JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Jumuiya ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) imesema moja ya mambo yaliyosababisha shule inazozimiliki kushuka kitaaluma na baadhi yake kuwa katika hatari ya kufungwa, ni ubadhirifu uliofanywva na baadhi ya viongozi wasiokuwa waaminifu.
Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, Gilbert Kalima amebainisha sababu hizo Jijini Mbeya alipokuwa anatangaza matokeo ya mtihani maalumu wa kuwapima wanafunzi wa kidato cha sita wanaosoma kwenye shule 14 za Jumuiya hiyo nchini.
Alisema baadhi ya wasimamizi wa shule hizo waliokuwa wameaminiwa na Jumuiya hiyo ndio waliofanya ubadhirifu huo ambao umezifanya shule hizo kuwa na hali mbaya na kwamba baadhi yake zimekimbiwa na wanafunzi.
Alizitaja sababu zingine kuwa ni serikali kuboresha shule zake za kata kwa kuhakikisha zinakuwa na miundombinu bora pamoja na vifaa vya kusomea hali ambayo imewafanya wazazi wengi kuanza kuziamini na kuwapeleka watoto wao huko.
Vilevile, alisema sera ya "Elimu Bila Malipo' inayotekelezwa na Serikali pia ni sababu mojawapoiliyosababisha shule za jumuiya hiyo kushuka kitaaluma kwa maelezo kuwa wazazi wengi wanawapeleka watoto wao kwenye shule za Serikali badala ya shule binafsi zikiwamo za jumuiya hiyo.
"Lakini sasa hivi tupo kwenye mikakati maalumu ya kuziboresha shule zetu zote ili sasa zirejee katika hali yake ya awali, moja ya mikakati ni kuimarisha usimamizi, kuboresha miundombinu ya shule na kuanzisha mitihani ya mara kwa mara kwa ajili ya kuwaandaa wanafunzi wetu," alisema Kalima.
Akitangaza matokeo ya mtihani huo maalumu, Kalima alisema ulishirikisha wanafunzi 1,202 ambao kati yao wanafunzi 984 ni watahiniwa wa shule na wengine 218 ni watahiniwa wa kujitegemea, na kwamba ambao hawakufanya mtihani huo walikuwa 37.
Alisema kwenye mtihani huo wanafunzi wamefanya vizuri kwa maelezo kuwa waliofaulu kwa kupata daraja la kwanza walikuwa 148, daraja la pili 394, daraja la tatu 369, la nne 33 na kwamba hakuna mwanafunzi aliyepata daraja sifuri.
Alizitaja shule tano vinara kuwa ni Wari Sekondari ya Mkoani Kilimanjaro, Shule ya Sekondari Mombo (Tanga), Shule ya Sekondari Ivumwe iliyopo Mkoani Mbeya, Shule ya Sekondari Mwembetogwa (Iringa) na Shule ya Sekondari Sangu (Mbeya).
"Shule ambazo ufaulu wake ni hafifu ni Shule ya Sekondari Kasulu na Shule ya Sekondari Ujiji zote za Mkoani Kilimanjaro na Shule ya Sekondari Mwanga iliyopo mkoani Kilimanjaro, hizi tumetoa maelekezo maalumu kwa walimu na bodi za shule ili waongeze ufaulu," alisema Kalima.
Alisema jumuiya hiyo haina mpango wa kuziuza wala kuzibadilisha matumizi shule hizo kama ilivyokuwa inazungumzwa mitaani na kwamba uvumi huo ulisababisha baadhi ya wazazi kuwa na wasiwasi na kuamua kuwahamishia watoto wao kwenye baadhi ya shule.
Source: Nipashe