Yoyo Zhou
Senior Member
- Jun 16, 2020
- 126
- 215
Serikali ya Uingereza imetangaza kuwa kuanzia tarehe 31 Desemba mwaka huu, kununua vifaa vya teknolojia ya 5G kutapigwa marufuku, na vifaa vyote vya kampuni ya Huawei vya teknolojia ya 5G vitaondolewa nchini Uingereza kabla ya mwisho wa mwaka 2027. Hatua hii inaonyesha kuwa Uingereza imesujudu kwa shinikizo la Marekani, ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikitaka nchi hiyo iache kushirikiana na kampuni ya Huawei.
Marekani imekuwa ikiiandama kampuni ya Huawei hasa kutokana na kuwa kampuni hiyo imekuwa na nafasi nzuri ya ushindani kwenye soko la maendeleo ya teknolojia za kidigitali duniani, na kuwa na mbele ya Marekani. Hofu kubwa ya Marekani dhidi ya kampuni hiyo ni kwamba itachukua nafasi yake ya uongozi dunia kwenye mambo ya digitali.
Marekani imekuwa inatumia kisingizio kuwa China inaitumia kampuni ya Huawei kufanya shughuli za kijasusi, na kutumia kisingizio hicho kuzishawishi nchi mbalimbali duniani na hata kuzitishia kuzichukulia hatua nchi zitakazoshirikiana na China kwenye teknolojia ya 5G. Lakini mara kwa mara imethibitishwa na watalaamu wa maswala ya usalama wa kimtandao kuwa kampuni ya Huawei haijishughulishi na maswala ya ujasusi, ni kampuni ya mambo ya kidigitali kama ilivyo kwa makampuni mengine.
Tukiangalia kwa undani tunaweza kujua kuwa tukio hili si jipya, ni tukio linalojirudia duniani likiishirikisha Marekani kwa mara nyingine. Huko nyuma kampuni ya umeme ya Ufaransa Alstom iliyokuwa kampuni kubwa na ya muhimu kwa nchi hiyo, ililazimishwa kutoa fidia ya dola za kimarekani milioni 700, na kuuza asilimia 70 ya hisa zake zote kwa kampuni ya General Electric, iliyokuwa mshindani wake mkubwa nchini Marekani.
Kilichotajwa ni kuwa mkuu wa kampuni hiyo Bw Frederic Pierucci alifanya makosa nchini Indonesia yaliyokwenda kinyume na sheria ya Marekani ya ufisadi wa makampuni nje ya nchi iliyopitishwa mwaka 1977, ambayo kampuni yoyote yenye shughuli zake Marekani inaweza kuchukuliwa hatua kama ikifanya makosa nje ya Marekani. Sheria hiyo imeyakumba makampuni zaidi ya 29, lakini kati ya hayo 15 ni ya Ulaya, 6 ni ya Marekani na 8 ni kutoka sehemu nyingine tofauti tofauti.
Mazingira ya kufikilisiwa kwa kampuni ya Alstom ya Ufaransa, kimsingi yalikuwa yanalenga kuilinda kampuni ya General Electric ambayo licha ya kuwa mshindani wake aliondolewa sokoni, bali pia iliongezewa mtaji wa asilimia 70 ya hisa kutoka kwa kampuni ya Alstorm.
Tunachokiona kwenye mvutano kati ya kampuni ya Huawei na Marekani, hakina tofauti na mambo yaliyotokea huko nyuma. Kukamatwa nchini Canada kwa ofisa mkuu wa kampuni ya Huawei anayeshughulikia mambo ya fedha Bibi Meng Wenzhou, hakukutajwa kuwa ni sababu za kijasusi bali ni za “uhalifu wa kifedha”, lakini kulionyesha wazi kuwa Marekani inaisakama kampuni hiyo na kutaka kuiondoa kwenye ushindani kwenye sekta ya mambo ya digitali.
Kwa sasa wakati inaonekana kuwa Uingereza ambayo mwanzo ilifanya uamuzi wa kujitegemea bila kuingiliwa na Marekani, imeamua kufuata nia ya serikali ya Marekani na kupuuza maslahi ya watu wake na maendeleo ya 5G.