Uamuzi wa Rais Magufuli Arusha ni wa kupongezwa

Uamuzi wa Rais Magufuli Arusha ni wa kupongezwa

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
9,780
Reaction score
15,488
Rais Magufuli tumpongeze pale anapofanya maamuzi ambayo yana manufaa kwa taifa kwa ujumla na hapa ameweka taifa kwanza. Kama nilivyosema kwa mimi navyomjua Rais Magufuli alikuwa anapenda vijana viongozi wa upinzani Arusha kwa maendeleo walioleta hata Lema Rais Magufuli anampenda kama mtu mwenye msimamo.

Wapinzani hasa wa Arusha Magufuli hajawahi kusema lolote baya hata siku moja. Lakini bahati mbaya vijana waliopelekwa pale hasa Mkuu wa Mkoa alikuwa ameweka siasa mbele kiasi kwamba alimnafiki mpaka Mkuu wa Mkoa wa zamani kuondolewa wakati akiwa Mkuu wa Wilaya; kumbe Rais Magufuli amegundua huyu Gambo ndiyo tatizo kuanzia mwazo.

1. Kwanza Gambo alikuwa aliwaambia viongozi wa KKT na wa Waislamu pale atawapa viwanja wakati huohuo msimamo wa serikali ni kutokutoa sehemu za wazi.

2. Alitaka stendi ijengwe kwenye kiwanja cha serikali wakati kuna utafiti na plan ya mji ambayo imeshaonyesha sehemu ya kujenga stendi.

3. Alikuwa hawahusishi halmashauri kwenye malalamiko ya yuko tayari kuongea na media kabla hata ya kuongea na watu wanaolipa kampuni za ujenzi sehemu mbalimbali.

4. Lema alileta mwekezaji waziwazi alimkataa kwasababu tu Lema angeweza kusifiwa. Waligombana mpaka kwenye Camera

Mpaka sasa Arusha hakuna stendi mpya sio kwasababu ya pesa kukosekana au sehemu ya kujenga kukosekana. Ni kwasababu Gambo na viongozi wa CCM walitaka serikali iwalipe CCM na wajenge stendi sehemu yao na jata ikiwezekana stendi iwe ya CCM kama ilivyo uwanja wa mpira wa pale Arusha. Hii sio raisi kwa Rais Magufuli kukubali ukweli kwamba stendi ya Arusha haijajengwa kwasababu za kisiasa tu na maslahi binafsi.

Lakini kingine cha kusifia ni Rais Magufuli kuwaambia wazi wateule kwamba wasitumie nafasi zao kutafuta sifa bila kujali kufuata utaratibu na maagizo ya serikali. Yaani kwa ufupi ni kwamba viongozi wateule wanatakiwa kufuata sheria na sio kila mmoja kufanya anavyotaka.
 
Back
Top Bottom