Uamuzi wa kuwaondoa Machinga mitaa ya Dar es Salaam urejewe upya

Uamuzi wa kuwaondoa Machinga mitaa ya Dar es Salaam urejewe upya

Kila utakapochelewa kuwaondoa ndio hali inavyozidi kuwa ghali na mbaya zaidi.

Wamachinga bado wanazalishwa kila siku na maeneo ya kuwapeleka sio mengi.

Walipaswa kuondolewa juzi sio tarehe 18 October
Nimepita maeneo mengi zoezi linaendelea kwa utulivu mkubwa na ufanisi wa hali ya juu.. Wananchi wameandaliwa vema hivyo wanabomoa kwa hiari bila shuruti
 
Mkuu, ukizungumzia masuala ya kilimo na ufugaji hakuna Kijana atakayekuelewa. Wewe leta story za kubet na kushinda milioni kadhaa utaona watakavyomiminika.
Wanasiasa wamewadanganya wananchi kwa miaka mingi sana, ndio maana Sasa hivi hakuna anaewaamini kila wanachosema. Miaka 60 ya uhuru vijijini hakuna maji, umeme, barabara Wala masoko ya mazao Yao. Hadi Leo serikali inaombwa ikanunue Mahindi ya wakulima. Bidhaa za viwandani na mafuta ni ghali zaidi vijijini kuliko mijini, Kodi ni kubwa au ileile vijijini. Hii inawafanya vijana wamiminike mijini. Watu wa vijijini walipaswa kuondolewa au kutozwa Kodi ndogo ili vitu viwe nafuu kijijini kama wanavyofanya nchi zilizoendelea.
 
Niliposema maandalizi ya kutosha yafuatayo aghalabu ni muhali hadi sasa kujulikana:-

1 Je, nani anajuwa takwimu halisi za idadi ya Wamachinga nchini? Mwaka 1995 wale wanaotembeza bidhaa (acha wanaotandika bidhaa chini idadi yao ilikuwa sawa na idadi ya watu wa Mwanza Mjini, over 8K)

2. Je, kuna sera, mwongozo kuhusu Wamachinga kwa miaka yote 36 tangu 1985? Kama havipo, tunahitaji miongo mingapi mbele kuandaa tools hizo?

3. Je, soko la Machinga Complex limeleta matokeo gani (kabla ya Kariakoo kuungua vizimba vilikuwa wazi kwa miaka nenda).

4. Je, kuna sensa ya Wamachinga imefanyika? Wako wangapi? Wanawake wangapi? Wanaume wangapi? Drop outs wangapi waliojiunga na Umachinga? Idadi kwa kila mji nchi nzima ni ngapi (ili wasije kuelemea Dar)? Graduates wangapi? Watanzania wangapi? Wachina wangapi? idadi kwa makabila ikoje ili tujuwe mkoa upi hauna mikakati ya kuwa-absorb wasije Dar? nk.

5. Je, Umachinga siyo jibu la madai ya taifa ya kutaka watu wajiajiri? Lkn katika mazingira gani?

6. Je, kuna sehemu zimeandaliwa za kuwameza wote waondoke mitaani?

7. Je, after-effects za kuwaondoa kwa dharura tumezipima tukazijuwa ni zipi na namna gani tumejiandaa kuzimitigate?

8. Je, Wamachinga ni matokeo au zao la mfumo wa elimu tulio nao?

9. Je, Wamachinga ni zao la Economic Model inayoongoza nchi/dunia?

10. Je, Mamlaka za Kodi zime-engage vipi Wamachinga kwenye mfumo wa kodi maana wako wengi sana?

11. Je, kwanini hakuna Sheria ya Bunge (Act of Parliament) inayoratibu shughuli za Wamachinga kwa tija ya taifa? Ikumbukwe idadi yao ambayo hatujaijuwa ni kubwa kiasi kwamba taifa halipaswi kukosa sheria ya kuwaratibu zaidi ya ile sheria ya uzururaji inayobana madadapoa na mission-town (wapiga misele).

