Ubaguzi: Machotara Hizbu, Zanzibar ni nchi ya Waafrika

Nashukru nilikaa huko,ukweli unauma lakini wanayoyafanya vijana wa Zanzibar hasa CCM ni hali yao ya ukosefu wa elimu. Lakini kinachoniachaga hoi bila jibu ni kuwa; asilimia zaidi ya 90% Wazanzibar ni waislamu,wanasali pamoja na mafundisho yao kiimani ni mamoja. Unashangaa hili bango!!? Zanzibar ukiwa na kichwa cha chogo hata kama ni mmakonde utaitwa Mpemba na unaweza kupatwa hata na mkong'oto kutoka kwa vijana wa CCM wakifikiri ni mpemba.
 
UNAFKI MKUBWA ndivyo navoweza kuanza. Tumeona wawakilishi na mawaziri wengi machotara ukiwa CCM ni mzalendo. Nje ya hapo utabaguliwa na kuitwa majina ya kibaguzi. CCM imebaki na akili hizo iwe Zanzibar na hata bara ukionekana tishio kwa uhai wa ccm utaanzishiwa lugha za kibaguzi (ukabila, ngozi na kidini) kwa ujumla ni manyani yasioweza kuona matatizo yao huku wakitaka kusuhisha wengine wakati ya hapa kwetu tu hawawezi kupata suluhu.
 
Chotara hizbu zanzibar si nchi ya wazungu. Chotara hizbu zanzibar si nchi ya waarabu. Chotara hizbu zanzibar si nchi ya wachina na nk.

Sasa wameandika Chotara hizbu zanzibar ni nchi ya Waafrika.

Ubaguzi ni wa kulaaniwa lakin katika hili sioni wapi ulipo hasa ukitilia maanani kuwa mtawala wa kabla ya Mapinduzi alikuwa mwarabu na kuna hisia kuwa anataka kurudi tena. Kuna ubaya gani kuwaambia wa zanzibar wenzao wanao shabikia kurudi kwa sultani kuwa zanzibar si nchi ya kiarabu bali ya kiafrika?
 
Mzee Mohamed Said yuko AzamTv muda huu akijidai kuwa yeye sio mbaguzi
 
Nenda ulaya utakuta zile nchi ni za wazungu. Nenda uarabuni utakuta zile nchi ni za waarabu. Lakini haimaanishi kuwa kule watu wa rangi na asili tofauti hawakaribishwi na kupewa uraia la hasha. Na ndio pia tufanyavyo hapa barani Africa.

Watu wa mabara yote wako hapa. Ni shwari kwetu na kwao. Lakini hizi nchi zetu pamoja na zanzibar ni nchi za kiafrika.

Tusilionee aibu hili
 
Kila mtu anamtaka Rais Magufuli aingilie kati. Hana ubavu huo. Someni katiba ya Zanzibar. Hata kichama, mwenyekiti wa ccm ndiye mwenye mamlaka. tusihamishe magoli. Magufuli hahusiki kabisa ktk mgogoro huu huu wa kisiasa. Wajibu wake ni kuhakikisha amani na utulivu vinatamalaki.

Ni kweli Zanzibar imepasuka katikati na kwa misingi ya ubaguzi. Wote tumelipalilia na kulikuza. Kwa mfano, mantiki ya kuendelea kuwa na baraza la mapinduzi ni nini miaka 50 na ushee. Pia watu gani wanahodhi uchumi wa Zanzibar. Mwenye kutawala uchumi ndiye atakayetawala siasa. Katika hili huenda ccm wakaisoma namba. Nguvu ya kiuchumi ya cuf inakua kila kukicha na wamepanua matawi ya kiuchumi hadi bara. Tatizo siyo Shein au maalim Seif bali msukumo wa mwenye nguvu ya uchumi kutaka ahodhi siasa pia. Kwa Zanzibar kufanya hivyo kunasababisha mpasuko wenye kuleta sura ya kibaguzi.
 
