasa ya kipuuzipuuzi, leo hii utawalaumu simba na yanga wakati serikali inawategemea hao kwa asilimia kubwa kuchukua pesa!!
 
Mafanikio yeyote yanahitaji jitihada ambayo kwa kiasi kikubwa tumeikosa hapa nchini kwetu. Tunaendeshwa na mihemuko na tunaridhika na mafanikio ya muda mfupi.
Mpira bila uwekezaji kuanzia kwenye ngazi ya chini kabisa itakuwa kazi bure.
 
Kocha mkuu ndagar nini sijui, kocha msaidizi matola&mwenine huyu kibonge wa coastal sijui. Ulitaka maajabu gani mkuu? Sometimes tufikirie. Mtu upo ugenini unatumia holding mildfilder 2. Maybe alitaka tushinde kuanzia matatu kwenda mbele
Hivi Matola ana cheti daraja gani na uzoefu upi wa kumfanya awe kocha wa timu ya taifa?
 
Tatizo makocha wanapangiwa vikosi kwa shinikizo la U_simba na U_yanga!
Mkuuu unakosea, Wamekuja makocha wa bei mbaya kama Poulsen, Maximo, Amunike nk nk nk. Yaaani hata aje Pochettinooooo au Zidane kwa aina ya Wachezaji wetu Wadumavu, Lishe Duni, Wasiofundishika, Waliobweteka na Vimafanikio kiduuuchu hutokuja kuona Maaajabu kwa hawa andunje wetu mkuu, tuache kuwalaumu makocha.
 
Back
Top Bottom