Mzee wa Code
Member
- Sep 23, 2024
- 61
- 91
Dodoma ni Makao Makuu ya Nchi kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na hivyo kumekuwa na changamoto ya kutokuwepo kwa Viongozi waandamizi wa Serikali katika ofisi zao.
Mwaka 2017, aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati John Magufuli, alitangaza rasmi kuhamia kwa Serikali Dodoma, hatua iliyopokelewa vyema na kuanza kutekelezwa, lakini miaka ya hiviri karibuni, uchunguzi umebaini shughuli nyingi za Serikali zimehamishiwa Dar es Salaam na Zanzibar, huku nyingine zikifanyika kwa njia za Mtandao.
Mifano, Machi 31, 2023, Mawaziri wapya waliapishwa kupitia Ikulu ndogo ya Tunguu, Zanzibar badala ya Dodoma, pia Julai 6, 2023, hafla nyingine kama hiyo ilifanyika Ikulu ya Dar es Salaam.
Mtumishi mmoja wa Serikali, ambaye hakutaka kutajwa jina lake kwa sababu za kiusalama, alieleza kuwa maamuzi mengi ya Serikali sasa yanafanyika kwa simu, barua pepe, na vikundi vya WhatsApp.
"Kuna kazi zinazofanywa kwa njia za mtandao ambazo zinawafanya viongozi waandamizi wasiwe Dodoma mara kwa mara," alisema mtumishi huyo.
Hali hii imesababisha Wananchi kadhaa kukosa huduma za haraka, kwani maafisa wa chini waliopo Dodoma mara nyingi wanakosa mamlaka ya kufanya maamuzi muhimu.
"Tabia hii ya kusafiri mara kwa mara inaonekana kuigwa kutoka kwa Viongozi wa Juu, ambaye pia mara nyingi hayupo Dodoma kwa shughuli rasmi," anasema mmoja wa Wananchi.
Jambo lingine la kujiuliza ni kuhusu gharamia safari za viongozi zinazotumika inaonekana kama hali hiyo inaweza kupunguza utendaji wa Watumishi wa Serikali pamoja na miradi yake.
Hali hiyo inaweza kushusha kasi ya ukuaji wa Mji wa Serikali wa Mtumba, ambao ulitarajiwa kuwa kitovu cha shughuli za Serikali.
Hivi karibuni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipotembelea Mtumba kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo ya Serikali, alijionea wazi majengo mengi bado hayajakamilika.
Mfano wa Baraza la Mitihani (NECTA), Mkurugenzi wake amekuwa akitangaza matokeo ya mitihani akiwa Dar licha ya ofisi za taasisi hiyo kuwa Dodoma.
Mawaziri na Makatibu Wakuu wengi wao wanaishi Dodoma kipindi cha Bunge pekee kuliko wakati mwingine.
Nitoe wito kuwa inahitajika juhudi za dhati ili kuhakikisha Dodoma inakuwa na maana halisi kama Makao Makuu na siyo jina tu.
Serikali inapaswa kuhamasisha viongozi na taasisi kufikia viwango bora vya utendaji na kuhakikisha kwamba mji mkuu unakuwa na ushawishi wa kivitendo katika utawala wa Serikali.
Ikiwa Viongozi hawawezi kuwepo Dodoma mara kwa mara, basi ni bora Serikali irudi Dar ili kupunguza gharama na usumbufu unaowakumba Wananchi.
Dodoma iliteuliwa kuwa Makao Makuu ya Nchi mwaka 1973 lakini utekelezaji wake ulianza rasmi chini ya uongozi wa Rais Magufuli. Wananchi sasa wanataka Rais Samia kufuata nyayo hizo kwa kuhakikisha viongozi wanazingatia majukumu yao ya kuwa makao makuu ili kurejesha heshima ya Dodoma.