12. Je, Sheria ya Nguvu Kazi ya 1984 inasema nini kuhusu Wamachinga? Au wakati sheria hiyo inatungwa Wamachinga hawakuwepo lakini kwamba sasa wapo ni kwanini sheria hiyo isifanyiwe marekebisho ili iwaongelee na wao pia?

13. Je, kwakuwa Umachinga ni zao la mfumo-liberali wa dunia hasa kwenye uchumi ambapo Ujamaa uliokuwa unasisitiza dola kuzalisha na kuwalisha je, ujio wa mfumo mpya uliowazalisha (siyo Ujamaa) unaowataka wale kwa jasho lao umewaandaliaje mazingira wezeshi na jumuishi ili waendelee kula kwa jasho lao wasijekuitegemea dola?

14. Nachelea kuamini kwamba kama sensa ya Wamachinga nchini ikifanyika idadi yao itazidi idadi ya watu wa Zanzibar (1.5ml), watu wa Shelisheli (0.9ml) na huenda ikakaribiana na idadi ya watu wa Lesotho na Eswatini kwa pamoja.

NB.
Fikiria, taifa liwe na kundi dogo la watu wa idadi ya nchi za Eswatini/Lesotho ambao hawalipi kodi kutokana na kwamba hakuna mazingira/mfumo wezeshi yaliyoandaliwa kwa ajili yao kulipa kodi na tozo za serikali? Baghosha!

Wamachinga wako maeneo mengi hata China, Nairobi Kikomba wako tangu enzi za Jomo Kenyatta.

R.e1ec613adc84bf0605423d19b716e466

Taswira kwa hisani ya google
Ni busara kuelekeza maswali yako kwa ofisa maendeleo ya jamii na ofisa biashara wa eneo husika, Hapa tunachotaka ni taratibu na sheria kuzingatiwa
 
Nilipata fursa ya kuishi marekani vijijini, wengi wetu tunaokwenda Marekani wanakwenda kuishi mijini, lakini mimi nimeishi kule vijijini kabisa kama Chelsea na kijijini zaidi ambako watu wanajikamulia wenyewe juice za apple na kuweka kwenye galoni na kuuza kiholela tu.

Ukweli ni kwamba hata Marekani wako machinga wengi sana, lakini hawa wako hukohuko vijijini. Watu kutoka mijini siku za weekeend na public holiday utaona misululu ya magari kuelekea huko vijijini kununua bidhaadh

Ok, Sir pamoja sana.

Mimi nimewahi kuishi Marekani mjini na vijijini pia. Nimeishi kwenye vijiji hasa kama Chelsea na vingine ambako wajasikiamali wadogo wanauza bidhaa zao hukohuko vijijini. Wanajikamulia wenyewe apple zao kupata juice wanazouza kwenye galoni kiholela TU kwa bei ndogo. Wamachinga kule vijijini wanauza bidhaa zenye bei nafuu sana kuliko mjini, bidhaa zao zimeondolewa Kodi mbalimbali hivyo ni rahisi sana kuliko kule mjini. Hivyo, kila weekends na public holidays utaona misululu mirefu ya magari kutoka mijini kwenda vijijini kufuata bidhaa za bei nafuu kuliko kwenye Malls.

Hivyo serikali inaweza kuondoa Kodi fulanifulani kwenye bidhaa zinazouzwa na machinga walioko kule Mlandizi, Mkuranga, kisarawe na bagamoyo ili machinga wavutike kwenda kule na wakazi wa mjini kuvutika kwenda kufanya manunuzi kule ya bei nafuu.

Mfano, kama bei ya seti ya sufuria inayouzwa laki 3 kariakoo itauzwa laki 2 kule Kisarawe kwenye maduka ya machinga watu wengi sana watakwwnda Kisarawe kununua sufuria hizo badala ya kariakoo. Tunahitaji sera na sio kutumia nguvu zaidi.

