Uamke asubuhi ukute account yako ina $150 billion utafanya nini?

Uamke asubuhi ukute account yako ina $150 billion utafanya nini?

Kwanza heshima bar

Pili natengeneza hela zangu mwenyewe

Tatu natafuta ukweli kuhusu matokeo ya uchaguzi 2015
 
Mzigo wote nauhamishia Cayman Islands ili usipigwe kodi baada ya hapo natulia mwezi mzima kuchua mwili!..
Mawazo ya kimasikini kuendelea nayo na mtonyo wote huo ndio utashangaa nusu unaipeleka kanisani bure!..
 
Asubuhi ukute bank account ina $150 billion kama Jeff Benoz utafanya nini?
Nasaidia ujenzi wa shule za msingi ziwe bora ( maabara na magorofa kama mbele), jenga apartments za haja Dodoma, jenga viwanja kama sita hivi vya kabumbu na nyasi la kitasha, jenga race track dar es salaam, jenga hospitali ya watoto ya kisasa, jenga kiwanda cha kusaga unga na kuufunga, kama bado hazijaisha ntajenga shule ya sekondari na kituo cha television, pia nta-fund projects za watanzania kama za kutengeneza magari, kompyuta, simu nk, mwisho ntasaidia elimu ya sekondari na kuendelea mpaka juu iwe kwa kiswahili ( hili ntalifanya kwa kuwahonga wanasiasa). Kama bado zipo ntaendeleza ujenzi
 
Nitarudi kulala, manake nikiamka tu hiyo $150B itayeyuka.
 
Ntamlipa fidia "Jamaa" ili akubali kuachia ngazi
 
Loo ndoto zinaleta shda kumbe shida zikizidi had ndoto zake huwa zinapatikana
 
Impossible !!! Did u convert to TZS and see the figure?
 
Back
Top Bottom