Filosofia ya Rorya
JF-Expert Member
- Sep 20, 2021
- 3,211
- 3,611
- Thread starter
- #101
Mkuu, na wakwepa kodi kubwa kubwa wana tofauti gani na Wamachinga wanaokwepa ushuru?. Kodi zinakuwaga kubwa kuliko ushuru ujuwe!Miaka 5 Maandalizi yalikuwaje
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu, na wakwepa kodi kubwa kubwa wana tofauti gani na Wamachinga wanaokwepa ushuru?. Kodi zinakuwaga kubwa kuliko ushuru ujuwe!Miaka 5 Maandalizi yalikuwaje
Mkuu, and that is why "Solution to one problem contains the seeds for the next problem"Kila mtu mwenye kosa ana story ya kuhalalisha kosa lake.
Ndio maana sheria haipindi kuonea mtu huruma.
Issue ya Tanzania ni tofauti kabisa na zile za mataifa mengine. WaTanzania bado tuna fursa nyingi ambazo hazijatumika. Tanzania tumejaliwa kuwa na ardhi kubwa sana ambayo hata bila kuweka mbolea watu wanavuna, tuna bahari, mito na maziwa ambayo watu bado wanatumia ndoana na mitumbwi ya mbao kuvua, tunafuga kienyeji. Na bahati nzuri sisi hapa kwetu ardhi, maji na kila maliasili ni Mali ya serikali. Hivyo hatuna sababu bado ya kuacha nguvu kazi yetu hii ichuuze mitumba na dawa za mbu kutoka nchi nyingine bila kulipa Kodi badala ya kuwapa moyo, maarifa na mikopo ya matrekta, pembejeo, mbegu bora, meli za uvuvi wa kisasa na uchakataji wa samaki , ufugaji wa kisasa na kuwatafitia masoko ya ndani na nje ya Nchi.Mkuu unawaongelea machinga kama kundi fulani maalumu lenye kuhitaji huruma hata kama uendeshaji wa shughuli zao unakiuka sheria za mipango miji. Kosa lililofanywa wakati wa mwendazake haliwezi kuhalalisha uholela wa shughuli zao.
Kuuza mashati 3 ya mitumba kutwa nzima halafu unahitaji huduma za ulinzi, afya, maji, shule, nk kutoka serikalini kunaisaidiaje nchi?ni upuuzi kuamini machinga wanarudisha nchi nyuma kwa namna yoyote ile.
Don't be obsessed with conspiracy theories. They are there since the existence of human beings to disort realityNimeipenda hii:-
"Na hii pengine ndiyo sababu kubwa inayowafanya mabwana wa dunia kutaka kupunguza idadi ya watu duniani kupitia vita, vyakula ya GMO, madawa, chanjo (sijasema ya UVIKO 19), mahusiano ya jinsia moja, uzazi wa mpango na ajenda zingine za hovyo ambazo zinapaswa kuwa "ratified" kimataifa."
Ukitaka ufanikiwe ni kuwabana viongozi wa serikali za mitaa, madiwani, DEDs na Chama. Hawa Wana hisa kwenye biashara hii, Wana conflict of interest. Hawa ndiyo wanaowatishia viongozi wa nchi kuwa CCM itakosa kura kama tukiwaondoa hawa kwenye maeneo ya wazi, njia za waenda kwa miguu na hata chini ya nyaya za umeme wa msongo mkubwa. Na viongozi wanashindwa kugundua mtego huu wa madiwani.Mimi nitakuwa Thomaso katika hili!! Me ni kweli wamachinga wametoka kabisa Dar na pembezoni mwa barabara ? Aliyepita kariakoo leo atujuze. Kama ndivyo basi mkuu wa mkoa wa Dar anastahili tuzo ya heshima ya juu kabisa! Huu mfupa ulishashindikana miaka nenda rudi!! Matatizo mengine yaliyoshindikana ni; 1. Tatizo la machangudoa, 2. Tatizo la ombaomba !
Kwenye jijj la Dar ukiweza kuwatoa machangudoa, omba omba na wamachinga wasiofuata utaratibu hapo utakuwa umefaulu sana!! Makamba alishindwa, Makonda alishindwa, Je huyu wa sasa ataweza?
