Uamuzi wa kuwaondoa Machinga mitaa ya Dar es Salaam urejewe upya

Uamuzi wa kuwaondoa Machinga mitaa ya Dar es Salaam urejewe upya

Nilipata fursa ya kuishi marekani vijijini, wengi wetu tunaokwenda Marekani wanakwenda kuishi mijini, lakini mimi nimeishi kule vijijini kabisa kama Chelsea na kijijini zaidi ambako watu wanajikamulia wenyewe juice za apple na kuweka kwenye galoni na kuuza kiholela tu.
Wenzetu marekani mifumo yao yote ya uongozi inaongozwa na watu smart, ndio maana kila changamoto wanayokutana nayo inapatiwa solution kiuwepesi kbsa....Bongo na africa kwa ujumla nepotism imetuharibu sana.
 
Wakuu sikuwahi fikiria kama ntakuja kuguswa moja kwa moja na suala la machinga,...iko hivi juzi juzi wakati narudi zangu ghetto nikakutana na mpangaji mwenzangu mdada wa makamo na katoto kake kama ka miezi minne hivi akiwa kajiinamia ,ikimbukwe kwamba sikuwahi kujua anafanya shughuli gani na hata wao hawakuwahi kujua ni kawaida kwangu kutokufatilia ya wengine labda ikibidi sana.,basi yule sister kumbe alikua ananisubiri aniage anahama kumuuliza kulikoni ! Kumbe yule dada alikua mama ntilie(lishe) wale wa pembezoni mwa bara bara hivyo alivunjiwa banda lake na ni single mama so akawa hana pa kwenda na alikua analia sana na kulaaani ,niwe mkweli mji umependeza lakini umegusa maisha ya watu kulivyo tunavyofikiri kuna tatizo mbeleni naliona.....,
Huo si ajabu faida yote alikuwa anakula na kununua vijora ..sasa yametokea ya kutokea hana hta mia ya kumsaidia.
 
Huo si ajabu faida yote alikuwa anakula na kununua vijora ..sasa yametokea ya kutokea hana hta mia ya kumsaidia

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
Hakuna atakayekufa kwa sababu ajira ovu imefika mwisho, machinga wote wanajua kuwa ipo siku warafurumushwa kwa kuwa wanapanga vitu sehemu zenye marufuku ila walijazwa kiburi wakajisahau. Uwezi kupanga vitu kwenye barabara reserve alafu tanroad inapiga x kila siku wao wanafuta wataendelea.

Alafu uje tuseme hawajui sheria za nchi. Machinga wa kweli anatembea na duka.sijui hawa machinga waku amia eneo wanapenda vitambulisho ili iwe. Wakati jina machinga linatokana na watu binafsi wanaotembeza city. Tunajiumiza wenyewe kwa kukumbatia ujinga
 
Kwenye kuleta maendeleo kuna wanaoumia kwa faida ya baadae, hawa waliifuata serikali ili iwaumize baadae, kuna ambao serikali inawafuata mfano barabara sita kimara waliumia wangapi kama hawazidi hawa wamachinga? Upanuzi wa ubungo mbona waliondoka bila malalamiko? Hapakuwa na kategoey hii?
Kuna na vyeti feki waliondoshwa bila mafao
Kuna waliotumbuliwa watu wakasherehekea
Kuna waliohamishiwa Dodoma bila kupenda

Wote hawa wapo
Ila sheria ilikua inafuatwa....
Machinga..........
 
Huo si ajabu faida yote alikuwa anakula na kununua vijora ..sasa yametokea ya kutokea hana hta mia ya kumsaidia

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
Hiyo ni tabia ya waafrika wengi wakiwemo waajiliw
Hakuna atakayekufa kwa sababu ajira ovu imefika mwisho, machinga wote wanajua kuwa ipo siku warafurumushwa kwa kuwa wanapanga vitu sehemu zenye marufuku ila walijazwa kiburi wakajisahau. Uwezi kupanga vitu kwenye barabara reserve alafu tanroad inapiga x kila siku wao wanafuta wataendelea. Alafu uje tuseme hawajui sheria za nchi. Machinga wa kweli anatembea na duka.sijui hawa machinga waku amia eneo wanapenda vitambulisho ili iwe. Wakati jina machinga linatokana na watu binafsi wanaotembeza city. Tunajiumiza wenyewe kwa kukumbatia ujinga
Machinga ni mradi madhubuti wa baadhi ya madiwani, maDED na viongozi wa Chama. Waulize machinga watakwambia nani amewaweka pale kwa vigezo na Mashariti gani.
 