Ukitazama bango hilo utagundua kabisa wakusudiwa hapo ni CUF kwa sababu ndani ya CUF ndio wanaonekana sana hao machotara,wanasahau kuwa kama wataanza kutazamana kwa uchotara robo 3 ya zanzibar wote machotara,
ukweli kuwa bara tunaamua mambo mengi ya zanzibar kama tungewaachia waamue mambo yao wenyewe sidhani kama yangefikia hayo,uchotara unawagusa wote Maalim seif ,Shein na Karume kwa jumla na wengi mno,
hili chokochoko linalopikwa hapo visiwani likija wiva tutashuhudia genocide nyingine afrika ajabu watu 1.2m wameshindwa kabisa kumaliza tofauti zao
 
Dhambi ya kwanza ni ile katiba yao iliyoibagua Tanganyika kiharamu kabisa, wakajiona "wao wazanzibar, sasa wameanza kushtuka kuwa kuna waarabu/machotara (wazanzibara na wazanzibari)" Dhambi ya ubaguzi haifi, itawatafuna mpaka watakapofumbua macho yao..!Maalim seifu hawezi hata kutangaza dukuduku lake zanzibar, anakuja serena hotel.. kuwambia nani habari za znz??:?
 
hapo msimtegemei Makufuli kuleta muafaka,hapo tegemeeni Makufuli kuzidisha mtafaruku kwa kuwa upande wa ccm na ndio mtakubaliana nami kwamba, Makufuli hana ubavu wa kuongoza nchi hii kwa haki
Ubaguzi walianza wao, kwa kuibagua Tanganyika. Magufuli hatakiwi kusuluhisha mgogoro wa znz anatakiwa awaache waliondaa katiba baguzi ya znz watatue mtafaruku. Znz ni nchi au umesahau....???
 
Hii ni dalili kuwa CCM hata Dr Shein mwenyewe hawamuheshimu.
Utapitishaje ujumbe wa kibaguzi na wa kuvunja sheria namna hii mbele ya Rais.
Hii ni ajabu sana.

Kwa kufanya hivi wanawatusi Wazalendo wa nchi hii waliochanganya damu zao

Wanamtusi Salim Ahmed Salim
Wanamtusi Balozi Ali Karume
Wanamtusi hata Abeid Karume kwa kuoa Chotara

Hii tabia ni ya kijinga na Ni ajabu sana, CCM ili iendelee kubaki madarakani wameamua kujiegemeza katika kigingi cha Ubaguzi.

CCM wameamua kuwagawa watu ili waendelee kubaki madarakani, hata hivyo hii ni kwa sababu wanatapatapa, hawana uhalali tena. WAZANZIBARI WAMEWAKATAA
 
ICC kama naiona asee nlikua siamini sasa nmeona
Hii isipotolewa kauli basi viongozi wakuu wa CCM waliwatuma kufanya haya
Haya ni ya kukemewa mchana kweupe tena kwa uso mkavu
Hii haikubaliki kabisa
 
Hujajadili hoja umejadili mtu rudi ujisahihishe ndipo uandike
 
Cha kushangaza hao viongozi wote wa CCM karibia wote wake zao ni machotora na watoto wa ni machotora.
Tifuaneni wenyewe tuone mwisho wake...vumbi likituama, shwari itarejea.
 
Zanzibar nchi huru watarudi vip waarabu mkuu mbona kama umeteleza kidogo
 
Tusingelikuwa tumeonywa na wanadunia wengine na hasa kutoka kwa Mwl. Nyerere wetu wenyewe juu ya ubaya na matokeo ya ubaguzi basi hata tungeliyafanya haya tusingelaumiwa sana. Hii inaonyesha Watanzania na hasa ccm tu wajinga kiasi gani, yaani mtu anakaa na kuchukua muda kuandika bango la kibaguzi kama hili!?? Kwa hakika historia itawahukumu!
....wait a moment ....jana nilimuona kiongozi mmoja wa ccm kwenye TV akiongelea juu ya mabalozi kususia sherehe hizi tata, Ukweli ni kwamba kama ni 'uarabu' (Mungu anisamehe kuendeleza ubaguzi kwa nia ya kueleweshana) basi yule ni mwarabu mara kumi kumzidi Seif!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…