OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Nimetazama Azam TV Kipindi cha Kipyenga cha Mwisho. Othmani Kazi amechambua kwa kina na kitaalamu sana mechi ya KMC dhidi ya Simba Sc.
Hii ni mechi iliyolalamikiwa sana na wapinzani wa Simba Sc kiasi cha kufanya waaamuzi wa mchezo huu kusimamishwa.
Naungana na Kipyenga cha mwisho kwamba Kambuzi ameonewa na mamlaka zimefanya uamuzi kwa msukumo,mhemko na kukurupuka.
Nimekuwa najiuliza je waliomsimamisha Kambuzi walipata muda wa kutosha kuchambua matukio pamoja na kupata maoni ya wadau? Au walizingatia kiwango cha kelele za Yanga?
Huo muda waliupata lini kama walimfungia ndani ya masaa takribani nane tu toka achezeshe mpira?
Niwashauri marefu wasijawe na uoga wa kufanya maamuzi,wazingatie sheria 17 za mchezo na sio kelele cha chura. Nawasisitiza hivyo kwa sababu ujinga unaofanywa na Yanga umeanza kutia wasiwasi waamuzi kuhofia kutoa penati kwa Simba. Tumeona jana mchezaji mahiri Emma Okwi akifanyiwa faulo ya wazi ndani ya eneo hatari.
Kelele za Yanga ni kutapatapa kwa mtu anayekaribia kifo. We umewahi kuona wapi,eti wanalalamika kwa nini lile goli la free kick dhidi ya Mbeya City amepewa Meddie Kagere badala ya Zimbwe Jr Shabalala??