Sema astakafiru.Jambo lililomshinda Rais Magufuli HAKUNA. Narudia HAKUNA kiongozi yeyote wa wakati huu anayeweza kuliweza.
Kaka umachinga uko hata kwenye elimu na afya. Kuna shule na vyuo vya machinga. Shule na vyuo viko kwenye mazingira yasiyofaa kuwa shule na chuo, hawana walimu Wala vifaa vya kufundishia, havina maabara, library Wala mitaala ya maana. Vina madarasa kama mabanda ya kuku.Siyo tu bodaboda, bali bado magereji bubu yaliyojaa mitaani, bado vituo holela vya mafuta hadi kwenye makazi ya watu bado waliowekeza kwenye hifadhi za barabara nchi nzima.
Best decisionUamuzi wa kuondoa wafanyabiashara wadogowadogo almaarufu Machinga 18 Oktoba, kwa maoni yangu una gharama kubwa kuliko faida/manufaa na kwamba unastahili kupitiwa/kudurusiwa upya.
Gharama ziko kiuchumi, kijamii, kiusalama na kisiasa. Sipingani na uamuzi huo, ni mzuri tu, isipokuwa nadhani maandalizi zaidi yanahitajika ili zoezi liwe na tija kwa pande zote husika.
Mkuu umetisha! Kwa kuongezea, hata baadhi ya wanasiasa ni Machinga.Kaka umachinga uko hata kwenye elimu na afya. Kuna shule na vyuo vya machinga. Shule na vyuo viko kwenye mazingira yasiyofaa kuwa shule na chuo, hawana walimu Wala vifaa vya kufundishia, havina maabara, library Wala mitaala ya maana. Vina madarasa kama mabanda ya kuku.
Kama kazi ya kuondoa machinga sio kwa wanaotandika bidhaa barabarani TU bali ziko biashara nyingine haziko sawa pia.
Kwenye kuleta maendeleo kuna wanaoumia kwa faida ya baadae, hawa waliifuata serikali ili iwaumize baadae, kuna ambao serikali inawafuata mfano barabara sita kimara waliumia wangapi kama hawazidi hawa wamachinga? Upanuzi wa ubungo mbona waliondoka bila malalamiko? Hapakuwa na kategoey hii?Wakuu sikuwahi fikiria kama ntakuja kuguswa moja kwa moja na suala la machinga,...iko hivi juzi juzi wakati narudi zangu ghetto nikakutana na mpangaji mwenzangu mdada wa makamo na katoto kake kama ka miezi minne hivi akiwa kajiinamia ,ikimbukwe kwamba sikuwahi kujua anafanya shughuli gani na hata wao hawakuwahi kujua ni kawaida kwangu kutokufatilia ya wengine labda ikibidi sana.,basi yule sister kumbe alikua ananisubiri aniage anahama kumuuliza kulikoni ! Kumbe yule dada alikua mama ntilie(lishe) wale wa pembezoni mwa bara bara hivyo alivunjiwa banda lake na ni single mama so akawa hana pa kwenda na alikua analia sana na kulaaani ,niwe mkweli mji umependeza lakini umegusa maisha ya watu kulivyo tunavyofikiri kuna tatizo mbeleni naliona.....,
kwani tafsiri ya kazi nini na je ni lazima serikali iajiri vijana wote wanaohitimu vyuo mbalimbali.ni kweli serikali ndo mwajiri pekee katika nchi hii?Mimi nina swali... Hivi Tanzania inazalisha wasomi wangapi kwa mwaka? 2 serikali idadi yao ya ajira kwa mwaka ukoje.. Na wale wasio ajiriwa wanafanya kazi gani?
