Ubaguzi uwanja wa ndege wa (JNIA)

Ubaguzi uwanja wa ndege wa (JNIA)

KAKA NASOKI

Senior Member
Joined
May 25, 2016
Posts
191
Reaction score
212
Leo tarehe 4Oktoba, 2021saa 11.15 Asubuhi nilisindikiza mtu Uwanjani anaenda Dodoma na Air Tanzania ya saa 12 Asubuhi. Watu walikuwa kwenye foleni ya kuingia, kuna Muhindi mmoja alivaa pensi na fulana nyekundu, mwenzie alishaingia yeye ni msindikizaji, nadhani kuna kitu alisahau kumwambia, alichofanya yule Muhindi ni kupita watu kwenye foleni hadi ndani bila mlinzi kumuuliza chochote wala kumkagua na hakuwa na tiketi.

Kilichoniuma zaidi mwenzie aliyekuwa naye huku nje alipoona jamaa anachelewa nae akaingia kumfuata na mlinzi akamuachia naye aingie.

Sasa nikajiuliza hivi magaidi au wanaoweza leta madhara pale Airport ni weusi tu? Sikuvumilia nilimuuliza yule mlinzi, mbona hawa wahindi unawaachia waingie na kutoka bila kukaguliwa?

Akajibu hiyo ni kazi yake. Ikiwa na maana anaamua yeye aingie nani asiingie nani. Wenye Mamlaka fuatilieni kwenye CCTV mtaona.
 
Ngoja mamlaka husika watakuja kukujibuuu

aina za ubaguzi
1. kuwapita watu kwenye foleni bila kuomba ridhaa yaooo
2. Wengine kukaguliwa tiketi/vitambulisho na wengine hapanaa

enjoy your life, usilalamike mnooo
 
Mbantu akienda jehanam atakua anaonewa maana maisha ya jehanam ameyaanza hapa duniani. Unabaguliwa nchini mwako, barani mwako, ukienda Ulaya na Asia unabaguliwa.

Madam ubaguzi mbaya sana,walinikatalia kuniuzia chakula visiwani kisa mwezi mtukufu!.lakini wazungu wanakula na kunywa mbaya zaidi walikuwa wakicheka wakati nacomplain kwa Meneja!

Unajiona kama sio binadamu hivi kwa muda [emoji26].
 
Mleta mada Kuna kitu hukiekewi hapo

Kutakuwa na mzigo au ulikuwa unaingia au unatoka wa madawa ya kulevya au madini yalikuwa yakiondoka

Upigaji umesharudi

Hizo CCTV camera waweza kuwa walilizizima hiyo deal ilipofanyika au walizielekeza angle ingine

Mtandao wote hapo airport waweza kuwa walikuwa wakijua hilo deal na kulifanyika timing Nani aingie Kwanza afuatiwe na nani Wanapeana ishara ingia

Mfano wa Kwanza aweza kuwa mbeba mzigo,wa pili bosi wake wa tatu tajiri mwenyewe wa kuhakiki Kila kitu sawa.
 
Safari za Dodoma airport inayotumika ni terminal two na siyo terminal three, terminal three ndio international route.

Mimi last wiki nimeingia ikulu ya Dar nikawa nahitaji bahasha kubwa ya A4! Nikatoka kwenda nje mpaka wizara ya ardhi nikanunuwa bahasha na nikarudi ikulu sikukaguliwa.

Usidhani mifumo ya ulinzi ipo unavyodhani wewe na akili zenu mbovu za kishamba za kisukuma.

Andika kwenye diary yako kwa kumbukumbu hii nchi kamwe haitokabidhiwa tena kwa washamba, kuna jamii bado haijastaarabika iendelee kuswaga ng'ombe na siyo binadamu.
 
Huelewi mzigo hapo waweza ingizwa au shushwa terminal yeyote movement ku u move ndani kwa ndani ukafanywa na wale wafanyakazi wa ndani ya uwanja madereva wa mabasi,mafuta, vile vigari vya kubeba masanduku kupeleka au kutoa kwenye ndege au gari zile zinabeba ngazi ya kupanda na kushuka kwenye ndege nk au akabeba mfanyakazi tu ndani ya uwanja kuupeleka terminal nyingine yeye au kukabidhi mwenzie wa terminal nyingine

Hujui kitu
 
Madam ubaguzi mbaya sana,walinikatalia kuniuzia chakula visiwani kisa mwezi mtukufu!.lakini wazungu wanakula na kunywa mbaya zaidi walikuwa wakicheka wakati nacomplain kwa Meneja!!
Unajiona kama sio binadamu hivi kwa muda [emoji26].
Sehemu kama hizo unatakiwa kuwaanika kwenye mtandao ya jamii kama facebook watakuomba poo wenyewe. Nenda group la Zanzibar Resident facebook.

Ni sehemu gani hiyo mkuu.?
 
Back
Top Bottom