Huo sasa ubaguzi, una agenda zako na wewe...uliposema hapo bora ukodishe panya kwa kuwa hio nyumba ina nini kikubwa?
Hao watanganyika wanaokuja zanzibar, wazanzibari nao wangesema hawawakodishi bora wakodishe panya si wangelala barabarani. Maana watanganyika wengine wanakuja zanzibar hawana hata issue, wanafuata mkumbo tu wa kuja kutafuta maisha Na huwa hawajui hata wataanzia wapi. Ndio wengine wakikuta nyumba hazijamaliza kujengwa wanavamia tu na kukaa hata kama hamna choo.
Kipindi naishi home mbweni, jirani kulikuwa kuna nyumba ndio kwanza imepauliwa tu...wakaja kuhamia wanyamwezi, walikuwa wanajisaidia kwenye mifuko na kutupa ovyo. Nyumba haina hata choo wala maji jiulize walikuwa wanakaa vp. Upande tuliokuwa tumepakana ukuta na hio nyumba kulikuwa kunanuka harufu ya uvundo. Sema tu walitukuta majirani hatuna midomo ya kugombana. Hapo bado usalama, ukisahau kitu nje asubuhi hukikuti washabeba