Uadui siasani uko huku chini kwa akina Mdude vs Lucas kule Juu Dr Nchimbi amesema " Mbowe alinipigia Simu mara 5"

Uadui siasani uko huku chini kwa akina Mdude vs Lucas kule Juu Dr Nchimbi amesema " Mbowe alinipigia Simu mara 5"

... huku chini tunaishia mikwara wakati huko juu wanarushiana makombora huku wanachekeana!
🀣
 
Hili liwe funzo zuri Kwa Wanasiasa wadogo Wadogo akina Yeriko, Maranja, Mdude, Choice variable nk

Katibu Mkuu wa CCM Dr Nchimbi amesema Mbowe alimpigia Simu mara 5 Ili kumjulisha habari za mauwaji ya Shujaa Ally Mohamed Kibao lakini yeye Nchimbi hakupokea kwani alishapata taarifa na alikuwa amevurugwa kweli kweli

Dr Nchimbi amesema alimjibu Mh Mbowe Kwa meseji na wakawa wameelewana.

Huu ndio Ukomavu wa kisiasa siyo kila jambo ni Siasa uchwara na kutukanana tu.

Soma Pia: Dkt Nchimbi: CCM imekasirishwa sana na mauwaji ya Ali Kibao na serikali iharakishe haraka uchunguzi na matukio yakomeshwe

Mungu wa mbinguni awabariki sana Dr Nchimbi na Freeman Mbowe

Ahsanteni sana 🌹
Sasa alimpigi mchimbi kama nani
 
Back
Top Bottom