1. Ile sheria ya kulazimisha wawakilishi wa wananchi, lazima wadhaminiwe na vyama, its a bad law, na inakwenda kinyume cha Katiba ya JMT inayotoa uhuru kwa kila raia kushiriki katika uongozi wa serikali tangu ya mitaa hadi serikali kuu, hadi mahakama kuu ilishatoa rulling hicho kipengele kuwa ni 'unconstitutional' na kiwe struck out from the books of law!. Naamini Chadema hilo wanalifahamu, hivyo kitendo cha kutumia kipengele hicho hicho ambacho ni bad law, to its advantage, is "A Big Mistake!".
2. Ukishachaguliwa, Diwani au Mbunge, hata kama ulidhaminiwa na chama, wewe, unakuwa umechaguliwa na wananchi, na unakuwa ni mtumishi wa watu na kule kwenye ngazi za maamuzi, Baraza la Madiwani na Bungeni, unawakilisha maslahi ya wananchi waliokutuma, na sio maslahi ya chama kilichokudhamini, japo katika uwakilishi wako, pia maslahi ya chama yatazingatiwa. Kitendo cha chama kuwafukuza wawakilishi halali wa wananchi kwa maslahi ya chama, is "A Big Mistake!".
3. Kitendo cha kuwavua uanachama madiwani wake hawa, waliochaguliwa na wananchi, (sio chama) bila kuwasikiliza, ni kuwa "condem Unheard", which is against principles of Natural Justice, and this is a "A Big Mistake!".
4. Uzoefu wa siasa za Kanda ya Kaskazini, watu wanachagua watu na sio vyama, ndio maana CCM wanajua wazi kuwa, wao CCM, kuanzia Mwenyekiti wao, sekretariat yake, CC yao na NEC nzima ya CCM, hata wakapige kambi Moshi mjini, wakeshe kwa siku 30 mfululizo usiku na mchana huku wakipiga kampeni ya nguvu kwa kutumia mabilioni yao wanayofisidi, na kuwavisha wanamoshi wote, zile T.Shirt na kofia, pamoja na kulisha pilau la nguvu siku zote 30, Ndesa hawatamng'oa!. Kitendo cha Chadema kuwavua uanachama watu wa watu mjini Arusha, it's "A Big Mistake!".
5. Wenzao CCM walipokuja na makelele ya kujivua gamba, nilisema CCM, kuanzia Mwenyekiti wao, na kelele zote za Nape na Chiligati, hawana ubavu wa kuwavua uanachama hao watuhumiwa wa ufisadi kwa kuhofia retaliation ya watu wao, ndio maana mtashuhudia kwenye kampeni za Igunga, CCM lazima impigie magoti RA. Amini nakuambia, hawawezi kuwafanya lolote EL na AC, sana sana watawabembeleza kujiudhuru nyadhifa zao, lakini sio kuwavua uanachama, kwanini Chadema, chama cha matumaini, kifanye makosa ambayo CCM iliyochokwa, haiwezi kuyafanya, ya kuwavua uanachama wachaguliwa wa wananchi?!. That is "A Big Mistake!".
6. Chama makini kama Chadema, is expected to do the right thing, at the right time. Hatua hii, ya kuwavua uanachama madiwani pendwa Arusha, hata kama it was the right step, imekuja at the wrong time!, wakati wakitafuta justification ya kulitwaa jimbo la Igunga, ndio chama kinaanzisha tifu kanda ya Kaskazini ambako ndiko kwenye mizizi yake, mimi sijui, Chadema, imeyafanya hayo kwa kutegemea nini?.
7. Wakati nikiuleta ukosoaji huu, sio vibaya nikiwakumbusha Chadema baadhi ya maamuzi yake na matokeo yake. -Kumuengua Mwera Tarime, niliwaambia humu humu JF, kuwa it was a mistake, matokeo sote tunayajua!. Kususia kutangazwa kwa matokeo na kutomtambua rais, nilicoment humu humu, matokeo yake sote tunayajua, na jinsi Chadema ilivyonufaika na hatua hizo.