Kule Marekani bei ya bidhaa inapungua bei kutokana na mambo yafuatayo:

1. Ubora wa bidhaa
2. Umbali kutoka mjini
3. Aina ya bidhaa
4. Parking, kama sehemu haina parking na bei ya bidhaa hapo itakuwa ndogo.
5. Public transport, kama hakuna usafiri wa umma na bei iya bidhaa husika inaweza kushuka pia.

Shida yetu sisi hapa bidhaa ni rahisi mijini kuliko vijijini, bei inaongezeka kadiri mtu anavyotoka city center. Hivyo kuvuta watu kuja kariakoo kufanya biashara na kununua. Inawezekana huku kariakoo yakaweko maduka ya jumla TU basi.
Reference za namna hii zinajenga sana na kusaidia kuelewa tatizo kwa marefu, kina na mapana, endelea kutuelimisha mkuu.
 
Hii sio kweli, Kuna kijana niliwahi kumshauri arudi mkoani na kuachana na kazi ya kuuza urembo kwa njia ya kutembezea wateja kwenye kapu, alinichukia sana lakini akarudi mkoani na kuanza kazi ya kufuga kuku wa kienyeji na kulima pilipili. Sasa hivi Yuko mbali sana, ana zaidi ya kuku 1000, Bata 200 na mbuzi 100. Anauza kuku na Mayai ya kuku wa kiejeji anapata hela hata kumzidi mtu aliyeajiliwa kwa mtu, amejenga na amepanua shamba lake kwa kulima kwa Trekta. Leo hii ni rafiki yangu na ananisifu kila siku.

Vijana hawa machinga kwa kuishi hapa mjini wamepata exposure kubwa sana, wanafahamu kitu gani kinatakiwa mjini, hivyo ukiwatimua hapa na kurudi kijijini watafanya vitu vya maana sana vya kimaendeleo. Unachosema wewe ni kinyume chale.

Mfano, sisi tulikulia mjini kwenye nyumba ya serikali ambako baba alikuwa akifanyakazi, nyumba ilikuwa Ina fanicha zote, maji na umeme wa bure. Siku baba alipotuambia tunahamia nyumbani kwetu huko salasala tulimchukia sana kwa kututoa kwenye mtaa na nyumba tuliozoea. Lakini hivi Sasa tunamsifu kwa kufanya uwamuzi ule badala angesubiri kustaafu au tuondolewe baada ya baba kuacha kazi. Tulipohamia kule tukajikuta tuko kwenye nyumba yenye nafasi hata ya kucheza na kulala. Badala ya kumchukia tukamuona shujaa.

Hata machinga ukiwatimua kwenye njia za waenda kwa miguu na chini ya nyaya za umeme Leo lazima kesho watakusifu TU kwa kuwaondolea mateso na hatari.
Wazo mbadala, unafikirisha sana mchango huu.
 
Zoezi la kuwaondoa machinga lazima liwe kama military operation: lazima lianze kwa Kasi na nguvu, Kisha ifuate hatua ya kuondoa mabaki ya uchafu, Kisha uboreshaji wa maeneo ili yasiwavutie machinga kurudi na mwisho ifuate hatua ya surveillance; kuhakikisha kuwa machinga hawarudi tena kwenye mazingira hayo milele. Kazi hiyo wapewe viongozi wa mitaa kuhakikisha kuwa kwenye mitaa Yao hakuna wafanyabiashara wanaoziba njia za waenda kwa miguu na njia za maji.

Baada ya vibanda kuondolewa nilishangaa sana kuona Kuna machinga ambao waliziba mtaro kwa udogo kuufukia ili wapate kujenga juu kwa mbao. Hili ni balaa
 
Kwahiyo wewe unaona chanjo ya korona ni sahihi.. Na kama ni sahihi kwanini unasaini nakuambiwa et madhara ni juu yako? Acha bangi kabisa... Chanjo ya korona haina uhakika duniani kote.. Hii ni vita ya uchumi
Acha propaganda za uongo, watu tumechanja mbona hakukuwa na hiyo concert form inayosema madhara ni juu yako.

