Leo tarehe 4Oktoba, 2021saa 11.15 Asubuhi nilisindikiza mtu Uwanjani anaenda Dodoma na Air Tanzania ya saa 12 Asubuhi. Watu walikuwa kwenye foleni ya kuingia, kuna Muhindi mmoja alivaa pensi na fulana nyekundu, mwenzie alisha ingia yeye ni msindikizaji, nadhani kuna kitu alisahau kumwambia, alichofanya yule Muhindi ni kupita watu kwenye foleni hadi ndani bila mlinzi kumuuliza chochote wala kumkagua na hakuwa na tiketi, kilichoniuma zaidi mwenzie aliyekuwa naye huku nje alipoona jamaa anachelewa nae akaingia kumfuata na mlinzi akmuachia nae aingie. Sasa nikajiuliza hivi magaidi au wanaoweza leta madhara pale Airport ni weusi tu?., sikuvumilia nilimuuliza yule mlinzi, mbona hawa wahindi unawaachia waingie na kutoka bila kukaguliwa? akajibu hiyo ni kazi yake. Ikiwa na maana anaamua yeye aingie nani asiingie nani. Wenye Mamlaka fuatilieni kwenye CCTV mtaona.