Uamuzi wa kuwaondoa Machinga mitaa ya Dar es Salaam urejewe upya

Uamuzi wa kuwaondoa Machinga mitaa ya Dar es Salaam urejewe upya

Mkuu unawaongelea machinga kama kundi fulani maalumu lenye kuhitaji huruma hata kama uendeshaji wa shughuli zao unakiuka sheria za mipango miji. Kosa lililofanywa wakati wa mwendazake haliwezi kuhalalisha uholela wa shughuli zao.
Issue ya Tanzania ni tofauti kabisa na zile za mataifa mengine. WaTanzania bado tuna fursa nyingi ambazo hazijatumika. Tanzania tumejaliwa kuwa na ardhi kubwa sana ambayo hata bila kuweka mbolea watu wanavuna, tuna bahari, mito na maziwa ambayo watu bado wanatumia ndoana na mitumbwi ya mbao kuvua, tunafuga kienyeji. Na bahati nzuri sisi hapa kwetu ardhi, maji na kila maliasili ni Mali ya serikali. Hivyo hatuna sababu bado ya kuacha nguvu kazi yetu hii ichuuze mitumba na dawa za mbu kutoka nchi nyingine bila kulipa Kodi badala ya kuwapa moyo, maarifa na mikopo ya matrekta, pembejeo, mbegu bora, meli za uvuvi wa kisasa na uchakataji wa samaki , ufugaji wa kisasa na kuwatafitia masoko ya ndani na nje ya Nchi.

Nchi za wenzetu fursa nyingi zimejaa kwasababu hakuna ardhi huru, bahari Wala mito. Ni ujinga mtupu kudhani kuwa ukiwaondoa watu barabarani watakufa njaa, hii dhana sio kweli kabisa, machinga wengi Wana kwao ambako wameacha ardhi, mashamba, mifugo, na mitumbwi. Ukiwafukuza Leo hii mijini utaona mabasi ya kwenda mikoano, wilayani na vijijini yamejaa watu wanarudi kwao walikotoka na wengine watajazana ofisi za ofisa biashara na TRA kutuatilia taratibu za kuanzisha biashara.

Shida kubwa hapa ni madiwani na viongozi wa serikali za mitaa na Chama Cha CCM. Viongozi hawa wana maslahi binafsi kwa wafanyabiashara hawa wadogo. Fanyeni uchunguzi mtaona hili.

Hata ukiwaondoa hawa utakosa kura wakati wa changuzi kwakuwa wanaokerwa na uchafu wa mazingira unaosababishwa na watu hawa ni wengi sana kuliko hao machinga wenyewe. Pili, hata wao Kuna siku watashukuru kuondolewa mitaani kwenye biashara zisizokuwa na uhakika na kwenda kufanya shughuli za uzalishaji zenye tija, uhakika na usalama kwao na watu wengine, yaani watajiona kuwa walikuwa wajinga. Mimi ni mmojawapo ya watu ambao nilikuwa naogopa kuondoka kwenye nyumba mwajiri wangu nikidhani kwenda kuishi kwangu kutakuwa ghali, usumbufu, nk. Lakini baada ya mwajili kuninyang'anya nyumba yake na kuhamia kwangu najiona kama vile nilikuwa mjinga sana kuishi kwenye nyumba kama Ile na mtaa kama ule. Nafuraahia kwangu, nafasi na kwangu kwa kudumu na uhakika.
 
ni upuuzi kuamini machinga wanarudisha nchi nyuma kwa namna yoyote ile.
Kuuza mashati 3 ya mitumba kutwa nzima halafu unahitaji huduma za ulinzi, afya, maji, shule, nk kutoka serikalini kunaisaidiaje nchi?
 
Nimeipenda hii:-

"Na hii pengine ndiyo sababu kubwa inayowafanya mabwana wa dunia kutaka kupunguza idadi ya watu duniani kupitia vita, vyakula ya GMO, madawa, chanjo (sijasema ya UVIKO 19), mahusiano ya jinsia moja, uzazi wa mpango na ajenda zingine za hovyo ambazo zinapaswa kuwa "ratified" kimataifa."
Don't be obsessed with conspiracy theories. They are there since the existence of human beings to disort reality
 
