Ubabe wa watawala wetu umepaisha umaarufu wa vyombo vya habari vya nje vya BBC, DW na VoA!

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Posts
15,843
Reaction score
31,057
Tokea watawala wetu watangaze kanuni zao za "kipuuzi" kuwa kuanzia sasa, hakuna chombo cha habari hapa nchini kurusha matangazo na vyombo vya habari vya washirika toka nchi za nje, hadi kwanza wapate kibali toka mamlaka ya TCRA, wamepaisha mno umaarufu wa vyombo hivyo vya nje maradufu bila ya wao kujua.

Kila Mtanzania hivi sasa hata yule ambaye alikuwa hana kawaida ya kusikikiza vyombo hivyo vya habari, ana hamu kubwa ya kusikiliza maudhui ya habari za BBC, DW, VoA na vyombo vingine vya habari vya vya kimataifa vya nje.

Siri kubwa kwa vyombo hivyo vya habari vya nje ambavyo umefanya wawe na wapenzi wengi hapa nchini ni kuzingatia weledi wa taaluma yao ya habari ya "kubalance story" na kutotaka kabisa kuegemea upande wa kutoa mema pekee ya watawala, tofauti na vyombo vya habari vya hapa nchini, ambavyo vyenyewe "vimelazimishwa" kuimba mapambio ya kusifu na kuabudu mazuri pekee ya serikali hii ya awamu ya 5

Hiyo ndiyo imekuwa sababu kubwa iliyosababisha shauku kubwa mno ya wasikilizaji na watazamaji ya Watanzania kuwa na hamu kubwa mno ya kusikiliza maudhui ya vipindi hivyo vya mashirika ya habari ya nje ambayo yamesababisha watawala wetu hadi waingie "mchecheto" hadi kusababisha wawapige "stop" mashirika ya habari ya ndani ili wasiendelee kueneza maudhui yao kwa wasikilizaji na watazamaji, ni ile shauku ya kuangalia ni kitu gani kimo kwenye maudhui ya vipindi hivyo vya mashirika ya nje ya habari, hadi watawala wetu washikwe na "kihoro" hadi kulazimisha kuvifungia vyombo hivyo vya habari vya nje visisikike tena hapa nchini!

Kila Mtanzania hivi sasa, hata kwa wale waliokuwa hawasikilizi kabisa vipindi kama vile Dira ya dunia na amka na BBC, Meza ya duara ya DW na vipindi vingine vya vyombo hivyo vya habari vya nje, vimekuwa lulu mno kwa watanzania, ambavyo hakuna mtanzania hata mmoja, anayependa vimkose.

Kuna principle moja kubwa kwenye sekta ya habari ya "kubalance story" ambavyo kwenye sekta ya habari nchini haipo na badala yake vyombo vyetu vya habari vya ndani, vinapata kibano kizito na "kulazimishwa" kutangaza habari za "kusifu na kuabudu" kwa massa 24 ya mazuri pekee yanayofanywa na watawala wetu wa serikali hii ya awamu ya 5!

Jambo lingine ambalo ni lazima watawala wetu watambue ni kuwa kwa vitendo vyao, wameshusha mno umaarufu wa vyombo vyetu vya habari vya ndani, kama vile maudhui ya vipindi yanayofanywa na chombo cha habari cha Umma wa watanzania TBC, ambacho chenyewe kinachojua toka asubuhi hadi jioni ni "kusifu na kuabudu" ya kile kinachoitwa mafanikio ya serikali ya awamu ya 5.

Kanuni kubwa iliyoweza kuvipaisha vyombo vya habari vya nje na kushusha umaarufu wa vyombo vya habari vya ndani, ni ile inayosema KIZURI CHAJIUZA na KIBAYA CHAJITEMBEZA.

Kila mtanzania hivi sasa ndiyo ameng'amua hali ngumu sana wanayopambana nayo ya vyombo vya habari vya ndani na kufanya "editors" wawe katika mazingira magumu mno ya kufanyia "censorship" ya habari zao za vyombo vyao habari baada ya "kulazimishwa" kutangaza mazuri pekee ya Jiwe na serikali yake na kuwafanyia "blackout" wale wote ambao wanaikosoa serikali hii wakiwemo viongozi wa vyama makini vya siasa vya Chadema na ACT Wazalendo.

Kwani siyo siri tena kuwa "Media House" ya nchi hii, wanaona kumtangaza mgombea Urais wa Chadema, Tundu Lissu, kwa mema, ni sawasawa na kukihatarisha chombo chao cha habari kufungiwa, wakati wakimtangaza kwa masaa 24, mgombea Urais wa CCM hata anapotafuna hindi la kuchoma hadharani!

