Ubabaishaji wa mfuko wa PSSSF

Ubabaishaji wa mfuko wa PSSSF

Lovren10

New Member
Joined
Feb 21, 2020
Posts
4
Reaction score
5
Kuunganishwa kwa mifuko ya PPF, LAPF, PSPF, GEPF n.k na kupata PSSSF limekua kaa la MOTO kwa wafanyakazi waliokua private sector na mda wa mikataba yao umekwisha. Nimekua nikifatilia sitahiki zangu tokea makataba wangu umekwisha pale PSSSF nikaambiwa kwa watu wa private wanatakiwa kuchukulia NSSF, eti ni utaratibu mpya.

Mie nilihoji why nikachukulie NSSF wakati pesa zote naziona mnazo PSSSF, Nikaambiwa ni utaratibu mpya. Baada ya kufatilia NSSF, Wao kama NSSF wamedai hawawezi kutoa hela kwakua hawana hizo pesa zimebakia PSSSF, Na PSSSF hawataki kuzitoa kwenda kwa mwananchi wala kwenda NSSF ambako mwananchi anatakiwa kuchukulia huko.

Mamlaka zinazohusika liangalieni suala hili kwa jicho la tatu. Nakumbuka tukiwa kazini hua mnakua kimbelembele sana kuja kudai hayo mafao hata kupelekea kwa waliochelewa kuwapiga fine/penati. PSSSF ni janga la Taifa kwasasa kwa wale tuliotoka private sector. Tambueni hela ni zetu sio zenu PSSSF.

Mamlaka zinazohusika tunaomba tatueni tatizo hili kwa ukaribu sana ikiwezekana kuweka sawa kati ya NSSF na PSSSF, na kuweza kutoa hizo pesa mapema iwezekananavyo
 
Kuna kitu kikubwa kinaendelea nyuma ya pazia , leo mwaka wa pili mtu hajalipwa mafao yake yaani kashakufa watoto wanahangaika hawana ada ni shida
 
Aisee hii mifuko kwa awamu hii haina msaada tena
 
Za chini ya kapeti ni kwamba mifuko hiyo imekauka. Hata hotuba ya rais juzi kwa madokta alizungumzia suala la mifuko hiyo kwa lugha ya mafumbo kwamba mifuko inadai pesa.
 
Aisee ili ni bomu kubwa bwana zmekuja sarakasi za fao la kukosa ajira hakuna anayelipwa imekua sarakasi time will tell
 
Niliwahi kusema hapa watu wanaotegemea mafao yao hasa wa private sector amkeni.Mchakato umekuwa mgumu sana mtu kupata pesa yake
 
Sheria mpya ya mafao inakandamiza wanachama.Lakini serikali ilisema imesitisha utekelezaji wa sheria mpya lakini tayar ilishaanza kufanya kazi
 
Niliwahi kusema hapa watu wanaotegemea mafao yao hasa wa private sector amkeni.Mchakato umekuwa mgumu sana mtu kupata pesa yake

Kutokana na hofu itakayojengwa na hizi sheria za mafao, wizi utatamalaki kwa watumishi wa uma hasa wanaotarajia kustaafu siku za karibuni.

Hata mimi inanibidi nizidishe mapambano ili nikiondoka niwe huru kuishi bila kujinyongesha kwa hawa madhalimu wa sasa wanaojitapa kunipigania.
 
Hali ni mbaya PSSSF WASTAAFU WENGI WAMENYIMWA PENSHION ZAO FEBRUARY ETI WAME HAKIKI BAADAYA 21/1/2020 japo ni kabla ya tarehe 31/1/2020. Hii nidhulumati na wapo walio hakiki 31/1/2020 wamelipwa. Zoezi lilikuwa linaendele January yote sasa itakiwaje wa suspend malipo ya wengi hasa wenye miaka zaidi ya 65.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii mifuko itaangamia kwa laana za hao wazee na watakaopoteza maisha kwa maradhi yatokanayo na kukosa pensheni.

Hii nchi siioni ikivuka salama bila kuingia kwenye machafuko na mauaji yanayolazimishwa na Magufuli.

Kitu wasichokijua hawa wanasiasa wapumbavu ni kuwa nchi ikishaingia kwenye machafuko yatokanayo na laana, itadumu kwenye machafuko kwa miaka hamsini au zaidi.

Kaitazameni Kongo au Somalia.
 
Daah pole Sana braza , pesa yako lakini watu wanakunyanyasa , kweli sisi ni shit hole country, so sad indeed , viongozi wananyanyasa Raia badala ya kuwasaidia , kweli aliyeshiba hamjui mwenye njaa
 
Hali ni mbaya PSSSF WASTAAFU WENGI WAMENYIMWA PENSHION ZAO FEBRUARY ETI WAME HAKIKI BAADAYA 21/1/2020 japo ni kabla ya tarehe 31/1/2020. Hii nidhulumati na wapo walio hakiki 31/1/2020 wamelipwa. Zoezi lilikuwa linaendele January yote sasa itakiwaje wa suspend malipo ya wengi hasa wenye miaka zaidi ya 65.

Sent using Jamii Forums mobile app

Mwendo mdundo tu,mambo ya PSSSF.
 
Back
Top Bottom