8. Niliwahi kuwapa Chadema, ushauri fulani, wapenzi na mashabiki wa Chadema, mlinibeza sana, including viongozi wenu. Mimi nikawasisitizia kuhusu, internal reforms na 'the winning coalition' including strategies kuelekea 2015, mpaka leo, bado sijaona, tuendelee kusubiri, 'the playing ground is not level, and never will it be, hivyo, 2015, tutaingia tena kwenye mechi ile ile, katika mazingira yale yale halafu tutegemee matokeo tofauti? UPDATE. Nime happen kukutana na mjumbe mmoja wa CC ya Chadema asubuhi hii, amenifafanulia A-Z ya kilichotokea. Chadema walifanya kila waliloweza ili kuwarudisha kwenye mstari lakini ilishindikana. Hao madiwani walizidi kuitunishia misuli CC ya Chadema, hivyo Chadema kama chama, was left with no option bali kuwatimuaPasco
Mkuu Pasco niruhusu nizirejee hoja zako kama ilivyozileta nikiwa na mawazo huru yasiyofungamana na siasa za upande wowote au kuwa na ushawishi.
Hoja # 1:Ni kweli sheria hiyo si sahihi kwasababu ulizozitaja. Mahakama kuu ilitoa hukumu nadhani kesi ya Mtikila(Judge Rugakingira RIP). Serikali ilikata rufaa na suala hilo bado lipo mahakamani na sijui kwanini mahakama imeamua kulikalia kimya, pengine ni kutokana na
conflict of interest kati ya wateule wa mahakama. Chadema inawajibika kwa sheria za nchi hata kama haikubaliani nazo hadi itapokuwa vinginevyo. Sisi wananchi tuna jukumu la kushinikiza kuhusu mabadiliko hayo. Labda ungesema Chadema walipaswa kuonyesha mfano tofauti ,lakini pia inategmea matokeo ya majadiliano kama ulivyoyaleta katika
update yako.
#2: Bado tunarudi pale pale kuwa sheria zetu zina utata sana na sio kwa Chadema tu. Chama kinapokudhamini ni sawa na mwajiri wako wa zamani anapokupa
reference letter na ukishaajiriwa ndio mwisho wa i
nfluency yake. Ndivyo ilivyo kwa madiwani, wabunge n.k mwajiri wao ni wananchi na wanawajibika kwao, lakini ni sheria hiyo hiyo inayosema chama kinauwezo wa kumvua uongozi mchaguliwa bila kumpa haki mwajiri (mwananchi) kumvua uongozi. Kwa mazingira yaliyopo Chadema ilikuwa na uamuzi unaolingana na sheria zetu, kama ni sahihi au la hilo ni jambo lingine,lakini je walifanya kulingangana na taratibu zetu, jibu ni ndiyo. Hapa ndipo tunatakiwa tuangalie upya wakati wa kujadili katiba mpya.
#3: Nadhani waliitwa katika vikao halali na hawakuwa condemned.Rejea
update yako.
#4: Chadema haina sababu ya kufuata mipangilio ya CCM, na inadhima kubwa sana ya kubadilisha mwelekeo wa watu kuhusu uchaguzi ili watu wachague sera za chama na si mtu au watu. Kosa hilo limefanywa na CCM na linawagharimu ni vema Chadema wakalitafutia dawa.
#5: Haa! yaani makosa yaliyofanywa na CCM ndiyo yarudiwe na Chadema! CCM kinameguka kwasababu kiliacha misingi ya uongozi (
principles) na kukumbatia haiba(
personalities). Uamuzi wa Chadema ni wa kuonyesha njia kuwa wao wanaweza na hakuna zaidi ya Chama. Kuendelea kuwalea watovu wa nidhani ni kufuga na kuzalisha vi-EL na vi-RA au vi-CH vidogo vidogo na vitakapo ota mbawa ndipo yatawakuta ya CCM. Kinga ni bora kulilo kuponya.