Ulivyo mjinga unawaza kura za 2025 badala ya suluhisho la kudumu

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
Watu wasiogope kuchukua hatua. Hakuna uwamuzi mgumu kama ule uwamuzi wa kuondoa usafiri wa Hiace (vipanya) barabarani, au kuwaondoa watumishi hewa na wasiokuwa na vyeti, au kuwavunjia wananchi wa ubungo/kimara kupisha upanuzi wa barabara au kuwaondoa watu woote wa Kipawa kupisha upanuzi wa airport. Mbona waliondoka na kura zilipogwa za ndiyo? Kaka watu wasiogope eti uchaguzi 2025, sio kweli kabisa maana tunaopenda miji iwe safi tuko wengi zaidi kuliko machinga.
 
Iko siku machinga watazuia barabara isipite magari kabisa ili wao wafanye biashara juu ya barabara. Na hii haiko mbali sana kama wamachinga hawataondolewa Leo kwenye maeneo yasiyofaa kumfanyia biashara. Mtoto umleavyo ndiyo akuavyo.
 
Hakuna madhala yoyote labda kisiasa machinga hawachangii lolote ktk uchumi wa nchi.

Wanasiasa wanawaofia wamachinga km mtaji wa kisiasa lkn ukweli ni kwamba kuendelea kuwabembeleza ni kupoteza nguvu kazi Watanzania umachinga wetu ni kilimo huko ndio kwenye ajira za uwahika km serikali inaamua kuweka mazingira mazuri ya kilimo na masoko hakuna kazi inayoitwa umachinga duniani

Unakuta mtu anatoa mzigo mpaka wa million 10 kwa wamachinga na hakati risiti

Tutafika kweli?
 
Uamuzi wa kuondoa wafanyabiashara wadogowadogo almaarufu Machinga 18 Oktoba, kwa maoni yangu una gharama kubwa kuliko faida/manufaa na kwamba unastahili kupitiwa/kudurusiwa upya.

Gharama ziko kiuchumi, kijamii, kiusalama na kisiasa. Sipingani na uamuzi huo, ni mzuri tu, isipokuwa nadhani maandalizi zaidi yanahitajika ili zoezi liwe na tija kwa pande zote husika.
Acha UPOTOSHAJI wamachinga hawaondolewi ila wana pangwa ktk kupangwa huko kuna faida
Kwanza utamfanya yule mfanyabiashara aweze kurasimishiwa biashara yake na ukisha rasimisha kuna faida zake likiwemo mikopo n.k
Chukulia ilivyokuwa awali Vitambulisho vya machinga vilikuwa havina picha wala signature ina maana hapo huja mrasimisha 100% kheri wapangwe then watanufaika zaidi
 
Kaka kama mji mzima wa Kipawa umehamishwa kupisha upanuzi wa airport wamachinga ni nani wasihamishwe kwenye maeneo waliyoyavamia? Hata serikali kuwapa maeneo ni hisani TU na mapenzi yake kwa wananchi, lakini hawa jamaa walitakiwa kupewa adhabu kwa kuchafua masingira na kuhatarisha maisha Yao na ya wengine kwa kuziba miundombinu ya watembea kwa miguu na maji taka. Kitu Cha ajabu mhalifu ndiye anataka kupewa haki asiyoistahili. Yaani serikalini itumie hela zetu kuwaondoa, kuondoa uchafu wao, kufagia na kutengeneza walipoharibu. Hii ni serikali ya wapi ya aina hii?

Huu ni mpango wa wanasiasa tu, ni mmachinga gani anakwenda kufungasha bidhaa China? Ni mmachinga gani ana mabegi 1000 Kando ya barabara TU. Hata lile jengo la machinga lazima liwe na ukomo wa kukaa pale, isiwe milele, kama mtaji wako ukiwa mkubwa uondoke uposhe wengine wadogo pia wakue.
 
"Solution to one problem contains the seeds for the next problem"
Mkuu, muda haupigwi masumbwi, ukiwadia utatuonyesha tatizo lingine lililozalishwa na ufumbuzi wa tatizo la msingi lililopita.
 