Na Kama issue ni concert form, hata ukiwa na mgonjwa anapohitaji kufanyiwa surgical operation, huwa kuna kujaza hizo form, je hiyo humaanidha operation ni mbaya? Na je, watu wasifanyiwe surgery kwa sababu ya kuwepo concert form?? Jamani kila taaluma ina taratibu zake, hivyo si kila kitu ni siasa.

Sent from my TECNO F3 using JamiiForums mobile app
 
Rais Samia hashauriwi vyema,

anatengeneza kundi kubwa sana la wapinzani nchini,

watu hao wakiachwa bila njia za kujipatia kipato wataichukia serikali yake.

Ni kweli tunahitaji miji misafi ila raia nao wanatakiwa kuwa huru kufanya shughuli zao.

CCM itapata wakati mgumu sana kujinadi 2025 kama hali hii ikiendelea.
Utatuzi wa kupata kura sio kuruhusu biashara sizizo rasmi na kuharibu uchumi wa nchi, hata hiyo ilani ya uchaguzi unaitekelezaje bila hela. Utatuzi unatakiwa uzingatie uhalisia, chanzo chake na utatuzi wa kudumu. Tusiende kwenye cheap politics.
 
Acha propaganda za uongo, watu tumechanja mbona hakukuwa na hiyo concert form inayosema madhara ni juu yako.

Na Kama issue ni concert form, hata ukiwa na mgonjwa anapohitaji kufanyiwa surgical operation, huwa kuna kujaza hizo form, je hiyo humaanidha operation ni mbaya? Na je, watu wasifanyiwe surgery kwa sababu ya kuwepo concert form?? Jamani kila taaluma ina taratibu zake, hivyo si kila kitu ni siasa.

Sent from my TECNO F3 using JamiiForums mobile app
Usihangaike na watu ambao kijijini kwao hawana vyoo mpaka Leo. Kama amekataa kutumia choo itakuwaje kwa chanjo ya covid-19?
 
Uamuzi wa kuondoa wafanyabiashara wadogowadogo almaarufu Machinga 18 Oktoba, kwa maoni yangu una gharama kubwa kuliko faida/manufaa na kwamba unastahili kupitiwa/kudurusiwa upya.

Gharama ziko kiuchumi, kijamii, kiusalama na kisiasa. Sipingani na uamuzi huo, ni mzuri tu, isipokuwa nadhani maandalizi zaidi yanahitajika ili zoezi liwe na tija kwa pande zote husika.
Binafsi sioni mantiki yoyote ya kuacha watu wafanye biashara barabarani... Mbona mitaani kumejaa fremu wakakodishe wauzie huko vitu vyao.
 
Binafsi sioni mantiki yoyote ya kuacha watu wafanye biashara barabarani... Mbona mitaani kumejaa fremu wakakodishe wauzie huko vitu vyao.
Wenzao wanayafuata magulio yaliko kuuza bidhaa zao wao wanapenda kuzuia kwenye njia za waenda kwa miguu, shame upon them.
 
Binafsi sioni mantiki yoyote ya kuacha watu wafanye biashara barabarani... Mbona mitaani kumejaa fremu wakakodishe wauzie huko vitu vyao.
Kweli kabisa mkuu, ila tunapowashughulikia Wamachinga tusiache kuwashughulikia/kuzishughulikia warasimu na taasisi zinazohusika na maeneo hayo na Wamachinga ambao tangu 1985 wamekuwa hawana jipya na kuwaachia Wanasiasa ndiyo washughulikie tatizo hili kisiasa huku ushughulikiaji wake kitaasisi ukiachwa tu. Kumaliza kichuguu usiue mchwa ua malkia.
 
