Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Uwekezaji wa Hospitali si uwekezaji wa kitoto , si uwekezaji wa bei rahisi na wala si uwekezaji wa kudra za Mungu , ni gharama kubwa mno , siyo sadaka za Waumini waliofanyiwa miujiza na Mungu , ni hela nyingi inatumika
Mimi ni Mfanyabiashara na natambua umuhimu wa Afya za binadamu , lakini ni lazima serikali iwajibike kwenye afya za watu wake , isitake kukandamiza Wenye Hospitali , jambo hili tukilinyamazia tutakuwa tunaunga mkono Unyonyaji uliojaa uonevu .
Kwanza Hospitali zilizofanya kazi na NHIF kwa muda wote huo zipongezwe , zimekuwa zikisubiri malipo hadi miezi 6 bila mafanikio , yaani unatoa huduma halafu unaenda NHIF ukapige magoti au utoe rushwa ndio ulipwe , huu ni uzalendo wa ajabu mno , haya mambo hayasemwi lakini huu ndio ukweli wenyewe .
Si rahisi kuendesha Hospitali , kwa maana ya majengo , vifaa , dawa na Wataalam wabobezi wanaolipwa pesa nyingi sana , ni lazima serikali iangalie jambo hili kwa mapana na marefu , njia za kibabe zitazidisha tatizo .
Njia pekee ni majadiliano tena ya fifty fifty , Serikali isijaribu kutoa maelekezo ya kukomoa Hospitali Binafsi , haitawezekana na wala haitasaidia chochote .