Acha UPOTOSHAJI wamachinga hawaondolewi ila wana pangwa ktk kupangwa huko kuna faida
Kwanza utamfanya yule mfanyabiashara aweze kurasimishiwa biashara yake na ukisha rasimisha kuna faida zake likiwemo mikopo n.k
Chukulia ilivyokuwa awali Vitambulisho vya machinga vilikuwa havina picha wala signature ina maana hapo huja mrasimisha 100% kheri wapangwe then watanufaika zaidi
Mkuu, siyo UPOTOSHAJI, Wamachinga wanaondolewa, unaposema kwamba wanapangwa ni UPOTOSHAJI, kwasababu hawapangwi mijinikati bali wanaondolewa mijinikati na kwenye hifadhi za barabara, nime-paraphrase andiko lako kwenye sentensi ya kwanza.

Sorry, nadhani umekuja late kwenye dialogue ya mada hii ambayo imejadiliwa na WanaJF 1092 na kuzalisha kurasa 7 hadi sasa, maoni mengi, michango mingi imetolewa ambayo nadhani hukuweza na huenda haiwezekani ukaipitia yote. Hata hivyo natamani ungerejea mada ili uone kwamba kimsingi sikupinga uamuzi wa Wamachinga kuondolewa na zaidi nilisema sipingani na uamuzi huu bali madai yangu yalikuwa ni yafanyike maandalizi ya kutosha tena nikasema ya kisera, kisheria, kanuni, miongozo nk ili taifa liwe na ufumbuzi wa kudumu wa tatizo hili, nikasisitiza kuwa kuna mengi yaliyofichama kwenye umachinga ambayo huenda warasimu hawayajui na wala hawajatafuta kuyajuwa zikiwemo: walianza lini? takwimu zao?

Nani yuko nyuma yao (maana kila mwaka wa uchaguzi wanaondolewa na wanarudi)? chanzo chao ni mfumo wa elimu? au ni sera ya taifa ya vijana? au mfumo usiorafiki wa kodi? au ni nini chanzo chao? nikasema tutafute kuyajuwa hayo yote, aidha, kwenye kuchangia uzi nikasema kwamba ili kuondoa kichuguu usiuwe mchwa ua malkia wa mchwa inapobidi, wengi walielewa sijui kwasababu walianza kusoma mada A-Z au? Kwenye uzi pia nilibainisha kwamba wamachinga ni tatizo la dunia (nikatoa mifano ya China, South Africa, Ethiopia, Kenya, South Korea nk, mmoja akasema kwamba hata US wako hadi vijijini aliwahi kuishi huko akawakuta wapo), nikasema hawa watu wanafaida, nikapendekeza zaidi kwamba huko kwingineko wanatumika kwa faida ya taifa (wamewekewa mfumo wa kuchangia pato la taifa kwasababu wako wengi na hivyo taifa linawahudumia kwa mzigo wa kibajeti kwenye huduma za jamii kwamba lazima na wao wachangie pato la taifa) nikaja na pendekezo la kuwa-export (nikatoa na takwimu za Nannies wa South Korea walioko Middle East wanaochangia 30% ya GDP na Kenya kabla ya Corona diaspora wao including Machinga walichangia 16% ya GDP, nikauliza sisi Tz hali ikoje?

Tunazo takwimu hizi kama za South Korea na Kenya?), sasa je, sisi tunaposhughulika nao tumezingatia hayo yote? Au tunatimiza bila kujuwa maandiko kwamba "Solution to one problem contains the seeds for the next problem" mdau mmoja akaguswa na mada na kutamani ije vita ya tatu ya dunia (anatamani kuviona kwa macho yake) ili kurekebisha mfumo mbovu wa sasa wa dunia akimaanisha nilivyomuelewa kwamba dunia kujivua gamba la mfumo usio sawia kwa wote. Mkuu, next time tunapochangia mada ni vizuri tukaelewa mada, na maudhui yake na maeneo yanayoposimamia mada na maeneo yanayopingwa na mada ili tutendeane justice kwa faida ya wote wanaosoma maandiko ya Jamvi hili ukiwemo kuhakikisha ubora wa JF.