Ubaya wa jambo hili ni kwamba hata viongozi wa serikali za mitaa, madiwani, halmashauri na Chama nao pia Wana biashara zao humo barabarani na sehemu za wazi. Hivyo hawa viongozi ndio wanaowadanganya wanasiasa kuwa hawa ndio wapiga kura wetu tusiwaondoe wasije kutunyima kura, lakini ukweli wenyewe sio huo bali conflict of interest.
 
Ngoja watoke kwanza maeneo yasio rasmi harafu tuone hiyo adhari itatoka wapi ?
 
Ubaya wa jambo hili ni kwamba hata viongozi wa serikali za mitaa, madiwani, halmashauri na Chama nao pia Wana biashara zao humo barabarani na sehemu za wazi. Hivyo hawa viongozi ndio wanaowadanganya wanasiasa kuwa hawa ndio wapiga kura wetu tusiwaondoe wasije kutunyima kura, lakini ukweli wenyewe sio huo bali conflict of interest.
Mkuu, this is very great point of all, tumekuwa tukisikia across the nation vizimba katika masoko na maeneo ya wazi ya biashara vikimilikiwa kwa siri na warasimu ambao ndiyo wanawakodishia Wamachinga, hata baadhi ya DEDs waliogundulika kushindwa kuwasimamia watendaji wao wenye tabia hii kupoteza nafasi zao za U-DED, so hii inathibitisha point yako hiyo kubwa sana.
 
Ulipaswa kufanywa kwa awamu taratibu WAMEKURUPUKA na italigharimu Taifa huo ndio ukweli wenyewe time will tell😊

Ni kweli mkuu, tatizo uliloishi nalo kwa miaka 36 tangu 1985 huwezi kuliita la dharura wala kulipa ufumbuzi wa dharura. Watu idadi yao huenda inazidi idadi ya watu wa nchi za Shelisheli, Lestho, Eswatini na Zanzibar ulione la kawaida lisilo na madhara kushughulikiwa kwa pupa. Baada ya Wamachinga tuna tatizo la bodaboda ambao nao idadi yao itaanza kuwa kubwa kwa sababu Wamachinga wengi sasa nao wanaenda kujiajiri kwenye bodaboda baada ya kuona karaha za Umachinga za kupoteza mitaji kila mara baada ya uchaguzi mkuu kukamilika. Hata bodaboda wanahitaji uratibu wa makini sana kabla hawajaielemea nchi. Yafuatayo ni madhara yatokanayo na biashara ya bodaboda ambayo hatuyaoni kwa sasa:-

1. Noise pollution (hii sasa hivi ni agenda ya dunia).

2. Emission of gases from the tailpipe of an internal combustion engine e.g. carbon monoxide (CO), hydrocarbons (HC), carbon dioxide (CO2), oxides of nitrogen (NOx). Carbon monoxide results from burned fuel. It’s an odorless, colorless, tasteless poisonous gas. Tunajuwa mafuta mengi sasa hivi ni unleaded lakini soko huria huja na uhuru wa uharibifu.

3. Security challenges. Baadhi ya waendesha bodaboda kwa wakati mmoja au mwingine wamejihusisha na uhalifu wa aina takriban zote hadi wa mauaji.

4. Mobbing. Baadhi ya waendesha bodaboda wameshiriki kwenye matukio ya uvamizi kwa njia ya Mob na kuleta taharuki kubwa na hujuma isiyofaa hiyo biashara.

5. Road accidents.

NB.
What if leo mtu akisema bodaboda zinaleta changamoto nyingi kwenye jamii hivyo kwa kuwa tuna mbadala wao kama madaladala, UBA, Taxi Fire, Borch, Taxi, Rickshaw (Bajaj), Toyo, Kirikuu, Guta, Treni za Mwakyembe, BRT, kwamba hizi zinatosha kuondoa adha zinazotokana na biashara ya bodaboda kwamba kuanzia sasa marufuku bodaboda, unadhani mapokeo yatakuwaje? Ni vivyo hivyo kwa Wamachinga ambao ni injini ya wafanyabiashara wakubwa, wa kati na wadogo na Mama na Baba Lishe.
 
