BUSH BIN LADEN ametoa mifano ahi wa kuonyesha umafia wa ma YANKEE (Gringos) si kwa Uchina tu bali kwa Urusi, Ufaransa na Ujerumani - binadamu gani anawagehuka hata rafiki wake wa karibu, anawakumbuka tu anapotaka kuvamia/pigana vita na Banana Republics, mfano: Iraq,Afghanistani, Syria walitaka kuivamia Venezuela wakagwaya kutoka na uwepo wa Urusi na Uchina.
Mwaka jana nilimuona kwenye luninga a former Alstrom CEO, mfaransa huyo ingawa hivi sasa amezeeka sana lakini alikuwa anatahadhalisha Dunia hasa kampuni za Uchina kwamba Amerika ni Taifa ambalo halitaki kabisa ushindani wa biashara kwa maneno mengine hawataki Makampuni ya USA kuzidiwa kete na Mataifa mengine wapo radhi hata to kill rivals ili wakidhi matakwa yao - hiki ndicho kinaendelea baina ya kampuni ya Huawei na Serikali ya Trump, kampuni ya Gasprom (Urusi) na Serikali ya Trump, Amerika iliwahi kutaka kuingilia Kampuni ya Urusi inayo zalisha products za Aluminium kwa wingi Duniani, walitaka eti Managing Director wake abadirishwe - akili gani hizi?
Mwisho nimalizie kwa kusema kwamba wewe unahoji eti "China ina ubunifu gani zaidi ya wizi!!"" unarudia propaganda zile zile za media za magharibi - unacho sahau ni kwamba masuala ya teknolijia to put into practice principles za physics, hakuna physics za Kichina,Kimerikana wala Urusi,vyuo vikuu vyote Duniani ufundisha kanuni zile zile tofauti ni lugha tu, sasa nikiona watu na akili zao timamu wanawasema vibaya wachina as if hawana akili za kujiendeleza kiteknolojia nawashangaa sana, Amerika unikumbusha imani ya Wamasai kwamba Ngombe wote Duniani belogs to them au mwanangu aliye wahi kuniambia kwamba magari yote Duniani ni TOYOTA i.e hakuna kampuni yoyote yenye uwezo wa kuunda magari zasidi ya Toyota, baadhi ya members wa JF wana amini the World is Amerika uwambii kitu wakakusikiliza. Eti: Wachina wezi! Mbona Wachina wana teknolijia ya mawasiliano ya kisasa kabisa(5G) ambayo USA hawana kabisa au unataka kusema Wachina wanaiba teknolojia ambayo USA hawana - hivi hii inaingia akili kweli? Vile vile Wachina wana latest Hypersonic missiles kitu ambacho USA hawana, mbona hayo hamuyasemi - mnakazania Wachina wezi,wezi - kisa? Wamerika wamesema hivyo, yaani mnachukulia madai ya US dhidi ya Taifa la Uchina as if madai hayo ni Gospel truth.