Uamuzi wa kuwaondoa Machinga mitaa ya Dar es Salaam urejewe upya

Uamuzi wa kuwaondoa Machinga mitaa ya Dar es Salaam urejewe upya

Kuwajua number yao si kupitia vitambulishio vyao vya biashara?
 
Kwani mkuu machinga ni nani? Kwa tulikokiwa tumefikia wamachinga walikuwa ni wale wote waliokuwa wanakwepa gharama za kufanya biashara ikiwa ni pamoja na kodi. Nahisi ulikuwa miongoni mwao.
Niliposema maandalizi ya kutosha yafuatayo aghalabu ni muhali hadi sasa kujulikana:-

1 Je, nani anajuwa takwimu halisi za idadi ya Wamachinga nchini? Mwaka 1995 wale wanaotembeza bidhaa (acha wanaotandika bidhaa chini idadi yao ilikuwa sawa na idadi ya watu wa Mwanza Mjini, over 8K)

2. Je, kuna sera, mwongozo kuhusu Wamachinga kwa miaka yote 36 tangu 1985? Kama havipo, tunahitaji miongo mingapi mbele kuandaa tools hizo?

3. Je, soko la Machinga Complex limeleta matokeo gani (kabla ya Kariakoo kuungua vizimba vilikuwa wazi kwa miaka nenda).

4. Je, kuna sensa ya Wamachinga imefanyika? Wako wangapi? Wanawake wangapi? Wanaume wangapi? Drop outs wangapi waliojiunga na Umachinga? Idadi kwa kila mji nchi nzima ni ngapi (ili wasije kuelemea Dar)? Graduates wangapi? Watanzania wangapi? Wachina wangapi? idadi kwa makabila ikoje ili tujuwe mkoa upi hauna mikakati ya kuwa-absorb wasije Dar? nk.

5. Je, Umachinga siyo jibu la madai ya taifa ya kutaka watu wajiajiri? Lkn katika mazingira gani?

6. Je, kuna sehemu zimeandaliwa za kuwameza wote waondoke mitaani?

7. Je, after-effects za kuwaondoa kwa dharura tumezipima tukazijuwa ni zipi na namna gani tumejiandaa kuzimitigate?

8. Je, Wamachinga ni matokeo au zao la mfumo wa elimu tulio nao?

9. Je, Wamachinga ni zao la Economic Model inayoongoza nchi/dunia?

10. Je, Mamlaka za Kodi zime-engage vipi Wamachinga kwenye mfumo wa kodi maana wako wengi sana?

11. Je, kwanini hakuna Sheria ya Bunge (Act of Parliament) inayoratibu shughuli za Wamachinga kwa tija ya taifa? Ikumbukwe idadi yao ambayo hatujaijuwa ni kubwa kiasi kwamba taifa halipaswi kukosa sheria ya kuwaratibu zaidi ya ile sheria ya uzururaji inayobana madadapoa na mission-town (wapiga misele).

12. Je, Sheria ya Nguvu Kazi ya 1984 inasema nini kuhusu Wamachinga? Au wakati sheria hiyo inatungwa Wamachinga hawakuwepo lakini kwamba sasa wapo ni kwanini sheria hiyo isifanyiwe marekebisho ili iwaongelee na wao pia?

13. Je, kwakuwa Umachinga ni zao la mfumo-liberali wa dunia hasa kwenye uchumi ambapo Ujamaa uliokuwa unasisitiza dola kuzalisha na kuwalisha je, ujio wa mfumo mpya uliowazalisha (siyo Ujamaa) unaowataka wale kwa jasho lao umewaandaliaje mazingira wezeshi na jumuishi ili waendelee kula kwa jasho lao wasijekuitegemea dola?

14. Nachelea kuamini kwamba kama sensa ya Wamachinga nchini ikifanyika idadi yao itazidi idadi ya watu wa Zanzibar (1.5ml), watu wa Shelisheli (0.9ml) na huenda ikakaribiana na idadi ya watu wa Lesotho na Eswatini kwa pamoja.

NB.
Fikiria, taifa liwe na kundi dogo la watu wa idadi ya nchi za Eswatini/Lesotho ambao hawalipi kodi kutokana na kwamba hakuna mazingira/mfumo wezeshi yaliyoandaliwa kwa ajili yao kulipa kodi na tozo za serikali? Baghosha!

Wamachinga wako maeneo mengi hata China, Nairobi Kikomba wako tangu enzi za Jomo Kenyatta.

