Uamuzi wa kumsimamisha Abdallah Kambuzi ulifanywa kimihemko kwa maslahi ya nani?!!!!

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001

Nimetazama Azam TV Kipindi cha Kipyenga cha Mwisho. Othmani Kazi amechambua kwa kina na kitaalamu sana mechi ya KMC dhidi ya Simba Sc.

Hii ni mechi iliyolalamikiwa sana na wapinzani wa Simba Sc kiasi cha kufanya waaamuzi wa mchezo huu kusimamishwa.

Naungana na Kipyenga cha mwisho kwamba Kambuzi ameonewa na mamlaka zimefanya uamuzi kwa msukumo,mhemko na kukurupuka.

Nimekuwa najiuliza je waliomsimamisha Kambuzi walipata muda wa kutosha kuchambua matukio pamoja na kupata maoni ya wadau? Au walizingatia kiwango cha kelele za Yanga?

Huo muda waliupata lini kama walimfungia ndani ya masaa takribani nane tu toka achezeshe mpira?

Niwashauri marefu wasijawe na uoga wa kufanya maamuzi,wazingatie sheria 17 za mchezo na sio kelele cha chura. Nawasisitiza hivyo kwa sababu ujinga unaofanywa na Yanga umeanza kutia wasiwasi waamuzi kuhofia kutoa penati kwa Simba. Tumeona jana mchezaji mahiri Emma Okwi akifanyiwa faulo ya wazi ndani ya eneo hatari.

Kelele za Yanga ni kutapatapa kwa mtu anayekaribia kifo. We umewahi kuona wapi,eti wanalalamika kwa nini lile goli la free kick dhidi ya Mbeya City amepewa Meddie Kagere badala ya Zimbwe Jr Shabalala??
 
Njaa sio mzur mkuu, waache watapetape, ila dawa itawaingia tu
 
Tff ni kama gari lililo katika stelingi. Linaenda shagala bagala. Wao wana sikiliza ujinga wa yanga badala ya kusimamia sharia? Mbona simba hawalalamiki kupangiwa mechi kila baada ya siku 1 kama sio hujuma ni nini?
 
Kocha Wa Mbeya City Analalamika Simba Wamebebwa Na Refa, Faulo Ya Goli La Pili La Simba Haikuwa Halali, Simba Wanaharibu Sana Ligi Kwa Rushwa Zao
 
Kwa hiyo?
 
Kocha Wa Mbeya City Analalamika Simba Wamebebwa Na Refa, Faulo Ya Goli La Pili La Simba Haikuwa Halali, Simba Wanaharibu Sana Ligi Kwa Rushwa Zao
Alivyo angushwa okwi hakuona! Simba wamenyimwa penalt ya wazi kwenye hiyo mechi. Marefa wa ligi yetu wanamapungufu tu, ila kutumia mapungufu yao kutetea vichapo ni upungufu wa makocha pia.
 
Makocha wa timu nyingi wanaongea saaana kuhusu marefa hassa wakicheza Simba. Eti mpira wa miguu hautafika mbali Tanzania kama marefa wanachezesha vile. Cha ajabu Timu zao ziko hovyo kabisa .. wanakamia mechi kubwa tu. Mechi ya jana Mbeya city ilikamia saana na walicheza mpira wa nguvu mara machache walitumia akili. Walistahili kadi sio chini ya 2 nyekundu na penalti halali walinyimwa Simba. Tff wataharibu kuwasikiliza makocha waliofeli kuwaadhibu waamuzi bila kukaa na kutafakari. Simba inacheza mechi kila siku 2 nayo siyo sawa kabisa eti viporo Kwani Simba ndio waliopanga ratiba?? Tff imefeli tangia mwanzoni kupanga ratiba uliona wapi timu inacheza mechi kumi mfululizo nyumbani. Makocha walioshindwa maisha wasije kuwa tabu kwenye soka letu na wengine wanawasema hovyo wachezaji wao kwa majina mbele vyombo vya habari... hii taaluma gani kama sio ujinga. Juzi kocha wa Prisons Adolf Richard aliongea kiutu uzima nampa bug up hakutaka ujinga.
 
Tff ni kama gari lililo katika stelingi. Linaenda shagala bagala. Wao wana sikiliza ujinga wa yanga badala ya kusimamia sharia? Mbona simba hawalalamiki kupangiwa mechi kila baada ya siku 1 kama sio hujuma ni nini?
Wewe ningekutukana. . Sheria ya FIFA mechi zichezwe kila baada ya masaa 72..cha ajabu Mikia walikuwa wanakaa zaidi ya siku 12 bila ya kucheza. Wakati DRC, Egypt, South Africa nk Hakuna viporo 11..sisi ni watu wa ovyo kabisa katika Dunia hii.
 
Inamaana hawa taki Simba iwe Bingwa tena ??
 
Waacheni Yanga watape tape

Tunahitaji kushinda mechi sita kati ya Tisa tuwe Mabingwa bila ya kujali wao watashinda ngapi
 
Naona hizi lawama, kelele na malalamiko kuhusu upendeleo kwa Simba umewakera sana Simba...Wanasimba wengi wanajitokeza kutetea malalamiko yanayojitokeza...Simba fans and leaders are on defensive....Huyo Othman Kazi naye ni Simba kwani inafahamika hivyo...wengi pia wanafahamu matatizo yaliyokuwa yakimpata huyo Ndugu wakati alipokuwa refa...Binafsi siamini kuwa huyo Ndugu ni mtu sahihi kweli kuchambua masuala hayo 'kipyenga cha mwisho'...kwa hakika uchambuzi hautendewi haki kabisa....
 
Alivyo angushwa okwi hakuona! Simba wamenyimwa penalt ya wazi kwenye hiyo mechi. Marefa wa ligi yetu wanamapungufu tu, ila kutumia mapungufu yao kutetea vichapo ni upungufu wa makocha pia.
Kama hiyo penati ingekuwa kafanyiwa madhambi mchezaji wa Mbea City na kunyimwa penati ungewasikia Yanga na Zahera wanavyolalamika.
 
waliomsimamisha kambuzi.waliangalia zile clips za lawama alizo kuwa anazirusha Mchambuzi janja janja shaffi mtoto wa dawda
 
Kocha Wa Mbeya City Analalamika Simba Wamebebwa Na Refa, Faulo Ya Goli La Pili La Simba Haikuwa Halali, Simba Wanaharibu Sana Ligi Kwa Rushwa Zao
Mnataka mpira uendeshwe vipi, mnataka hata mchezaji wa simba akivunjwa mguu refa apete, sheria za mpira hamjui but kutwa kulaumu vitu visivo na msingi,
 
Vipoli 11, ama kweli soka la bongo ni kama siasa za chama kimoja..
 
Wewe ningekutukana. . Sheria ya FIFA mechi zichezwe kila baada ya masaa 72..cha ajabu Mikia walikuwa wanakaa zaidi ya siku 12 bila ya kucheza. Wakati DRC, Egypt, South Africa nk Hakuna viporo 11..sisi ni watu wa ovyo kabisa katika Dunia hii.
Tatizo sio simba ni tff , yanga alicheza mechi 12 nyumbani mbona hamkusema, saivi simba anacheza mechi after one day unahisi ni sawa? Unapotoa point usiwe bias ndugu!! Kocha enu anajifanya kujua kumbe hajui
 
Sasa uyo Othuman kazi sindó wale wale tu marefa wa mbumbumbu fc
 
Wamrudishe kambuzi haraka kabla sijawatokea huko tiefu efu..ohooo hawanijui vizuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…