Uangalie muundo wa Tume Huru ya Uchaguzi halafu tafakari mwenyewe

Nashauri neno Mh. kwasasa lisitumike litumike neno ndugu,mwalimu,dk,injinia nk. Neno mh. lipumzishwe kwanza maana hao waheshimiwa hawaeleweki
 
Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi anapelekewa matokeo atangaze. Mamlaka yake ni madogo sana.
 
Kuna watu walikuwa Wana mtuhumu JPM kwa udini, ila huyu naye ndiyo walewale

Tena ameongeza sifa nyingine ya kuendekeza Uzanzibari wake katika teuzi

Yaani katika wajumbe 6, kutoka Bara ni 2 na 4 wote wametokea Zanzibar 🙌

Kwasisi tuliosoma Hesabu 33.3% Tanzania Bara huku 66.7% ni Wazanzibar
 
Hivi Asina ni Mzanzibari? Naomba kujuzwa tu. Mapuri na Mbarouk ni wazanzibari.
 
Hivi tume iliyopita ikampa Jiwe ushindi wa kutisha ilikuwa na wajumbe gani ati!
Kama hutojali tuwekee hapa pia kwa mchanganuo Kama huo wa wazanzibari na wabara wangapi.
Waislamu na wakristo wangapi
 
Tunapoteza hela za uchaguzi...type hio hela tugawane
 
Owky tumeiacha udini ila kwa nini hakuna usawa kwenye representation ya tume? Unakuwaje na wajumbe wapiga kura wanne kutoka upande mmoja wa muungano wakati ni fika uchaguzi ni jambo nusu la muungano? Kuna uchaguzi wa wabunge wa Tanganyika kuja kwenye bunge la Muungano. Hilo sio jambo la Muungano na ndio maana Zanzibar Wana tume yao. Wanachagua wampendae.

Haki inatakiwa kuonekana imefanyika mpaka kwa macho. Atleast 3 from each side hata kama ni kujipendelea.
 
"Wajumbe wengine wanne (4) wanatakiwa wawe na uelewa wa kutosha kuhusiana na kusimamia nakuendesha Uchaguzi wa Wabunge au sifa nyingine kama ambavyo Rais wa Jamhuri ya Muungano atakavyoona inafaa kwa ajili ya kuendesha shughuli za Tume"!
Hii sifa wanaipata toka wapi au chuo gani! Uchaguzi hufanyika kila baada ya miaka mitano kabla ya wao kuteuliwa wanakwenda wapi kusomea ili wawe na sifa! Hata hivyo hiyo tume haina sifa ya kuitwa "tume huru" kwani ni ile ya zamani ila ilisilimu usiku na asubuhi ikaitwa "tume huru"!
 
Chukueni mfano wa jirani yetu Kenya. (1) Kuwa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti (2) Kuwa Kamishna wa Tume Huru pia unapaswa kuomba nafasi hiyo. Nafasi hiyo inatangazwa HADHARANI kwenye vyombo vya habari, Magazeti na popote ambapo wananchi watapata taarifa hiyo. Na lazima uwe Jaji au mtu mwenye elimu ya Sheria. (2) Kuwa Kamishna wa Tume Huru pia lazima uombe nafasi hiyo na matangazo yanatolewa kupitia vyombo vya habari na magazeti. (3) Kuna jopo la watalaam wanaoteuliwa kuwafanyia usaili na kwa nafasi ya Mwenyekiti na Makamu mwenyekiti kila nafasi wanateuliwa washindi wawili na orodha hiyo inapelekwa kwa Mhe. Rais ili ateue mshindi mmoja. Kwa nafasi ya Makamishna kama wanatakiwa kumi basi Mhe. RaIs anapelekewa orodha ya washindi kumi walioshinda kwenye usaili na Mhe. Rais anawateua watano.

Kutokana na utaratibu huu kuna uwazi na hakuna upendeleo. Tume yao inaundwa kila baada ya miaka 10. Juzi tayari wamemaliza kuunda Tume yao kwa ajili ya uchaguzi wao wa 2027. Nashauri tuige mfano wao ili kuondoa malalamiko ya kila mara kuhusu Tume yetu Huru ya Uchaguzi.
 
Nani anateuwa jopo la wataalamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…