Hii ndiyo shida ya kuacha kufuata ya sheria na taratibu halali. Unapoacha kufuata sheria na taratibu matokeo yake inazoeleka na inaonekana ni haki na ikishakuwa hivyo inakuwa ngumu sheria kutekelezwa. Leo machinga wanajenga vibanda popote bila utaratibu na mwishowe watajenga vibanda mpaka kwenye plot za watu. Acha waondolewe wapelekwe sehemu maalum. Bidhaa zao zinahitajika wanunuzi tutaenda na with time patazoelekaUamuzi wa kuondoa wafanyabiashara wadogowadogo almaarufu Machinga 18 Oktoba, kwa maoni yangu una gharama kubwa kuliko faida/manufaa na kwamba unastahili kupitiwa/kudurusiwa upya.
Gharama ziko kiuchumi, kijamii, kiusalama na kisiasa. Sipingani na uamuzi huo, ni mzuri tu, isipokuwa nadhani maandalizi zaidi yanahitajika ili zoezi liwe na tija kwa pande zote husika.
Iko kazi kubwa kuliko watu wanavyodhani, CCM ni janga la Taifa, haya yote yanafanyika chini ya usimamizi wa CCM. Wanamtengenezea tatizo mtanzania Kisha wanamtafutia suluhisho wao wenyewe na kudai wapigiwe makofi ya pongeziMkuu umetisha! Kwa kuongezea, hata baadhi ya wanasiasa ni Machinga.
Eti machinga kaweka biashara makusudi kwenye barabara unapomwabia ondoka umekosea kuweka biashara hapo anakuuliza Sasa nikaweke wapi, niende wapi na nionyeshe kwanza mahali pa kuweka biashara yangu. Hii inapatikana Tanzania TU serikalini ya CCM. Mwizi anakuuliza nikale wapi unapotaka kumkamata!!!Hii ndiyo shida ya kuacha kufuata ya sheria na taratibu halali. Unapoacha kufuata sheria na taratibu matokeo yake inazoeleka na inaonekana ni haki na ikishakuwa hivyo inakuwa ngumu sheria kutekelezwa. Leo machinga wanajenga vibanda popote bila utaratibu na mwishowe watajenga vibanda mpaka kwenye plot za watu. Acha waondolewe wapelekwe sehemu maalum. Bidhaa zao zinahitajika wanunuzi tutaenda na with time patazoeleka
Ule ulikuwa ni uamuzi wa Mahakama Kuu ambapo serikali ilishinda wavamizi wa hifadhi ya barabara ya Tanzaniaone ambao walikuwa wanaongozwa na Wakili Prof. Mgongofimbo wa UD.Kwenye kuleta maendeleo kuna wanaoumia kwa faida ya baadae, hawa waliifuata serikali ili iwaumize baadae, kuna ambao serikali inawafuata mfano barabara sita kimara waliumia wangapi kama hawazidi hawa wamachinga? Upanuzi wa ubungo mbona waliondoka bila malalamiko? Hapakuwa na kategoey hii?
Umachinga ni athari za Class Struggle kwenye jamii inayodhaniwa iko huru kiuchumijamii. Nasema hivi kwasababu madaraja haya katika huduma za jamii kama elimu yanazalisha Wamachinga mfano, ni wanafunzi wangapi wa shule binafsi hasa za english medium wanakuwa Wamachinga baada ya kuhitimu dhidi ya wanafunzi wa shule za umma almaarufu kama St' Kayumba? Wale wanaobahatika kupata elimu ya juu je, ni wangapi waliotoka shule binafsi wanakuwa Wamachinga baada ya kuhitimu vyuo dhidi ya wale waliotokea shule za umma (St' Kayumba?) Tuna mengi ya kurekebisha zaidi ya kuwafukuza, kubana warasimu wanaofaidika nao nk.Mkuu umetisha! Kwa kuongezea, hata baadhi ya wanasiasa ni Machinga.
Ulivyo mjinga unawaza kura za 2025 badala ya suluhisho la kudumuRais Samia hashauriwi vyema,
anatengeneza kundi kubwa sana la wapinzani nchini,
watu hao wakiachwa bila njia za kujipatia kipato wataichukia serikali yake.
Ni kweli tunahitaji miji misafi ila raia nao wanatakiwa kuwa huru kufanya shughuli zao.
CCM itapata wakati mgumu sana kujinadi 2025 kama hali hii ikiendelea.