Acha UPOTOSHAJI wamachinga hawaondolewi ila wana pangwa ktk kupangwa huko kuna faida
Kwanza utamfanya yule mfanyabiashara aweze kurasimishiwa biashara yake na ukisha rasimisha kuna faida zake likiwemo mikopo n.k
Chukulia ilivyokuwa awali Vitambulisho vya machinga vilikuwa havina picha wala signature ina maana hapo huja mrasimisha 100% kheri wapangwe then watanufaika zaidi
Mkuu, siyo UPOTOSHAJI, Wamachinga wanaondolewa, unaposema kwamba wanapangwa ni UPOTOSHAJI, kwasababu hawapangwi mijinikati bali wanaondolewa mijinikati na kwenye hifadhi za barabara, nime-paraphrase andiko lako kwenye sentensi ya kwanza.
Sorry, nadhani umekuja late kwenye dialogue ya mada hii ambayo
imejadiliwa na WanaJF 1092 na kuzalisha kurasa 7 hadi sasa, maoni mengi, michango mingi imetolewa ambayo nadhani hukuweza na huenda haiwezekani ukaipitia yote. Hata hivyo natamani ungerejea mada ili uone kwamba kimsingi sikupinga uamuzi wa Wamachinga kuondolewa na zaidi nilisema
sipingani na uamuzi huu bali madai yangu yalikuwa ni yafanyike maandalizi ya kutosha tena nikasema ya
kisera, kisheria, kanuni, miongozo nk ili taifa liwe na ufumbuzi wa kudumu wa tatizo hili, nikasisitiza kuwa kuna mengi yaliyofichama kwenye umachinga ambayo huenda warasimu hawayajui na wala hawajatafuta kuyajuwa zikiwemo: walianza lini? takwimu zao?
Nani yuko nyuma yao (maana kila mwaka wa uchaguzi wanaondolewa na wanarudi)? chanzo chao ni mfumo wa elimu? au ni sera ya taifa ya vijana? au mfumo usiorafiki wa kodi? au ni nini chanzo chao? nikasema tutafute kuyajuwa hayo yote, aidha, kwenye kuchangia uzi nikasema kwamba ili
kuondoa kichuguu usiuwe mchwa ua malkia wa mchwa inapobidi
, wengi walielewa sijui kwasababu walianza kusoma mada A-Z au? Kwenye uzi pia nilibainisha kwamba wamachinga ni tatizo la dunia (nikatoa mifano ya China, South Africa, Ethiopia, Kenya, South Korea nk, mmoja akasema kwamba hata US wako hadi vijijini aliwahi kuishi huko akawakuta wapo), nikasema hawa watu wanafaida, nikapendekeza zaidi kwamba huko kwingineko wanatumika kwa faida ya taifa (wamewekewa mfumo wa kuchangia pato la taifa kwasababu wako wengi na hivyo taifa linawahudumia kwa mzigo wa kibajeti kwenye huduma za jamii kwamba lazima na wao wachangie pato la taifa) nikaja na pendekezo la kuwa-export (nikatoa na takwimu za Nannies wa South Korea walioko Middle East wanaochangia 30% ya GDP na Kenya kabla ya Corona diaspora wao including Machinga walichangia 16% ya GDP, nikauliza sisi Tz hali ikoje?
Tunazo takwimu hizi kama za South Korea na Kenya?), sasa je, sisi tunaposhughulika nao tumezingatia hayo yote? Au tunatimiza bila kujuwa maandiko kwamba
"Solution to one problem contains the seeds for the next problem" mdau mmoja akaguswa na mada na kutamani ije vita ya tatu ya dunia (anatamani kuviona kwa macho yake) ili kurekebisha mfumo mbovu wa sasa wa dunia akimaanisha nilivyomuelewa kwamba dunia kujivua gamba la mfumo usio sawia kwa wote. Mkuu, next time tunapochangia mada ni vizuri tukaelewa mada, na maudhui yake na maeneo yanayoposimamia mada na maeneo yanayopingwa na mada ili tutendeane justice kwa faida ya wote wanaosoma maandiko ya Jamvi hili ukiwemo kuhakikisha ubora wa JF.
A stitch in time saves nine
Cal Tinney, (1937)
The moral of the idiom is that "if you sort out a problem immediately it may save a lot of extra work later"
Kwa kuzingatia methali hiyo hapo juu Chinga wamekuwepo nasi kwa miaka 36 sasa je, leo tunaweza kusema ni tatizo la dharura? Au ni tatizo sugu (lililokomazwa?) je, tatizo sugu linaweza kumalizwa kwa matamko? miaka yote ya uchaguzi mkuu kuanzia 1990 - 2010 waliondolewa lakini walirudi. Leo hii wanaendelea kuwepo pale CBD kwenye jiji la kibiashara hata baada ya ultimatum kwisha. Jiji la kibiashara na utalii la Arusha waliwekewa mpango mzuri madhubuti kabisa wa kumaliza tatizo ambapo walipelekwa pembezoni na bado wateja wao wameendelea kuwafuata huko kwanini? Kwasababu maandalizi bora yalifanyika, tukajifunze Arusha.