Mfano mzuri ni kuyafungia magazeti makini ya Tanzania Daima na Mwanahalisi kwa kile kinachoitwa na watawala wetu kuwa magazeti hayo yanaandika habari za uchochezi na kuliacha likiendekea "kujimwambafai" gazeti linaloongoza hapa nchini kwa kuleta uzushi, chuki na utengano wa kitaifa la "kijarida cha Tanzanite" ambacho kimeendelea kwa nguvu zote "kusifu na kuabudu" mafanikio ya serikali hii ya awamu ya 5

Kwani watawala wetu wameingilia "Media House" ya nchi hii na kuwabadilishia kanuni ya kuviendesha vyombo hivyo vya habari vya hapa nchini ya kuwa badala ya habari inayouzika kwa jamii ndiyo ya kuitangaza. badala yake wameweka wao kanuni yao na "kuvilazimisha" kutangaza habari wanayoiona wao ni ya kizalendo ya kutangaza masaa 24 mfululizo ya yanayoitwa mafanikio makubwa ya uongozi wa serikali hii, aka kishindo cha awamu ya 5

Niwausie hawa watawala wetu kuwa kama vile kanuni ya kibinadamu inayosema kuwa kizuri chajiuza na kibaya chajitembeza, siyo vyema hata kidogo "kutulazimisha kututembezea" kuangalia TBC, kwa kuviondoa kwenye ving'amuzi vyombo vya habari vya ndani makini vya Azam TV na ITV, ambavyo "vinabalance story" .na kuona ni habari gani ni ya kuipa "priority" kuitangaza na habari gani haina umuhimu wa kuipa kipaumbele
 
Awamu hii Tanzania tumepata kiongozi wa ajabu sana, analazimisha kuwaongoza watu wazima kama watoto wake nyumbani, kitu ambacho hakiwezekani.
denooJ
Na kibaya zaidi ni pale unapoona wasaidizi wake, wanaamua kuziweka taaluma zao pembeni na kuamua kucheza mdundo wa ngoma inayopigwa na Bosi wao!
 
Huyu mtawaka tuliye naye hivi sasa, ni mtawala wa ajabu ambaye Taifa hili halijawahi kuwa naye!

Kwa kuwa katika utawala bora wa Taifa lolote duniani wanaruhusu "constructive criticism" kwani ndiyo nijia pekee ya kusahisishwa pale unapoonekana hukufanya sawa na hivyo kusababisha Taifa hilo kupiga hatua kimaendeleo...

Badala yake mtawala huyu anataka vyombo vyote vya habari vya ndani ya nchi na vile vya nje ya nchi viimbe mapambio ya "Praise & worship" kwa masaa 24 kwa kile kinachodaiwa ni mafanikio ya utawala wake na yule atakayeonekana anakosoa ndani ya utawala wake anakiona cha moto!
 
ukiwa muongo na muovu mara zote huishi kwa hofu ya kuumbuka. hali hiyo ndio inayo itesa serikali ya Magufuli. miaka mitano waliona haita isha wakaziba mdomo kila mtu wakabaki wenyewe wakilisha watu matangu poli wakifikiri baada ya miaka mtano kila mtu atakuwa anakula matangu poli kama bila kujuwa kama ni matangu poli. Sasa Lissu kaja kufundisha watanzania tafauti ya tangu poli na boga. matangu poli hayana soko tena. Magufuli anahaha kuokowa soko lake la matangu poli kwa kuzuwia watu wasijuwa utamu wa boga. jee atafanikiwa? hakuna ujawaye.
 
Walichofanya watawala wetu ni namna ya "kuviadvertise" na bonge la "promo" kwa vyombo hivyo vya habari vya nje, vya BBC, DW na VoA, bila wenyewe watawala wetu kujua!
Sasa bbc tunaweza kuwapataje mngetupa mwongozo tuingie wapi tusikilize taarifa zao maana Sasa hv tupo gizan
 
Serikali ya ccm na watumishi wake ni nazi inayo jiamini kuwa imekomaa bara bara so inaanza kujiongopea kuwa inaweza kulivunja JIiwe (mabeberu)

Hivyo vyombo vya habari vyote ni vya mabeberu watakapo chafuka na kuitoa ccm madarakani msije anza kulia lia tu nakudai kuwa mmeonewa
 
Tokea watawala wetu watangaze kanuni zao za "kipuuzi" kuwa kuanzia sasa, hakuna chombo cha habari hapa nchini kurusha matangazo na vyombo vya habari vya washirika toka nchi za nje, hadi kwanza wapate kibali toka mamlaka ya TCRA, wamepaisha mno umaarufu wa vyombo hivyo vya nje maradufu bila ya wao kujua.

Kila Mtanzania hivi sasa hata yule ambaye alikuwa hana kawaida ya kusikikiza vyombo hivyo vya habari, ana hamu kubwa ya kusikiliza maudhui ya habari za BBC, DW, VoA na vyombo vingine vya habari vya vya kimataifa vya nje.

Sababu kubwa iliyosababisha shauku kubwa mno ya wasikilizaji na watazamaji ya Watanzania kuwa na hamu kubwa mno ya kusikiliza maudhui ya vipindi hivyo vya mashirika ya habari ya nje ambayo yamesababisha watawala wetu hadi waingie "mchecheto" hadi kusababisha wawapige "stop" mashirika ya habari ya ndani ili wasiendelee kueneza maudhui yao kwa wasikilizaji na watazamaji, ni ile shauku ya kuangalia ni kitu gani kimo kwenye maudhui ya vipindi hivyo vya mashirika ya nje ya habari, hadi watawala wetu washikwe na "kihoro" hadi kulazimisha kuvifungia vyombo hivyo vya habari vya nje visisikike tena hapa nchini!