A stitch in time saves nine Cal Tinney, (1937)
The moral of the idiom is that "if you sort out a problem immediately it may save a lot of extra work later"

Kwa kuzingatia methali hiyo hapo juu Chinga wamekuwepo nasi kwa miaka 36 sasa je, leo tunaweza kusema ni tatizo la dharura? Au ni tatizo sugu (lililokomazwa?) je, tatizo sugu linaweza kumalizwa kwa matamko? miaka yote ya uchaguzi mkuu kuanzia 1990 - 2010 waliondolewa lakini walirudi. Leo hii wanaendelea kuwepo pale CBD kwenye jiji la kibiashara hata baada ya ultimatum kwisha. Jiji la kibiashara na utalii la Arusha waliwekewa mpango mzuri madhubuti kabisa wa kumaliza tatizo ambapo walipelekwa pembezoni na bado wateja wao wameendelea kuwafuata huko kwanini? Kwasababu maandalizi bora yalifanyika, tukajifunze Arusha.
 
"Solution to one problem contains the seeds for the next problem"
Mkuu, muda haupigwi masumbwi, ukiwadia utatuonyesha tatizo lingine lililozalishwa na ufumbuzi wa tatizo la msingi lililopita.
Kaka hakuna ubishi hata chembe kuwa tatizo hili ni zao la wanasiasa uchwara ambao wanatafuta nafuu ya muda mfupi TU. Wananchi hawa walianza kidogokidogo kwa kuvamia maeneo ya wazi ambayo yametengwa kwa kazi nyingine. Kila walipopavamia walitundika bendera ya Chama na wakati mwingine kufungua matawi ya wakereketwa. Baada ya maeneo ya wazi kwisha wakaanza kuvamia njia za waenda kwa miguu, service roads, na vituo vya mabasi.

Na huko kulipojaa wakahamia kandokqndo mwa barabara za magari. Kunakoelekea machinga wanakwenda kufunga barabara ili magari yasipite kabisaaa, na gari likipita wanalitoboa typre au kumpiga dereva au kuvunja vioo vya gari. Machinga Sasa wamevamia ofisi za kazi kuwauzia watu nyanya, vitunguu, viungo vya pilau, chupi nk. Hospitali na vyuo vimezingirwa na machinga.

Hali hii inakwenda kuwa bomu kwa serikali kama haitarekebishwa leoleo.
 
Mkuu, siyo UPOTOSHAJI, Wamachinga wanaondolewa, unaposema kwamba wanapangwa ni UPOTOSHAJI, kwasababu hawapangwi mijinikati bali wanaondolewa mijinikati na kwenye hifadhi za barabara, nime-paraphrase andiko lako kwenye sentensi ya kwanza.

Sorry, nadhani umekuja late kwenye dialogue ya mada hii ambayo imejadiliwa na WanaJF 1092 na kuzalisha kurasa 7 hadi sasa, maoni mengi,
Tatizo la Tanzania sio kwa wamachinga TU, hata wakulima, wafugaji, wavuvi, wachoma mkaa, nk wote wameachiwa walime, wafuge, wavue na kuchoma mkaa kiholela. Kuja kutahamaki wakulima na wafugaji wanauana kugombea maeneo ya malisho na sehemu ya kulima, wakata mkaa wanakata miti hata kwenye vyanzo vya maji, wavuvi wanavua hata Mayai na makinda ya samaki, wachimbaji madini wanachimba kiholela.

Kama wakulima na wafugaji hawapewi na serikali maeneo ya kufugia na kulima ni makosa kuwatreat machinga tofauti na wananchi wanaokosa pia maeneo ya kuchungia, kulima, kuvua na kuchimba madini. Wavuvi wenye nyavu za matundu madogo wananyanganywa na kuzichoma bila kupewa nyavu sahihi lakini machinga wanadai wapewe maeneo sahihi.

Serikali lazima Ije na mpango utakaotatua shida na kero za makundi yote.

Serikali
 
Kuna na vyeti feki waliondoshwa bila mafao
Kuna waliotumbuliwa watu wakasherehekea
Kuna waliohamishiwa Dodoma bila kupenda

Wote hawa wapo
Ila sheria ilikua inafuatwa....
Machinga..........
Na je hayo maeneo wanayopewa/hamishiwa yana ukomo wa mtu kufanyia biashara hapo, au mtu anakwenda kuwa mmachinga milele kwenye eneo hilo?

Kuna mtu ni "mmachinga" pale manzese anauza mitumba Kando ya barabara hadi Leo ingawa anamiliki madaladala hapa mjini kwa biashara hii, lakini bado anajiita mmachinga na hataki kuondoka eneo hilo.

