Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu amerudishwa rumande baada ya kumalizika kwa usikilizwaji wa Shauri la Kikatiba kwa siku ya leo Julai 23, 2026 Shauri Na. 7300/2026 limesikilizwa Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu Dodoma, inayoketi vikao vyake katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, ambapo uamuzi wa Shauri hilo utatolewa Septemba 16, 2026.
Shauri hilo lilifunguliwa na mawakili Kulwa William Maduhu, Nashon Nkung na Paul Kisabo dhidi ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP), Mkuu wa Gereza la Ukonga, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na Tundu Lissu.
Soma: Bwana Jela Gereza asema hatawaruhusu viongozi wa CHADEMA kumuona Lissu sababu kesi iko mahakamani. Jaji amshangaa
Shauri hilo linasikilizwa na jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Amir Mruma. Leo lilikuja mahakamani kwa ajili ya kuendelea na maswali ya dodoso kwa shahidi pekee wa Jamhuri, Mkuu wa Gereza la Ukonga, Andrew N'tamamiro.
Mahojiano hayo yalifanywa na wadaawa wengine baada ya mjibu maombi wa nne katika shauri hilo, baada ya Tundu Lissu kukamilisha jana maswali yake ya dodoso kwa shahidi huyo.