R.e1ec613adc84bf0605423d19b716e466

Taswira kwa hisani ya google
 
Sisi hatuna tatizo la ajira hata kidogo kiasi Cha kuulizana maswali magumu kuhusu watu wanaaovamia barabara za magari, njia za waenda kwa miguu na njia za maji. Tanzania ardhi IPO ya kulima, kufuga, kuchimba madini, kuvua na kufanyia biashara. Ardhi ni Mali ya serikali na IPO tele kabisa kila mahali. Vijana wetu waelimishwe kuhusu kanuni na taratibu za kulima, kufuga, kuvua, kuchimba madini, na kufanyabiashara ili tukaijaze ardhi yote kwa uwekezaji kabla wageni hawajaivamia kwa kisingizio Cha uwekezaji huku watu wakitandika chini bidhaa za kichina kuuza.

Lazima tufanye hivyo Leo sio kesho kwakuwa maeneo yapo na fursa zipo.

Tuongelee habari za mikopo na elimu ya uzalishaji kwa wajasiliamali lakini sio kutetea watu walioziba njia zote, vituo vyote vya mabasi na mitaro yote ya majitaka. Leo hii stendi zote za dalala zimewekwa meza, mikokoteni na miamvuli watu wanauza miwa, sigara, machungwa, handcachifu, mafenesi, nk. Hakuna nchi ya hovyo nyingine kama hii.
 
Uamuzi wa kuondoa wafanyabiashara wadogowadogo almaarufu Machinga 18 Oktoba, kwa maoni yangu una gharama kubwa kuliko faida/manufaa na kwamba unastahili kupitiwa/kudurusiwa upya. Gharama ziko kiuchumi, kijamii, kiusalama na kisiasa. Sipingani na uamuzi huo, ni mzuri tu, isipokuwa nadhani maandalizi zaidi yanahitajika ili zoezi liwe na tija kwa pande zote husika.

Hawaondolewi bali wanapangwa kwenda sehemu sahihi ,haiwezekani mfanyabiashara anapanga bidhaa zake katikati ya barabara ,ajenga banda juu ya mtaro ,wapita njia wanapata tabu ,mitaro michafu na kusababisha magonjwa ya milipuko,ajali ,sasa kipi cha umuhimu afya ya jamii au uchumi? Hata hapo unapoona k/kkoo palipangwa ,hata huko wanapopelekwa watakaa vizuri tu na wateja wataenda huko bila shurti.

Naipongeza serikali kwa uamuzi mzuri wa kuwapanga wamachinga maana walikuwa KERO sana!! Serikali isirudi nyuma kwenye hili,mwezi mzima umetosha kujipanga,wanaboa sana wanavyozuia njia,wamejenga hadi kwenye mitaro yaani kupita ni shida inabidi upie kwenye lami ambapo ni hatari sana,karibu na mitar huwa kuna njia za watembea kwa miguu ila zote zile occupied na mabanda yao....Ni shida watoke tu.
 
Kama Wana bidhaa muhimu na zinazohitajika kwa watu wateja watawafuata TU popote watakakokwenda kufanyia biashara zao. Hata Babu wa Loliondo alipata wateja wengi sana ingawa kwake kilikuwa hakuna barabara Wala mawasiliao ya simu. Hivyo, serikali isipate shida ya kuwapangia wamachinga ambao walivamia wenyewe maeneo. Kazi ya serikali za miji ni kufuata mipangomiji Yao basi. Kila anaetaka kufanya biashara aende akamuone afisa biashara wa eneo husika ili ampe vigezo na masharti ya Biashara anayotaka kufanya.
 
Hakuna madhala yoyote labda kisiasa machinga hawachangii lolote ktk uchumi wa nchi ..
Wanasiasa wanawaofia wamachinga km mtaji wa kisiasa lkn ukweli ni kwamba kuendelea kuwabembeleza ni kupoteza nguvu kazi watanzania umachinga wetu ni kilimo huko ndio kwenye ajira za uwahika km serikali inaamua kuweka mazingira mazuri ya kilimo na masoko hakuna kazi inayoitwa umachinga duniani
Uko sahihi. Sijui kama viongozi huwa wanatafakari kuona kijana mwenye nguvu za kutunza shamba au mifugo kwa faida anatembeza saa na handkerchief kutoka china. Kikubwa Barabara zijengwe maeneo ya mashambani vijana wajiajiri kwenye kilimo na mifugo.
 
