Uambiwe?!

Uambiwe?!

unaweza ukaambiwa na usichape lapa vile vile, jamaa wakazidi kukucheka ujinga. Jibu la uambiwe au usiambiwe litategemea kama unapenda "love iz blind" au unapenda "love is passtime".

Kutembea au kukaa sio swali...uzuri wa kujua ni kwamba utakachofanya baada kinakua ni maamuzi yako wewe...huku ukijua kila kinachoendelea!
 
Lizzy mambo vipi wewe, me naona bora kuambiwa ingawa wakati mwingine anaekwambia nae awe kweli ana nia ya kujenga na si kubomoa, mwengine atakuwa ana nia ya kubomoa ili ajenge yeye...
 
Lets say kuna uhakika....hamna chokochoko, wivu wala unoko!!!Bora kuambiwa uamue mwenyewe kusuka au kunyoa!!!
Hata kama utasamehe itakua ni kwa terms zako binafsi na hutochoreka tena maana huwezi kutamba ama kujionyesha mbele za watu kwamba ni hivi na vile kumbe hujui tu!!!

kuna kipindi nilikuwa na malumbano na mr, nilikuja kuambiwa na dada yangu hii ishu lakini alinianzia mbali...kistaarabu/kunipooza/kunishauri...hapo unapata nafuu coz unatapa na counselling kabisa....ilinisaidia sana kujua malumbano yanaletwa na nn, baada ya hapo tuliweka mambo sana maisha yanasonga kwasasa, na nadhani amekuwa pia na kauoga fulani hata kama anafanya anajua mkataba tuliowekeana nikija kujua kwamba bado anafanya bac atakuwa ameuvunja mwenyewe na hapo hakutakuwa na maelezo...ndio mana nasema kuna faida na hasara zake na inategemea na mleta habari ameileta kivipi.
 
Mimi nafikiri kwa hali ya ubinadamu kama kweli unampenda nduguyo ni vema ukamwambia au kumpa tahadhari juu ya mambo flani ambayo hayako sawa. But kama alivyosema nyamayao umwambie kistaarabu. Si lazima uanze na haloo haloooo nimemwona mwaflani kasijui nini nii...................au jana shemeji alikuwa na ,.... hapana tafuta mwanzo mzuri kisha muwe kama mwadiscuss ucheck mwelekeo wake kisha wezamalizia tu na mh kuwa makini mwenzangu maana wanaume/wake hawaaminiki..........likitoka hili toka kwako lazima mwambiwaji atahisi kuna kitu so up to yeye aombe apewe mkanda mzima au aanze chunguza mwenyewe..........Ukikurupuka itakugeukia weye.
 
Wewe niambie na mimi nitatumia muda wangu kwa ajili ya kuchunguza ukweli wa jambo uliloniambia

Wengine wanaambiwa....wanachunguza.....wanathibitisha....wanaombana msamaha.....maisha yao yanaendelea kama kawa.....then mtoa habari anaonekana hana maana.....
 
Wengine wanaambiwa....wanachunguza.....wanathibitisha....wanaombana msamaha.....maisha yao yanaendelea kama kawa.....then mtoa habari anaonekana hana maana.....
RR kweli kabisa mtoa habari baadae huja kuonekana ni kama vile mnafiki ila mimi huwa nafikiria kuwa yule mtoa habari inategemea uhusiano wenu wa karibu ukoje
 
maumivu basi bwana finest ,hili limoyo langu haliwezi tena beba vitu acha yakae huko ikitokea nikajua haya tutajuana mbele kwa mbele woi.
Tatizo huwa linakuwa pale unapogundua halafu wengine huwa wanaanza kuwaambia rafiki zao "Kwanini hamkuniambia kwani mlikuwa kimya kwanini mlinificha" basi anaanza ugomvi na marafiki pia
 
Mimi nafikiri kwa hali ya ubinadamu kama kweli unampenda nduguyo ni vema ukamwambia au kumpa tahadhari juu ya mambo flani ambayo hayako sawa. But kama alivyosema nyamayao umwambie kistaarabu. Si lazima uanze na haloo haloooo nimemwona mwaflani kasijui nini nii...................au jana shemeji alikuwa na ,.... hapana tafuta mwanzo mzuri kisha muwe kama mwadiscuss ucheck mwelekeo wake kisha wezamalizia tu na mh kuwa makini mwenzangu maana wanaume/wake hawaaminiki..........likitoka hili toka kwako lazima mwambiwaji atahisi kuna kitu so up to yeye aombe apewe mkanda mzima au aanze chunguza mwenyewe..........Ukikurupuka itakugeukia weye.

nina ndugu ambae ana kifua cha wacwac kama chako, cku ya cku alivyokuja kuambiwa alinical kunielezea hayo mambo kumbe mie nayajuaa kitambo sana...nilimckiliza kama ndio kwanza nayackia kwake kumbe yeye anafanya marudio 2 bado kuna mengi hayajui na cwez kumwambia coz nitaendelea kumuumiza tu...pa1 na kujua ndoa yake inaendelea kama kawaida...haya mambo hayatabiriki jamani.
 