Niliposema maandalizi ya kutosha yafuatayo aghalabu ni muhali hadi sasa kujulikana:-

1 Je, nani anajuwa takwimu halisi za idadi ya Wamachinga nchini? Mwaka 1995 wale wanaotembeza bidhaa (acha wanaotandika bidhaa chini idadi yao ilikuwa sawa na idadi ya watu wa Mwanza Mjini, over 8K)

2. Je, kuna sera, mwongozo kuhusu Wamachinga kwa miaka yote 36 tangu 1985? Kama havipo, tunahitaji miongo mingapi mbele kuandaa tools hizo?

3. Je, soko la Machinga Complex limeleta matokeo gani (kabla ya Kariakoo kuungua vizimba vilikuwa wazi kwa miaka nenda).

4. Je, kuna sensa ya Wamachinga imefanyika? Wako wangapi? Wanawake wangapi? Wanaume wangapi? Drop outs wangapi waliojiunga na Umachinga? Idadi kwa kila mji nchi nzima ni ngapi (ili wasije kuelemea Dar)? Graduates wangapi? Watanzania wangapi? Wachina wangapi? idadi kwa makabila ikoje ili tujuwe mkoa upi hauna mikakati ya kuwa-absorb wasije Dar? nk.

5. Je, Umachinga siyo jibu la madai ya taifa ya kutaka watu wajiajiri? Lkn katika mazingira gani?

6. Je, kuna sehemu zimeandaliwa za kuwameza wote waondoke mitaani?

7. Je, after-effects za kuwaondoa kwa dharura tumezipima tukazijuwa ni zipi na namna gani tumejiandaa kuzimitigate?

8. Je, Wamachinga ni matokeo au zao la mfumo wa elimu tulio nao?

9. Je, Wamachinga ni zao la Economic Model inayoongoza nchi/dunia?

10. Je, Mamlaka za Kodi zime-engage vipi Wamachinga kwenye mfumo wa kodi maana wako wengi sana?

11. Je, kwanini hakuna Sheria ya Bunge (Act of Parliament) inayoratibu shughuli za Wamachinga kwa tija ya taifa? Ikumbukwe idadi yao ambayo hatujaijuwa ni kubwa kiasi kwamba taifa halipaswi kukosa sheria ya kuwaratibu zaidi ya ile sheria ya uzururaji inayobana madadapoa na mission-town (wapiga misele).

12. Je, Sheria ya Nguvu Kazi ya 1984 inasema nini kuhusu Wamachinga? Au wakati sheria hiyo inatungwa Wamachinga hawakuwepo lakini kwamba sasa wapo ni kwanini sheria hiyo isifanyiwe marekebisho ili iwaongelee na wao pia?

13. Je, kwakuwa Umachinga ni zao la mfumo-liberali wa dunia hasa kwenye uchumi ambapo Ujamaa uliokuwa unasisitiza dola kuzalisha na kuwalisha je, ujio wa mfumo mpya uliowazalisha (siyo Ujamaa) unaowataka wale kwa jasho lao umewaandaliaje mazingira wezeshi na jumuishi ili waendelee kula kwa jasho lao wasijekuitegemea dola?

14. Nachelea kuamini kwamba kama sensa ya Wamachinga nchini ikifanyika idadi yao itazidi idadi ya watu wa Zanzibar (1.5ml), watu wa Shelisheli (0.9ml) na huenda ikakaribiana na idadi ya watu wa Lesotho na Eswatini kwa pamoja.

NB.
Fikiria, taifa liwe na kundi dogo la watu wa idadi ya nchi za Eswatini/Lesotho ambao hawalipi kodi kutokana na kwamba hakuna mazingira/mfumo wezeshi yaliyoandaliwa kwa ajili yao kulipa kodi na tozo za serikali? Baghosha!