Uamuzi wa kuondoa wafanyabiashara wadogowadogo almaarufu Machinga 18 Oktoba, kwa maoni yangu una gharama kubwa kuliko faida/manufaa na kwamba unastahili kupitiwa/kudurusiwa upya. Gharama ziko kiuchumi, kijamii, kiusalama na kisiasa. Sipingani na uamuzi huo, ni mzuri tu, isipokuwa nadhani maandalizi zaidi yanahitajika ili zoezi liwe na tija kwa pande zote husika.
Madhara ya kiuchumi ni kua uchumi utapanda maana walipa kodi watafanya biashara zaidi kwani maduka yao yataonekana mbele ya wateja
 
Uamuzi wa kuondoa wafanyabiashara wadogowadogo almaarufu Machinga 18 Oktoba, kwa maoni yangu una gharama kubwa kuliko faida/manufaa na kwamba unastahili kupitiwa/kudurusiwa upya. Gharama ziko kiuchumi, kijamii, kiusalama na kisiasa. Sipingani na uamuzi huo, ni mzuri tu, isipokuwa nadhani maandalizi zaidi yanahitajika ili zoezi liwe na tija kwa pande zote husika.
Safi sana mkuu,
Ila kuna tatizo lingine kariakoo linakuja kwa kasi sana na linaweza kuwa na matokeo mabaya sana kila likicheleweshwa kuchukuliwa hatua mapema, nalo ni malori kati kati ya kariakoo
Hili ni tatizo na linakuwa kwa kasi sana na kwa kuwa wewe unaonekana una uwezo wa kupangilia hoja hembu tusaidie kuliwekea uzi ili watu wachangie huwenda wahusika wakalisikia na kulifanyia kazi
Natanguliza shukurani
 
Niliposema maandalizi ya kutosha yafuatayo aghalabu ni muhali hadi sasa kujulikana:-

1 Je, nani anajuwa takwimu halisi za idadi ya Wamachinga nchini? Mwaka 1995 wale wanaotembeza bidhaa (acha wanaotandika bidhaa chini idadi yao ilikuwa sawa na idadi ya watu wa Mwanza Mjini, over 8K)

2. Je, kuna sera, mwongozo kuhusu Wamachinga kwa miaka yote 36 tangu 1985? Kama havipo, tunahitaji miongo mingapi mbele kuandaa tools hizo?

3. Je, soko la Machinga Complex limeleta matokeo gani (kabla ya Kariakoo kuungua vizimba vilikuwa wazi kwa miaka nenda).

4. Je, kuna sensa ya Wamachinga imefanyika? Wako wangapi? Wanawake wangapi? Wanaume wangapi? Drop outs wangapi waliojiunga na Umachinga? Idadi kwa kila mji nchi nzima ni ngapi (ili wasije kuelemea Dar)? Graduates wangapi? Watanzania wangapi? Wachina wangapi? idadi kwa makabila ikoje ili tujuwe mkoa upi hauna mikakati ya kuwa-absorb wasije Dar? nk.

5. Je, Umachinga siyo jibu la madai ya taifa ya kutaka watu wajiajiri? Lkn katika mazingira gani?

6. Je, kuna sehemu zimeandaliwa za kuwameza wote waondoke mitaani?

7. Je, after-effects za kuwaondoa kwa dharura tumezipima tukazijuwa ni zipi na namna gani tumejiandaa kuzimitigate?

8. Je, Wamachinga ni matokeo au zao la mfumo wa elimu tulio nao?

9. Je, Wamachinga ni zao la Economic Model inayoongoza nchi/dunia?

10. Je, Mamlaka za Kodi zime-engage vipi Wamachinga kwenye mfumo wa kodi maana wako wengi sana?

11. Je, kwanini hakuna Sheria ya Bunge (Act of Parliament) inayoratibu shughuli za Wamachinga kwa tija ya taifa? Ikumbukwe idadi yao ambayo hatujaijuwa ni kubwa kiasi kwamba taifa halipaswi kukosa sheria ya kuwaratibu zaidi ya ile sheria ya uzururaji inayobana madadapoa na mission-town (wapiga misele).

12. Je, Sheria ya Nguvu Kazi ya 1984 inasema nini kuhusu Wamachinga? Au wakati sheria hiyo inatungwa Wamachinga hawakuwepo lakini kwamba sasa wapo ni kwanini sheria hiyo isifanyiwe marekebisho ili iwaongelee na wao pia?

13. Je, kwakuwa Umachinga ni zao la mfumo-liberali wa dunia hasa kwenye uchumi ambapo Ujamaa uliokuwa unasisitiza dola kuzalisha na kuwalisha je, ujio wa mfumo mpya uliowazalisha (siyo Ujamaa) unaowataka wale kwa jasho lao umewaandaliaje mazingira wezeshi na jumuishi ili waendelee kula kwa jasho lao wasijekuitegemea dola?