Mimi nitakuwa Thomaso katika hili!! Me ni kweli wamachinga wametoka kabisa Dar na pembezoni mwa barabara ? Aliyepita kariakoo leo atujuze. Kama ndivyo basi mkuu wa mkoa wa Dar anastahili tuzo ya heshima ya juu kabisa! Huu mfupa ulishashindikana miaka nenda rudi!! Matatizo mengine yaliyoshindikana ni; 1. Tatizo la machangudoa, 2. Tatizo la ombaomba !
Kwenye jijj la Dar ukiweza kuwatoa machangudoa, omba omba na wamachinga wasiofuata utaratibu hapo utakuwa umefaulu sana!! Makamba alishindwa, Makonda alishindwa, Je huyu wa sasa ataweza?
Ukitaka ufanikiwe ni kuwabana viongozi wa serikali za mitaa, madiwani, DEDs na Chama. Hawa Wana hisa kwenye biashara hii, Wana conflict of interest. Hawa ndiyo wanaowatishia viongozi wa nchi kuwa CCM itakosa kura kama tukiwaondoa hawa kwenye maeneo ya wazi, njia za waenda kwa miguu na hata chini ya nyaya za umeme wa msongo mkubwa. Na viongozi wanashindwa kugundua mtego huu wa madiwani.
 
Siyo tu bodaboda, bali bado magereji bubu yaliyojaa mitaani, bado vituo holela vya mafuta hadi kwenye makazi ya watu bado waliowekeza kwenye hifadhi za barabara nchi nzima.
Kaka umachinga uko hata kwenye elimu na afya. Kuna shule na vyuo vya machinga. Shule na vyuo viko kwenye mazingira yasiyofaa kuwa shule na chuo, hawana walimu Wala vifaa vya kufundishia, havina maabara, library Wala mitaala ya maana. Vina madarasa kama mabanda ya kuku.

Kama kazi ya kuondoa machinga sio kwa wanaotandika bidhaa barabarani TU bali ziko biashara nyingine haziko sawa pia.
 
Uamuzi wa kuondoa wafanyabiashara wadogowadogo almaarufu Machinga 18 Oktoba, kwa maoni yangu una gharama kubwa kuliko faida/manufaa na kwamba unastahili kupitiwa/kudurusiwa upya.

Gharama ziko kiuchumi, kijamii, kiusalama na kisiasa. Sipingani na uamuzi huo, ni mzuri tu, isipokuwa nadhani maandalizi zaidi yanahitajika ili zoezi liwe na tija kwa pande zote husika.
Best decision
 
Machinga wameonewa,wangewaondoa wa katikati ya mji pekee kama wanaogopa macho ya wageni.
Pembeni mwa mji wangewaacha
 
Machinga ni zao la ukosefu wa sera za ccm kuhusu uchumi na raslimali za nchi ni nyingi kuliko idadi ya watu shida tumekosa viongozi wabunifu
 
Kaka umachinga uko hata kwenye elimu na afya. Kuna shule na vyuo vya machinga. Shule na vyuo viko kwenye mazingira yasiyofaa kuwa shule na chuo, hawana walimu Wala vifaa vya kufundishia, havina maabara, library Wala mitaala ya maana. Vina madarasa kama mabanda ya kuku.

Kama kazi ya kuondoa machinga sio kwa wanaotandika bidhaa barabarani TU bali ziko biashara nyingine haziko sawa pia.
Mkuu umetisha! Kwa kuongezea, hata baadhi ya wanasiasa ni Machinga.
 
Wakuu sikuwahi fikiria kama ntakuja kuguswa moja kwa moja na suala la machinga,...iko hivi juzi juzi wakati narudi zangu ghetto nikakutana na mpangaji mwenzangu mdada wa makamo na katoto kake kama ka miezi minne hivi akiwa kajiinamia ,ikimbukwe kwamba sikuwahi kujua anafanya shughuli gani na hata wao hawakuwahi kujua ni kawaida kwangu kutokufatilia ya wengine labda ikibidi sana.,basi yule sister kumbe alikua ananisubiri aniage anahama kumuuliza kulikoni ! Kumbe yule dada alikua mama ntilie(lishe) wale wa pembezoni mwa bara bara hivyo alivunjiwa banda lake na ni single mama so akawa hana pa kwenda na alikua analia sana na kulaaani ,niwe mkweli mji umependeza lakini umegusa maisha ya watu kulivyo tunavyofikiri kuna tatizo mbeleni naliona.....,
Kwenye kuleta maendeleo kuna wanaoumia kwa faida ya baadae, hawa waliifuata serikali ili iwaumize baadae, kuna ambao serikali inawafuata mfano barabara sita kimara waliumia wangapi kama hawazidi hawa wamachinga? Upanuzi wa ubungo mbona waliondoka bila malalamiko? Hapakuwa na kategoey hii?
 
Mimi nina swali... Hivi Tanzania inazalisha wasomi wangapi kwa mwaka? 2 serikali idadi yao ya ajira kwa mwaka ukoje.. Na wale wasio ajiriwa wanafanya kazi gani?
kwani tafsiri ya kazi nini na je ni lazima serikali iajiri vijana wote wanaohitimu vyuo mbalimbali.ni kweli serikali ndo mwajiri pekee katika nchi hii?
 