Wamachinga wako maeneo mengi hata China, Nairobi Kikomba wako tangu enzi za Jomo Kenyatta.

R.e1ec613adc84bf0605423d19b716e466

Taswira kwa hisani ya google
Jambo lililomshinda Rais Magufuli HAKUNA. Narudia HAKUNA kiongozi yeyote wa wakati huu anayeweza kuliweza.
 
Mnadekeza wachuuzi wasiokuwa na faida kuja mjini huku mkiimiza kilimo ni uti wa ngono mkiwaacha utitiri wa vijana kuja kuleta uchafu wa mji kwa kujaza mambao mitaani na kuharibu miundo mbinu. Wafukuzeni warudi kwao wakulima wakina mjini waje kama wafanyabiashara walipe kodi sitahiki wachangie maendeleo ya taifa. Hasara za kuzoa taka wanazozizalisha hazilingani na faida tunayopata kutokana na kuwepo kwao. Wafanyabiashara waliozibiwa njia , zuio la parking huenda vikapandisha mapato ya mikoa iliyoathirika na zoezi la machinga
 
Ni kweli mkuu, tatizo uliloishi nalo kwa miaka 36 tangu 1985 huwezi kuliita la dharura wala kulipa ufumbuzi wa dharura. Watu idadi yao huenda inazidi idadi ya watu wa nchi za Shelisheli, Lestho, Eswatini na Zanzibar ulione la kawaida lisilo na madhara kushughulikiwa kwa pupa. Baada ya Wamachinga tuna tatizo la bodaboda ambao nao idadi yao itaanza kuwa kubwa kwa sababu Wamachinga wengi sasa nao wanaenda kujiajiri kwenye bodaboda baada ya kuona karaha za Umachinga za kupoteza mitaji kila mara baada ya uchaguzi mkuu kukamilika. Hata bodaboda wanahitaji uratibu wa makini sana kabla hawajaielemea nchi. Yafuatayo ni madhara yatokanayo na biashara ya bodaboda ambayo hatuyaoni kwa sasa:-

1. Noise pollution (hii sasa hivi ni agenda ya dunia).

2. Emission of gases from the tailpipe of an internal combustion engine e.g. carbon monoxide (CO), hydrocarbons (HC), carbon dioxide (CO2), oxides of nitrogen (NOx). Carbon monoxide results from burned fuel. It’s an odorless, colorless, tasteless poisonous gas. Tunajuwa mafuta mengi sasa hivi ni unleaded lakini soko huria huja na uhuru wa uharibifu.

3. Security challenges. Baadhi ya waendesha bodaboda kwa wakati mmoja au mwingine wamejihusisha na uhalifu wa aina takriban zote hadi wa mauaji.

4. Mobbing. Baadhi ya waendesha bodaboda wameshiriki kwenye matukio ya uvamizi kwa njia ya Mob na kuleta taharuki kubwa na hujuma isiyofaa hiyo biashara.

5. Road accidents.

NB.
What if leo mtu akisema bodaboda zinaleta changamoto nyingi kwenye jamii hivyo kwa kuwa tuna mbadala wao kama madaladala, UBA, Taxi Fire, Borch, Taxi, Rickshaw (Bajaj), Toyo, Kirikuu, Guta, Treni za Mwakyembe, BRT, kwamba hizi zinatosha kuondoa adha zinazotokana na biashara ya bodaboda kwamba kuanzia sasa marufuku bodaboda, unadhani mapokeo yatakuwaje? Ni vivyo hivyo kwa Wamachinga ambao ni injini ya wafanyabiashara wakubwa, wa kati na wadogo na Mama na Baba Lishe.
Siyo tu bodaboda, bali bado magereji bubu yaliyojaa mitaani, bado vituo holela vya mafuta hadi kwenye makazi ya watu bado waliowekeza kwenye hifadhi za barabara nchi nzima.
 
Back
Top Bottom