14. Nachelea kuamini kwamba kama sensa ya Wamachinga nchini ikifanyika idadi yao itazidi idadi ya watu wa Zanzibar (1.5ml), watu wa Shelisheli (0.9ml) na huenda ikakaribiana na idadi ya watu wa Lesotho na Eswatini kwa pamoja.

NB.
Fikiria, taifa liwe na kundi dogo la watu wa idadi ya nchi za Eswatini/Lesotho ambao hawalipi kodi kutokana na kwamba hakuna mazingira/mfumo wezeshi yaliyoandaliwa kwa ajili yao kulipa kodi na tozo za serikali? Baghosha!

Wamachinga wako maeneo mengi hata China, Nairobi Kikomba wako tangu enzi za Jomo Kenyatta.

R.e1ec613adc84bf0605423d19b716e466

Taswira kwa hisani ya google
Hizi ni siasa . Watu wakae kwa mipango Na miji iendelee kupanuka , huduma watu watawafuata sehemu walipo. Ni vizuri katikati ya majiji pawe na maduka ya jumla tu. Rejareja zirudi kwenye mitaa midogo na nje ya miji ili kupanua huduma na biashara.
 
Tangu utawala wa Mkapa mpaka sasa kila siku wamachinga wanaomba muda kujiandaa.
Huwezi kumwacha mtu ajenge kibanda mtaroni kisha ili tu umfurahishe.
Wanaharibu barabara.
Ni lini nasi Tanzania tutakuwa na mazingira safi?
 
Uamuzi wa kuondoa wafanyabiashara wadogowadogo almaarufu Machinga 18 Oktoba, kwa maoni yangu una gharama kubwa kuliko faida/manufaa na kwamba unastahili kupitiwa/kudurusiwa upya. Gharama ziko kiuchumi, kijamii, kiusalama na kisiasa. Sipingani na uamuzi huo, ni mzuri tu, isipokuwa nadhani maandalizi zaidi yanahitajika ili zoezi liwe na tija kwa pande zote husika.
Hahaaa!!mkuu zoezi limeshashika kasi tena maeneo mengi hasa wale wenye mabanda, wameshaanza kuyavunja wenyewe kwani wanajua nini kinaweza tokea baada ya tarehe hiyo, wewe tena una taka kurudisha mambo nyuma tena jamani?
 
Uamuzi wa kuondoa wafanyabiashara wadogowadogo almaarufu Machinga 18 Oktoba, kwa maoni yangu una gharama kubwa kuliko faida/manufaa na kwamba unastahili kupitiwa/kudurusiwa upya. Gharama ziko kiuchumi, kijamii, kiusalama na kisiasa. Sipingani na uamuzi huo, ni mzuri tu, isipokuwa nadhani maandalizi zaidi yanahitajika ili zoezi liwe na tija kwa pande zote husika.
Wamachinga wapo kwa mujibu wa sheria????
Tuanzie hapa
 
Huyu jamaa sijui alikuwa kwenye usingizi wa pono. Hapo kuna point gani jameni
Waondoke TU, tutawafuata hukohuko watakakoenda. Mfano, kama Mayai makubwa na yenye kiini Cha njano yatapatikana kwa wingi na bei nafuu huko mbondole kwa wamachinga wakaanga chips wote dar es Salaam watawafuata hukohuko mbondole
 
Good writtings though, walikuwa wapi waliponza kuingina kidogo kidogo hadi kufikia hivi sasa. Influx kubwa ilikuja Rais aliepita aliposema hoadharani waachwe wafanye biashara zao, madhara yalipimwa? je ukusanyaji wa kodi ulikuwaje kwa maduka yenye leceni? kodi zilishuka kwa kiasi kikubwa. Je tuendelee na huu utitiri wa machinga mitaani hadi mfanye research na upate matokeo ndio action ifanyike? Hiyo ni long route the answer. Tuiache serikali ifanye inachoona kinafaa nawaunga mkono kwa asilimia zote. Umetoa mifano kote nimefika huwezi kuta Nairo city center ipo kama Dar es Salaam no way. Narudia tuache cheap politics.

Mkuu Douglas Majwala hongera kwa Kujenga hoja. Hivi mkuu unafanya PhD mahali fulani? Hivi majuzi niliziona tena hoja zako chokonozi kuhusu "Nani ni Rais bora zaidi ambaye tumeshakuwa naye hapa Tanzania" Niseme tu kwamba uandisi kama huu na hoja fikirishi unazoziibua wewe pamoja na Great Thinker wengine zinaifanya JF iwe pia darasa la baadhi yetu

Tafadhali usiwe na hasira unaposoma hoja za Douglas Majwala
Mkuu Douglas Majwala Hongera sana
Tafakari haya:-

1. Je, Wamachinga ni matokeo au zao la mfumo wa elimu tulio nao?

2. Je, Wamachinga ni zao la Economic Model inayoongoza nchi na sayari?

3. Je, Mamlaka za Kodi zime-engage vipi Wamachinga kwenye mfumo wa kodi maana wako wengi sana?

4. Je, kwanini hakuna Sheria ya Bunge (Act of Parliament) inayoratibu shughuli za Wamachinga kwa tija ya taifa? Ikumbukwe idadi yao ambayo hatujaijuwa ni kubwa kiasi kwamba taifa halipaswi kukosa sheria ya kuwaratibu zaidi ya ile sheria ya uzururaji inayobana madadapoa na mission-town (wapiga misele).

5. Je, Sheria ya Nguvu Kazi ya 1984 inasema nini kuhusu Wamachinga? Au wakati sheria hiyo inatungwa Wamachinga hawakuwepo lakini kwamba sasa wapo ni kwanini sheria hiyo isifanyiwe marekebisho ili iwaongelee na wao pia?

6. Je, kwakuwa Umachinga ni zao la mfumo-liberali wa dunia hasa kwenye uchumi ambapo Ujamaa uliokuwa unasisitiza dola kuzalisha na kuwalisha je, ujio wa mfumo mpya uliowazalisha (siyo Ujamaa) unaowataka wale kwa jasho lao umewaandaliaje mazingira wezeshi na jumuishi ili waendelee kula kwa jasho lao wasijekuitegemea dola?

7. Nachelea kuamini kwamba kama sensa ya Wamachinga nchini ikifanyika idadi yao itazidi idadi ya watu wa Zanzibar (1.5ml), watu wa Shelisheli (0.9ml) na huenda ikakaribiana na idadi ya watu wa Lesotho na Eswatini kwa pamoja.

8. Je, mbona uamuzi wa kuwaondoa huwa unafanyika tu baada ya uchaguzi na serikali kusimikwa? Karibu na uchaguzi hawaondolewi? Serikali inakuwa wapi? Bajeti ya kuwaondoa kipindi hicho inakuwa wapi?

9. Mbona ilani za uchaguzi hazisemi moja kwa moja kwamba tukishika madaraka ya nchi tutawaondoa Wamachinga; ili utekelezaji wa kuwaondoa unapofanyika basi ionekane wazi kwamba Ilani inatekelezwa?

10. Je, kama Wamachinga wanachafua miji vipi magereji na vituo holela vya mafuta kwenye makazi vinapamba miji?

11. Pana tofauti gani kati ya Wamachinga waliovamia mitaa nchi nzima na watu waliowekeza na kuishi kwenye hifadhi za barabara za Tanroads na Tarura nchi nzima kwa miaka nenda miaka rudi?

12. Wamachinga walianza mwaka 1985. Wakati wa uchaguzi 1990 Wamachinga hawakuondolewa, 1995 muda wa uchaguzi hawakuondolewa, 2000 muda wa uchaguzi hawakuondolewa, 2005 muda wa uchaguzi hawakuondolewa, 2010 muda wa uchaguzi hawakuondolewa, 2015 muda wa uchaguzi hawakuondolewa, 2020 hawakuondolewa muda wote wa uchaguzi na ule usio wa uchaguzi. Maswali:-

1. Tatizo ni warasimu au Wamachinga?

2. Tatizo ni Demokrasia mbovu?

3. Tatizo ni ombwe la sheria, sera, kanuni, miongozo, ubovu wa sera ya taifa ya vijana, mfumo wa elimu au nini?

4. Sheria (kama ipo) inayowaondoa muda usio wa uchaguzi kwanini isiwaondoe muda wa uchaguzi pia?

5. 2025 wakati wa mchakato wa uchaguzi hasa kampeni Wamachinga watarejea tena mitaani (na hawataguswa) kwa sababu hatuna utaratibu mzuri endelevu kuhusu Umachinga. Mama atatafuna mfupa huu bila shaka.

NB.
Fikiria, taifa liwe na kundi dogo la watu wa idadi ya nchi za Eswatini na Lesotho ambao hawalipi kodi kutokana na kwamba hakuna mazingira/mfumo wezeshi ulioandaliwa kwa ajili yao kulipa kodi na tozo za serikali? Tunayo ya kujifunza Kigali.

Athari za kuondoka Wamachinga bila maandalizi ya kutosha Kisera, Sheria, Kanuni na Miongozo husika.