.Je, umachinga hauna ukomo? Lazima serikali Ije na sera, kanuni na taratibu za biashara hii. Jengo la machinga mtu hapaswi kukaa kwa zaidi ya muda fulani ili kupisha wamachinga wengine wakuze mitaji Yao, vinginevyo hakuna maana yoyote kwenye jina hili la machinga. Lazima serikali na tafsiri ya nani ni mmachinga.
 
Kaka hakuna ubishi hata chembe kuwa tatizo hili ni zao la wanasiasa uchwara ambao wanatafuta nafuu ya muda mfupi TU. Wananchi hawa walianza kidogokidogo kwa kuvamia maeneo ya wazi ambayo yametengwa kwa kazi nyingine. Kila walipopavamia walitundika bendera ya Chama na wakati mwingine kufungua matawi ya wakereketwa. Baada ya maeneo ya wazi kwisha wakaanza kuvamia njia za waenda kwa miguu, service roads, na vituo vya mabasi. Na huko kulipojaa wakahamia kandokqndo mwa barabara za magari. Kunakoelekea machinga wanakwenda kufunga barabara ili magari yasipite kabisaaa, na gari likipita wanalitoboa typre au kumpiga dereva au kuvunja vioo vya gari. Machinga Sasa wamevamia ofisi za kazi kuwauzia watu nyanya, vitunguu, viungo vya pilau, chupi nk. Hospitali na vyuo vimezingirwa na machinga.

Hali hii inakwenda kuwa bomu kwa serikali kama haitarekebishwa leoleo.
Mkuu,
Umekita kwenye point! Somehow somewhere kuna uzembe wa makusudi wa warasimu ulifanyika. Literally uvamizi wao wa maeneo ni kama ni majibu ya uvamizi wa maeneo ya wazi "open spaces" uliokuwa ukifanywa na matajiri enzi zileeeee hadi viwanja vya Mnazi Mmoja, Biafra, Kawe, Jangwani, Rangi Tatu, mashule ama kuvamiwa au kumegwa.
 
Tatizo la Tanzania sio kwa wamachinga TU, hata wakulima, wafugaji, wavuvi, wachoma mkaa, nk wote wameachiwa walime, wafuge, wavue na kuchoma mkaa kiholela. Kuja kutahamaki wakulima na wafugaji wanauana kugombea maeneo ya malisho na sehemu ya kulima, wakata mkaa wanakata miti hata kwenye vyanzo vya maji, wavuvi wanavua hata Mayai na makinda ya samaki, wachimbaji madini wanachimba kiholela.

Serikali
Umeona mkuu,
Ndiyo maana nilisema pia tuna Wamachinga wa kati na wakubwa ukiacha hawa wadogo, wa kati ni kama wale wanaoendesha magereji kama uyoga kila eneo na wakubwa ni kama wale waliojenga vituo vya mafuta hadi kwenye madirisha ya vyumba vya kulala watu kwenye makazi yao na pia wale waliovamia na kujenga kwenye hifadbhi za barabara za Tanroads na Tarura nchi nzima. Kumbe basi tafsiri ya Machinga ni mtu anayefanya shughuli za kibiashara kiholela bila kufuata taratibu zikiwemo za mipango miji.
 
Na je hayo maeneo wanayopewa/hamishiwa yana ukomo wa mtu kufanyia biashara hapo, au mtu anakwenda kuwa mmachinga milele kwenye eneo hilo?

Kuna mtu ni "mmachinga" pale manzese anauza mitumba Kando ya barabara hadi Leo ingawa anamiliki madaladala hapa mjini kwa biashara hii, lakini bado anajiita mmachinga na hataki kuondoka eneo hilo.
.Je, umachinga hauna ukomo? Lazima serikali Ije na sera, kanuni na taratibu za biashara hii. Jengo la machinga mtu hapaswi kukaa kwa zaidi ya muda fulani ili kupisha wamachinga wengine wakuze mitaji Yao, vinginevyo hakuna maana yoyote kwenye jina hili la machinga. Lazima serikali na tafsiri ya nani ni mmachinga.
Na ndio maana wanaondolewa
Serikali ishawashtukia

Wapangishe fremu watambulike km wafanyabiashara wengine na kodi walipe

Ukipata kizimba nafikiri haina haja ya kupisha wengine
Wengine waende maeneo mengine
 
Back
Top Bottom