Niliposema maandalizi ya kutosha yafuatayo aghalabu ni muhali hadi sasa kujulikana:-
1 Je, nani anajuwa takwimu halisi za idadi ya Wamachinga nchini? Mwaka 1995 wale wanaotembeza bidhaa (acha wanaotandika bidhaa chini idadi yao ilikuwa sawa na idadi ya watu wa Mwanza Mjini, over 8K)
2. Je, kuna sera, mwongozo kuhusu Wamachinga kwa miaka yote 36 tangu 1985? Kama havipo, tunahitaji miongo mingapi mbele kuandaa tools hizo?
3. Je, soko la Machinga Complex limeleta matokeo gani (kabla ya Kariakoo kuungua vizimba vilikuwa wazi kwa miaka nenda).
4. Je, kuna sensa ya Wamachinga imefanyika? Wako wangapi? Wanawake wangapi? Wanaume wangapi? Drop outs wangapi waliojiunga na Umachinga? Idadi kwa kila mji nchi nzima ni ngapi (ili wasije kuelemea Dar)? Graduates wangapi? Watanzania wangapi? Wachina wangapi? idadi kwa makabila ikoje ili tujuwe mkoa upi hauna mikakati ya kuwa-absorb wasije Dar? nk.
5. Je, Umachinga siyo jibu la madai ya taifa ya kutaka watu wajiajiri? Lkn katika mazingira gani?
6. Je, kuna sehemu zimeandaliwa za kuwameza wote waondoke mitaani?
7. Je, after-effects za kuwaondoa kwa dharura tumezipima tukazijuwa ni zipi na namna gani tumejiandaa kuzimitigate?
8. Wamachinga wako maeneo mengi hata China, Nairobi Kikomba wako tangu enzi za Jomo Kenyatta.