Mgandamizo wa Kijamii (Social Pressure)

1. Ujambazi, Udokozi na Vibaka (Banditry, Pilfering and Thugs)

Akili iliyolala kwa kukosa cha kufanya huvutiwa na uhalifu. Uhalifu uchukuwa sura mbalimbali zikiwemo umalaya ambao utaongeza mzigo wa magonjwa kwa watu na serikali kununua madawa na vifaatiba, aidha, kuna uhalifu wa kuhujumu taasisi kupitia deals za kupiga fedha za taasisi ili watu waweze kuishi.

2. Magereza Kujaa (Prisons Runoff)

Namba moja hapo juu inazua athari za moja kwa moja kwa idara za Magereza na Mahakama na kulazimisha mahitaji ya ajira mpya za Mahakimu na Majaji wa kutosha na pia kutanua bajeti ya Magereza ambayo serikali haijajiandaa nayo.

3. Kutanuka kwa Soko la Mihadarati (Burgeoning of Drugs Market Niche)

Wengi walio mateja ni wale waliokosa cha kufanya kuingizia kipato. Wafalme wa mihadarati mbinu wanayotumia kwenye marketing yao ni kugawa fedha na mihadarati bure kwa wateja wapya kwa muda maalum ambao unatosha kuwatengenezea uraibu hawa newcomers, baada ya muda huo pesa za bure na ngada za bure zinasitishwa ili sasa ununuwe, uraibu uliotengenezewa utakusukuma kutafuta ela hata kwa kukata kiungo cha Albino au hata kumvamia Askari mwenye bunduki na kumpiga sachi ili upate ama ela au mali ya thamani ukauze ukanunue ngada ya kipimo tu cha ukucha ili arosto isikuondoe kwenye uso wa dunia.

4. Migogoro ya Familia (Household Disorders)

Wamachinga wengi wanasomesha, wamejenga, ni bima ya afya kwa ndugu zao, ni breadwinners wa familia zao na jamaa zao. Kama breadwinner akikosa cha kufanya kuleta mkate nyumbani familia itaingia kwenye mgogoro. Taifa lenye migogoro ya kifamilia halina ustawi mzuri. Umoja wa Mataifa umeweka siku maalum kimataifa ya kutafakari juu ya migogoro ya kifamilia na kuna itifaki zake.

Changamoto za Kiuchumi (Economic Challenges)

1. Mikopo (Credit Facility)

Wamachinga wengi wamekopa kwenye masoko ya mitaji ama yasiyo rasmi au yaliyo rasmi. Kuondoka kwa dharura bila fidia ya kutengenezea vizimba vipya kwenye site mpya kutayumbisha mitaji yao na biashara zao na kufanya urejeshaji wa mikopo yao kuyumba pia, masoko haya ya mitaji yatakosa uwezo mkubwa wa kuendelea kuwahudumia wakopaji wapya. Hili wakati wa Corona 2020 liliyumbisha masoko ya hisa duniani. Kenya, serikali ili-guarantee masoko haya ili yarefushe muda wa mikopo kwa mwaka mbele kuwapunguzia waliokopa athari za Corona zilizotokana na lockdown kwamba dhamana zao za mikopo zisiuzwe. Hongera SSH kwa kutenga 5bl za zoezi la ku-relocate Wamachinga hofu iko kwenye usalama wa matumizi ya fungu hili lakini pia fungu linatosha idadi kubwa ya Wamachinga nchini?

2. Nadharia ya Uhitaji na Ugavi (Theory of Demand and Supply)

Kuondoka kwa Wamachinga kutaathiri mnyororo wa ugavi (Supply Chain) ambapo wagavi watakuwa wachache na wahitaji kuwa wengi hivyo bei ya bidhaa na huduma kupanda (Price Elasticity of Demand and Supply) na kufanya uwezo wa manunuzi (Purchasing Power) ya wahitaji hasa wanyonge kuathirika, na huenda tukaona mfumuko wa bei kwenye uchumi wa nchi, ikumbukwe kuwa hatuna takwimu za sensa ya Wamachinga na huenda makisio ni kuwa idadi yao nchini huenda inazidi watu wa Zanzibar (1.5ml), watu wa Shelisheli (0.9ml) na huenda ikakaribiana na idadi ya watu wa Lesotho na Eswatini kwa pamoja. Wamachinga walikuwa wana-regulate mfumuko wa bei (Inflation) na kuruhusu nguvu za soko za uhitaji na ugavi (Demand and Supply) kinyume na sasa ambapo tutaona Business Syndicates na Cartels zikiibuka na kujifanya Mawakala wa Kudhibiti Bei (Price Control Agents). Serikali itakapowataka wenye maduka sasa kulipa kodi na tozo halali za serikali (ambazo kimsingi sipingani nazo maana zina manufaa kwangu pia) misuguano itaanza kati ya wafanyabiashara hawa na Mamlaka za Kodi na Ushuru na wimbo utabadilika kwamba serikali inanyanyasa wafanyabiashara, Afrika ndivyo tulivyo, tunapenda kuona serikali ikikosa mapato yake halali sisi pekee wafanyabiashara tupate. Aidha, Wamachinga wanategemewa na Wafanyabiashara wakubwa kabisa maarufu nchini wanaouza vinywaji laini, barafu za kulamba, vitafunwa nk. Hawa nao wanakuwa wahanga wakubwa wa kuondoka Wamachinga katikati ya miji/mitani. Wamachinga kumbe ni injini inayotegemewa na wafanyabiashara wadogo, wa kati na wakubwa kabisa licha ya mlaji tu. Mafunuo mapya hayo.