Uamuzi wa kuondoa wafanyabiashara wadogowadogo almaarufu Machinga 18 Oktoba, kwa maoni yangu una gharama kubwa kuliko faida/manufaa na kwamba unastahili kupitiwa/kudurusiwa upya.

Gharama ziko kiuchumi, kijamii, kiusalama na kisiasa. Sipingani na uamuzi huo, ni mzuri tu, isipokuwa nadhani maandalizi zaidi yanahitajika ili zoezi liwe na tija kwa pande zote husika.
Hii ndiyo shida ya kuacha kufuata ya sheria na taratibu halali. Unapoacha kufuata sheria na taratibu matokeo yake inazoeleka na inaonekana ni haki na ikishakuwa hivyo inakuwa ngumu sheria kutekelezwa. Leo machinga wanajenga vibanda popote bila utaratibu na mwishowe watajenga vibanda mpaka kwenye plot za watu. Acha waondolewe wapelekwe sehemu maalum. Bidhaa zao zinahitajika wanunuzi tutaenda na with time patazoeleka
 
Mkuu umetisha! Kwa kuongezea, hata baadhi ya wanasiasa ni Machinga.
Iko kazi kubwa kuliko watu wanavyodhani, CCM ni janga la Taifa, haya yote yanafanyika chini ya usimamizi wa CCM. Wanamtengenezea tatizo mtanzania Kisha wanamtafutia suluhisho wao wenyewe na kudai wapigiwe makofi ya pongezi
 
Hii ndiyo shida ya kuacha kufuata ya sheria na taratibu halali. Unapoacha kufuata sheria na taratibu matokeo yake inazoeleka na inaonekana ni haki na ikishakuwa hivyo inakuwa ngumu sheria kutekelezwa. Leo machinga wanajenga vibanda popote bila utaratibu na mwishowe watajenga vibanda mpaka kwenye plot za watu. Acha waondolewe wapelekwe sehemu maalum. Bidhaa zao zinahitajika wanunuzi tutaenda na with time patazoeleka
Eti machinga kaweka biashara makusudi kwenye barabara unapomwabia ondoka umekosea kuweka biashara hapo anakuuliza Sasa nikaweke wapi, niende wapi na nionyeshe kwanza mahali pa kuweka biashara yangu. Hii inapatikana Tanzania TU serikalini ya CCM. Mwizi anakuuliza nikale wapi unapotaka kumkamata!!!
 
Kwenye kuleta maendeleo kuna wanaoumia kwa faida ya baadae, hawa waliifuata serikali ili iwaumize baadae, kuna ambao serikali inawafuata mfano barabara sita kimara waliumia wangapi kama hawazidi hawa wamachinga? Upanuzi wa ubungo mbona waliondoka bila malalamiko? Hapakuwa na kategoey hii?
Ule ulikuwa ni uamuzi wa Mahakama Kuu ambapo serikali ilishinda wavamizi wa hifadhi ya barabara ya Tanzaniaone ambao walikuwa wanaongozwa na Wakili Prof. Mgongofimbo wa UD.
 
Mkuu umetisha! Kwa kuongezea, hata baadhi ya wanasiasa ni Machinga.
Umachinga ni athari za Class Struggle kwenye jamii inayodhaniwa iko huru kiuchumijamii. Nasema hivi kwasababu madaraja haya katika huduma za jamii kama elimu yanazalisha Wamachinga mfano, ni wanafunzi wangapi wa shule binafsi hasa za english medium wanakuwa Wamachinga baada ya kuhitimu dhidi ya wanafunzi wa shule za umma almaarufu kama St' Kayumba? Wale wanaobahatika kupata elimu ya juu je, ni wangapi waliotoka shule binafsi wanakuwa Wamachinga baada ya kuhitimu vyuo dhidi ya wale waliotokea shule za umma (St' Kayumba?) Tuna mengi ya kurekebisha zaidi ya kuwafukuza, kubana warasimu wanaofaidika nao nk.
 
Rais Samia hashauriwi vyema,

anatengeneza kundi kubwa sana la wapinzani nchini,

watu hao wakiachwa bila njia za kujipatia kipato wataichukia serikali yake.

Ni kweli tunahitaji miji misafi ila raia nao wanatakiwa kuwa huru kufanya shughuli zao.

CCM itapata wakati mgumu sana kujinadi 2025 kama hali hii ikiendelea.
Ulivyo mjinga unawaza kura za 2025 badala ya suluhisho la kudumu

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom