Uaminifu ndio ishara ya kumpenda Yesu

Uaminifu ndio ishara ya kumpenda Yesu

Niseme ukweli, mimi nilishakuaga mlokole, na kiukwel kwa mara ya kwanza baada ya kutokewa na scenario hii ya kutokwa machozi bila kujua, ndipo nikaachaga kuwakebehi walokole mpaka hiv leo.

Sikua na shida kusema nilikwenda church kulia shida.
Sikua naumwa
Sikua na uhitaji wowote nakumbuka.

Ila kuna ile feeling automatic ilinikumba ya kumtafakari Mungu na upendo wake na kisha kuona kama Mungu kanitendea mambo meengi sana na wala sikua nina muda wa kujal hayo. Bas automatically nilijikuta nimepiga magoti na kulia machozi ikiwa ni ishara ya ku appreciate yale Mungu alikua amenitendea.
Ilitokea tu na baadae nikaja kujishtukia nikajiona kama nimechanganyikiwa hiv, how come na mimi nalia lia.😂😂😂.

NB
siku hiz nilishaanguka na kurud dhambini. Ila maisha yale ni mazuri sana
Hongera kwa kuijua kweli nayo kweli itakuweka huru.


Lakini bado liko tumaini la kurejea kwa Mungu pamoja na makosa, maovu na dhambi ambazo tumemkosea Mungu.

1 Yoh 1:8-10​

Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu. Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote. Tukisema kwamba hatukutenda dhambi, twamfanya Yeye kuwa mwongo wala neno lake halimo mwetu.


Usife moyo wa kukata tamaa, Mungu ni pendo anatupenda sote, tena anafurahi kuona tunaziacha njia zetu mbaya na kumrudia yeye.

Haijalishi tumejikwaa na kuanguka mara ngapi, ila yeye husamehe na kusau yote.
 
Hakika, naamin Mungu atanipa tena nafasi ya pili kwa wakat wake.

Hii situation haijaniondoka completelly,mara kadhaa bado huwa nakumbwa na ile hali ya kuugua sana moyoni kila napojiona kama nimepotea kabisaa, bas naomba tu Mungu anisaidie nisifie huku niliko.
Ninakuombea,

Mungu Afanye njia na kukurudisha kundini,

Maana imeandikwa hayupo ajaye Kwa Yesu bila Mungu kuachilia kibali juu yake, maombi yangu Kwa Mungu, yakupe kibali, minyororo ikuachie uwe huru.

Ubarikiwe. Amen
 
Ujinga na upumbafu ni kule kujiona ni wewe tu upo kamili mbele za Mungu! Halafu wengine wote wasiotenda kama wewe unawaona wote ni wenye dhambi!

Huo ndio upumbavu kwa wote wenye kujiona ni wakamilifu sana kuliko wengine

Shenzi kabisa
Hii ni kauli ya mtu aliyeshindwa maishani. Ptuuuuuuuuuu
 
Alafu mbona huu umumbe hauhusiani kabisa na walokole? Walokole hawalii kama anavyosema huho Kardinali, wao wapo tofauti kabisa.
 
Akiisha maliza kulia;
Anakwenda kusimanga majirani
Kunanyasa na kutesa wa nyumbani kwake
Tegeneza vita na mwandoa mwenzie
Nk
Nk
 
Back
Top Bottom