3. Kuathiri Tasnia ya Mama na Baba Lishe (Affecting Food Vending Industry)

Mama na Baba Lishe soko lao kubwa mijini ni mamilioni ya Wamachinga wanaouza bidhaa zao maeneo hayo. Mama na Baba Lishe wanategemea Wamachinga kuliko wanavyowategemea Wachina, Wahindi, Waarabu, Wakinga na Wachaga wachache waliosalia (kwa Kariakoo). Biashara za Mama & Baba Lishe na Wamachinga zinategemezana (Solution to one problem contains the seeds for the next problem. Ukiondoa Wamachinga kwa pupa umeleta tatizo la Mama na Baba Lishe ambao wengi hivi sasa wako kisheria kupitia mradi wa Majiji Salama Afrika uliofadhiliwa na UN na serikali kuhalalisha biashara zao kupitia Healthy Cities Project). Case Study: Hoteli ya Kitalii zamani Holiday Inn mkabala na Benki ya Standard Chartered jijini Dsm mwekezaji mpya alipochukuwa hoteli ile akaondoa kibanda cha Mama na Baba Lishe kilichokuwepo jirani kabisa na hoteli, kilichotokea ni kwamba wageni wake wakiwemo wa kizungu walikuwa wanalipia tu malazi hotelini lakini chakula wanawafuata Mama na Baba Lishe wale waliosukumiziwa mita kama 25 hivi, walichokuwa wakifuata wageni wale pale kwa Mama na Baba Lishe ni bei nafuu, African cuisine na wadada wazuri wa Kitz, matokeo yake wageni wale wakawa wanawaambia keep change hata $, hoteli ile ikapoteza asilimia kubwa ya mapato ya chakula hadi pale mamlaka zilipowafuata wale Mama na Baba Lishe na kuwafungia kabisa biashara ile lakini ikaathiri mamia ya wafanyakazi maofisini waliokuwa wakitegemea vibanda vile kwa sababu hawawezi kula hoteli ile ya kitalii.

4. Halmashauri za Dar Hazina Ardhi (Metropolitan Dar Land Scarcity)

Ardhi zote zimeishamilikiwa na watu, serikali ikihitaji ardhi inabidi ifidie watu iwahamishe au iende kwenye wilaya za jirani na mkoa wa Dar (Temeke inapumulia Mkuranga, Ilala inapumulia Kisarawe, Ubungo inapumulia Kibaha, Kinondoni inapumulia Bagamoyo). Population ya Wamachinga Dar pekee ni kubwa kuliko inavyofikiriwa na wanahitaji maeneo mengi ya kutosha. Mwaka 1995 idadi yao ilikuwa sawa na wakazi wa jiji la Mwanza, leo miaka 26 imepita je, idadi yao imeongezeka kiasi gani? Dar inayo ardhi hiyo?

Uzorotefu wa Kisiasa (Political Meltdown)

1. Machafuko (Mayhem)

Tunisia iliingia machafuko yaliyosambaa katika ukanda mzima wa Waarabu wa Kaskazini mwa Jangwa la Sahara na Sahel na baadaye Mashariki ya Kati kwa cheche ndogo tu ya Mmachinga aliyeuawa kwa kipigo cha Mgambo akimtuhumu kujipumzisha kwenye bustani ya ofisi za umma, ndipo jeshi kubwa la Wamachinga wakaungana kukoleza moto. Mazingira ya kwetu siyo ya Tunisia ila for knowledge and reference sake hii inatupa kioo kizuri cha kujitazamia tunaposhughulika na kikundi hiki kinachokuwa siku hadi siku bila kuwa na sera, kanuni, mwongozo au hata sheria ya kuwaratibu moja kwa moja kama wao.