Kila Mtanzania hivi sasa, hata kwa wale waliokuwa hawasikilizi kabisa vipindi kama vile Dira ya dunia na amka na BBC, Meza ya duara ya DW na vipindi vingine vya vyombo hivyo vya habari vya nje, vimekuwa lulu mno kwa watanzania, ambavyo hakuna mtanzania hata mmoja, anayependa vimkose.

Kuna principle moja kubwa kwenye sekta ya habari ya "kubalance story" ambavyo kwenye sekta ya habari nchini haipo na badala yake vyombo vyetu vya habari vya ndani, vinapata kibano kizito na "kulazimishwa" kutangaza habari za "kusifu na kuabudu" kwa massa 24 ya mazuri pekee yanayofanywa na watawala wetu wa serikali hii ya awamu ya 5!

Jambo lingine ambalo ni lazima watawala wetu watambue ni kuwa kwa vitendo vyao, wameshusha mno umaarufu wa vyombo vyetu vya habari vya ndani, kama vile maudhui ya vipindi yanayofanywa na chombo cha habari cha Umma wa watanzania TBC, ambacho chenyewe kinachojua toka asubuhi hadi jioni ni "kusifu na kuabudu" ya kile kinachoitwa mafanikio ya serikali ya awamu ya 5.

Kanuni kubwa iliyoweza kuvipaisha vyombo vya habari vya nje na kushusha umaarufu wa vyombo vya habari vya ndani, ni ile inayosema KIZURI CHAJIUZA na KIBAYA CHAJITEMBEZA.

Kila mtanzania hivi sasa ndiyo ameng'amua hali ngumu sana wanayopambana nayo ya vyombo vya habari vya ndani na kufanya "editors" wawe katika mazingira magumu mno ya kufanyia "censorship" ya habari zao za vyombo vyao habari baada ya "kulazimishwa" kutangaza mazuri pekee ya Jiwe na serikali yake na kuwafanyia "blackout" wale wote ambao wanaikosoa serikali hii wakiwemo viongozi wa vyama makini vya siasa vya Chadema na ACT Wazalendo.

Kwani siyo siri tena kuwa "Media House" ya nchi hii, wanaona kumtangaza mgombea Urais wa Chadema, Tundu Lissu, kwa mema, ni sawasawa na kukihatarisha chombo chao cha habari kufungiwa, wakati wakimtangaza kwa masaa 24, mgombea Urais wa CCM hata anapotafuna hindi la kuchoma hadharani!

Mfano mzuri ni kuyafungia magazeti makini ya Tanzania Daima na Mwanahalisi kwa kile kinachoitwa na watawala wetu kuwa magazeti hayo yanaandika habari za uchochezi na kuliacha likiendekea "kujimwambafai" gazeti linaloongoza hapa nchini kwa kuleta uzushi, chuki na utengano wa kitaifa la "kijarida cha Tanzanite" ambacho kimeendelea kwa nguvu zote "kusifu na kuabudu" mafanikio ya serikali hii ya awamu ya 5

Kwani watawala wetu wameingilia "Media House" ya nchi hii na kuwabadilishia kanuni ya kuviendesha vyombo hivyo vya habari vya hapa nchini ya kuwa badala ya habari inayouzika kwa jamii ndiyo ya kuitangaza. badala yake wameweka wao kanuni yao na "kuvilazimisha" kutangaza habari wanayoiona wao ni ya kizalendo ya kutangaza masaa 24 mfululizo ya yanayoitwa mafanikio makubwa ya uongozi wa serikali hii, aka kishindo cha awamu ya 5

Niwausie hawa watawala wetu kuwa kama vile kanuni ya kibinadamu inayosema kuwa kizuri chajiuza na kibaya chajitembeza, siyo vyema hata kidogo "kutulazimisha kututembezea" kuangalia TBC, kwa kuviondoa kwenye ving'amuzi vyombo vya habari vya ndani makini vya Azam TV na ITV, ambavyo "vinabalance story" .na kuona ni habari gani ni ya kuipa "priority" kuitangaza na habari gani haina umuhimu wa kuipa kipaumbele
Huu sio ubabe bali ni upumbavu wa watawala wetu!
 
ukiwa muongo na muovu mara zote huishi kwa hofu ya kuumbuka. hali hiyo ndio inayo itesa serikali ya Magufuli. miaka mitano waliona haita isha wakaziba mdomo kila mtu wakabaki wenyewe wakilisha watu matangu poli wakifikiri baada ya miaka mtano kila mtu atakuwa anakula matangu poli kama bila kujuwa kama ni matangu poli. Sasa Lissu kaja kufundisha watanzania tafauti ya tangu poli na boga. matangu poli hayana soko tena. Magufuli anahaha kuokowa soko lake la matangu poli kwa kuzuwia watu wasijuwa utamu wa boga. jee atafanikiwa? hakuna ujawaye.
Hahahahaa
 
Back
Top Bottom