#6: Uamuzi sahihi ni ule unaofaa kwa muda muafaka. Igunga ni jimbo moja tu na pengine RA asingejiuzulu tusingekuwa na uchaguzi. Ni bora Chama kikajijengea imani ya kuaminika bila hofu ya uchaguzi kwani chaguzi zipo nyingi na zitakuja lakini
credibility ya chama hutengenezwa kwa miaka mingi na kuharibika kwa saa moja. Hakuna haja ya kuogopa maamuzi magumu kama yanayoisumbua CCM na serikali yake kwa hofu ya jimbo moja au mawili, gharama za
credibility ya chama ni kubwa sana.
#7: Siasa za Tarime ni
very complicated, Mwera alipotemwa Chadema akarudi CCM huyu hakuwa muumini wa sera bali tumbo lake. Nashukuru mh Mbowe alikwenda Tarime na kuwapasha ukweli. Kwa hali yoyote lazima tukubali siasa za Tarime ni
beyond politics, ideology na policy.
#8: Nakubaliana na wewe kuwa bado uwanja wa mapambano si sawa(level), kuhusu kuunda
coalition nadhani una maanisha na wapinzani wengine, labda tujiulize Mrema ba Cheyo ni wapinzani? CUF yenye uhusiano wa karibu na CCM ni wapinzani. Nadhani ili tuwe na uwanja mzuri agenda ya katiba mpya lazima ipewe kipaumbele , ichukuliwe na Chadema kabla ya mwaka kesho.
Hitimisho
Uamuzi wa Chadema kuwavua uanachama ni sahihi kwasababu hakuna mtu au watu au Organization iliyowahi kufanikiwa bila nidhamu.
Ni nidhamu inayowatesa CCM sasa hivi.
Nilishawahi kuwaonya Chadema kuwa suala la Arusha lilikuwa la kitaifa na zaidi, na kuliachia madiwani ilikuwa kosa kubwa sana.
Hata baada ya kutangazwa muafaka niliwasihi watoe msimamo cha kushangaza walikaa kimya kwa wiki mbili.
Hii inaonyesha kuwa Chadema hawana vitengo vya kutathmini hali ya kisiasa na kufanya maamuzi ya haraka na busara.
Hili lilipelekea
political base' kuwa
demoralized.
Mkuatano wao wa Arusha na maoni juu ya uamuzi wao katika blogs na vijiwe unatetea hoja yangu kuwa wapenzi na wanachama walikereka sana na mwenendo wa Chama chao na kwamba maamuzi magumu waliyochukua wame
excite base yao tena.
Ingawaje naunga mkono maamuzi ya CC lakini nadhani kuna mapungufu ambayo hayaelezeki kwa njia ya kawaida.
Uongozi wa mkoa na wilaya ulihusika vipi katika sakata zima na je hakuna uzembe miongoni mwao.
Najua uongozi wa wilaya umejikosha kwa kufanya mabadiliko lakini CC ya Chadema inapaswa kutoa kauli kuhusu ushiriki wao.
Pili, je mbunge wa Arusha anahusika vipi na amechukuliwa hatua gani. Kama uwajibikaji wake akiwa mjumbe wa Halamshauri ya jiji la Arusha ungekuwa sahihi mambo yasingefikia hapo yalipofikia. Yeye angekuwa kiungo muhimu sana kwa mawasiliano kati ya makao makuu na madiwani.
Nadhani inabidi CC itolee kauli kuhusu ushiriki wake vinginevyo itakuwa ni
double standard.
Mwisho, je muundo wa Chadema upo kamilifu? Vinginevyo habari hizi zisingekuwa za mshtuko, na hii inapelekea niamini kuwa kuna vitengo ndani ya chama haviwajibiki. Utamaduni wa kuunda tume ni ishara ya uzembe kama tunavyoona ndani ya CCM na serikali yake.
Haiwezekani chama chanye sekretariati na CC vishindwe kuelewa nini kinaendelea katika
political sphere hasa mambo ndani ya chama chao.
Kuna umuhimu wa Chadema kurejea utendaji wa vitengo vyake na wawepo watu makini zaidi. Chama hakiendeshwi na tume bali
facts and principles
Ahsante