2. Mtaji wa Kisiasa (Political Capital Investment)

Wanasiasa wa wastani pote duniani hupenda kutumia Wamachinga kama mtaji wa kisiasa badala ya kutumia hoja kama mtaji wa kisiasa. Nchini Kenya Wamachinga ni mtaji mkubwa kuelekea 2022 ambapo wamepewa jina la Hustlers na kutoa tafsiri kama ile ya Biblia kwenye kitabu cha Muhubiri.10:5-7 “Liko baa nililoliona chini ya jua, nalo ni kama kosa litokalo kwake yeye atawalaye; ya kuwa upumbavu huwekwa mahali pa juu sana, nao wakwasi hukaa mahali pa chini mimi nimeona watumwa (uongozi ni utumwa) wamepanda farasi, na wakuu (wenye nchi yao ndiyo wakuu) wakienda kwa miguu juu ya nchi kama watumwa” Uganda 2021 Wamachinga walikuwa kama mpira wa kona vile, wanasiasa wengine wakiwavuta kwa sanaa ya muziki wengine wakiwavuta kwa sera jadidifu. Zambia, Mhe. Lungu moja ya sababu zilizofanya akapoteza ni China-zation of Zambia Micro Economy ambayo ndiyo wamo Wamachinga kwa 100%. Mchina mchana ni Project Engineer usiku ni Waiter kwenye Chinese Restaurant, lugha ya mitaani inasema ‘wametumwa ela’ (kwa Mtz hii inatafsirika kama Professional Suicide). Siku moja nikapost hapa kwamba kuna Mchina mmoja aliwahi kushangaa kusikia kwamba Afrika kuna kitu kinaitwa fedha haramu/illicit money. Afrika Kusini Wamachinga wanatengenezewa sera yao na sheria vitakavyoratibu shughuli zao rasmi na serikali kujipatia mapato. Hii imekuja baada ya xenophobia kulipuka kila mwaka na kila awamu (kasoro ya Mandela) na hasa baada ya jumuiya za kimataifa kama SADC na AU kuweka chagizo kwa serikali ya ANC kufanya kitu kwa ajili ya ustawi wa Wamachinga. Raia wa nchi zingine walijiuza wenyewe Afrika Kusini kusaka maisha wakawa Wamachinga. Ethiopia iliyokosa sera na sheria ya kuratibu Umachinga ikashuhudia uhamiaji haramu mkubwa toka Ethiopia kwenda Afrika Kusini kupitia EAC kama njia. Hapa ndipo ninapokuja na hoja kwamba kama taifa tunaweza kuanzisha programu kabambe ya kuuza Wamachinga kama rasilimalibinadamu nje ya mipaka kwa tija ya taifa (hii siyo biashara ya utumwa bali ni labour migration protocol kwenda kwenye nchi ambazo zinaendesha chumi zao kwa mfumo wa labour intensive/mitulinga).

3. Kuibuka kwa Mivutano ya Kiitikadi za Kisiasa (Eruption of Political Ideological Tensions)

Ili Afrika Kusini ipone vizuri itahitaji kuondoa sumu kali ya hisia za mapambano ya kizalendo ya kudai ukombozi kila wakati hata baada ya ukombozi huo kupatikana; ambazo ndizo zimewajaa vijana wengi ambao ndiyo wanatengeneza kundi kubwa la Wamachinga. Aidha, Wamachinga wanaotoka nchi zingine kuzamia Afrika Kusini nao wanajifunza mienendo ya Wamachinga wa Afrika Kusini ya mapambano ya kudai ukombozi wa kiuchumi na ajira wanaporudi kwenye nchi zao. Hii hali imeziweka kwenye tahadhari kubwa nchi za Lesotho na eSwatini. Wamachinga ambao ni vijana kwa asilimia kubwa wanaongozwa na hisia kali za kutaka kuona mabadiliko katika mifumo ya maisha wanayoishi. Fursa hii ya mabadiliko inapokosekana tamaa kali (lust) ya kutafuta itikadi sahihi na mrengo sahihi inaibuka ndani yao na inapokutana na wanasiasa uchwara basi unaweza kujuwa kuwa 1 + 1 siyo lazima iwe 2 bali kutegemea mazingira inaweza kuwa hata 11. Mwenye masikio na asikie, mwenye macho na aone, asomaye na afahamu.

R.83e27eaf0fc4e8335d92d5f002b8a7b3

OIP.wrKP-8aI1XLG6NmZ1e85FwAAAA

Taswira zote kwa hisani ya google.
 
Back
Top Bottom