Tatizo huwa linakuwa pale unapogundua halafu wengine huwa wanaanza kuwaambia rafiki zao "Kwanini hamkuniambia kwani mlikuwa kimya kwanini mlinificha" basi anaanza ugomvi na marafiki pia

ukiona lawama zimeanza moja kwa moja na unajua yaliyopo nyuma ya pazia bac huna budi kunyamaza uckilizie tu mwenzio anavyougulia otherwise labda uwe umetajwa kwenye kesi...kama hukutajwa unapiga kimya tu kuepusha malumbano.
 
Kabisa Nyamayao halafu mimi naona kama hii ishu kama vile haina formula
 
Wengine wanaambiwa....wanachunguza.....wanathibitisha....wanaombana msamaha.....maisha yao yanaendelea kama kawa.....then mtoa habari anaonekana hana maana.....

Nadhani hii ndo sababu kubwa ya watu kushindwa kuwaambia,
usaliti anaoufanya mmoja baina ya wapendanao,kwani mwisho wa siku,
AIBU inakuwa kwako!!!!!!!!!
 
Nadhani hii ndo sababu kubwa ya watu kushindwa kuwaambia,
usaliti anaoufanya mmoja baina ya wapendanao,kwani mwisho wa siku,
AIBU inakuwa kwako!!!!!!!!!
Mkuu ulikuwa wapi ulikuwa busy unajivua MAGAMBA nini??
 
infidelity zipo tu hata tufanyaje!

mi naprefer msiniambie kama namegewa.. its better that i don know and life goes on.. sasa ukijua ndo utafanyaje? umuache uliye nae? una uhakika gani mwingine atakua perfect?
 
Mkuu ulikuwa wapi ulikuwa busy unajivua MAGAMBA nini??

We acha tu,
wengine wanajivua magamba, wengine samonge kwa Babu,
Basi balaa tu!
Anasemaje hapa Lizzy na mambo yake ya UAMBIWE AU?
 
NIKIWA NA MIAKA 25 (ENZI HIZOOOO)NILIWAHI KUMWAMBIA RAFIKI YANGU JUU YA MAHUSIANO YA MPENZI WAKE NA MWANAMKE MWINGINE , KWA BAHATI NZURI AKAJIHAKIKISHIA KWA MACHO YAKE ALIPOENDA KUWAKUTA NYUMBANI KWA YULE MWANAMKE WA NJE ...RAFIKI YANGU ALIZIMIA KWA MUDA WA SAA 5 (KUANZIA SAA 11 JION MPAKA 3.50 USIKU) NDIPO ALIPOZINDUKA, da!! NILIOGOPA KUPITA KIASI NIKAHISI SASA NTAENDA KUOZEA JELA HUYU AKIFA, BAHATI NZURI ALIZINDUKA .MWANAUME AKAOMBA MSAMAHA WAKASULUHISHA NA MAISHA YAMEENDELEA WAMEOANA SASA HIVI. YULE MWANAUME (SHEMEJI YANGU) HAKUNICHUKIA KSB ALISEMA ETI YULE MWANAMKE WA NJE HAKUMPENDA BALI ALIMKUBALIA KUONDOA USUMBUFU KSB ALIKUWA ANAMSUMBUA SANA, HATA RAFIKI YANGU HAKUNICHUKIA ILA KILE KITENDO CHA KUZIMIA KILINIUMIZA SANA NA NILIAPA,NA NAENDELEA KUAPA KUWA SITAMWAMBIA TENA MTU MWINGINE MAOVU YA MPENZI/MUME WAKE BORA APATE HABARI HIZO KUPITIA MWINGINE AU YEYE MWENYEWE.

MIMI NAPENDA SANA KUAMBIWA HAIJALISHI NIMEAMBIWA NA NANI IWE NDUGU,RAFIKI AU YEYOTE YULE , ILA HATA NIKIAMBIWA NI LAZIMA NIFUATILE JE NI KWELI?? AU UZUSHI TU, NDIPO NICHUKUE HATUA.NAENDELEA KUAPA KUMWAMBIA MTU HABARI MBAYA ZA MPENZI/MUME WAKE SIWEZI TENA NA TENA.
 
Binafsi hua nafikiria siku nikiwa kwenye mahusiano alafu mwenzangu akawa sio mwaminifu...mtu wangu yeyote wa karibu akajua ningependa aniambie.Na ikitokea asipofanya hivyo nikaja kugundua alijua akanyamaza ntamkasirikia.

Faida ya kuambiwa ni kwamba unajua kinachoendelea na unajipanga kukabiliana na ulichoambiwa.Ubaya ni pale unapotembea kichwa juu ukijua umepata kumbe kila mtu anajua umepatikana.Wanakuchora kwa maana nyingine.
Je wewe unaonaje?Uambiwe au uachwe kizani?

Kwanini tuna-focus kwenye negative tunapokuwa kwenye mahusiano??
Hebu tubadilike tunavyoyachukulia mahusiano. Kwenye mahusiano kuna raha nyingi sana, kama kufundishana, kukumbushana, kuelemishana, kutiana moyo, kufarijiana, kuonyana, na n.k.
Sio vizuri kuanza mahusiano ukiwa na wasiwasi au hujiamini au kumuamini mwenzio..
 
Back
Top Bottom