Uchaguzi 2020 Ubaguzi wa kiitikadi haukubaliki

Uchaguzi 2020 Ubaguzi wa kiitikadi haukubaliki

kirengased

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2016
Posts
6,348
Reaction score
7,058
Salaam,

Wandugu, binafsi nimesikitishwa sana kwa kauli za kibaguzi zilizotolewa na mgombea mmoja wakati akimnadi Diwani wa chama chake asiyekubaliwa na wananchi.

Kwa kauli yake mgombea huyo wa Rais alitisha wananchi kwa kuwaambia wasipompa Diwani huyo ushindi wasimuulize yeye kuhusu maendeleo.

Isivyoeleweka Mgombea Urais huyo amekuwa akisema maendeleo hayana chama lakini anatoa mfano wa jinsi walivyoistopisha barabara ya lami kusudi isiingie eneo linaloongozwa na Wapinzani.

Unaposema hadharani huwezi kufanya kazi na Wapinzani maana yake una ubaguzi wa kiitikadi.

Pamoja na maendeleo tunayotafuta lazima tujue umoja wetu, haki na kuheshimiana ndiyo nguzo kuu za amani na utangamano.

Ni aibu kwa kiongozi mkubwa kutoa kauli za kivitisho ili kulazimisha yeye ama chama chake kuchaguliwa!

Ni muhimu tukakemea vitendo hivi visivyotuunganisha na kuuinua utaifa wetu na uzalendo Wetu.
 
Hizo ni kauli za ki siasa kwani mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro si alikua Mpinzani. Mbona Kuna mbaka manaibu waziri na nafasi nyingine mbalimbali serikalini wakitokea upinzani?
 
Sio saw kabisa ukianzia hapo kwenye ubaguzi wa kiitikadi ni wazi kwamba hutaishia hapo it is possibly ukaenda hadi kwenye masuala ya kidini as far as umejitanabaisha kwamba ww ni mbaguzi ikiwa unambagua Wananchi kwasababu ya imani yao ya kisiasa vipi wale wasioamin kuhusu dini yako itafikia hatua tutaamini wale Mashekh wa Zenji hadi leo wapo ndani kwasababu labda wao sio wa dini ya Mtukfu.

A president should be a symbol or unit he/ she should unite all people as one regardless their political, ethnic, regional, tribal or religious differences.
 
kirengased,

2B9AD329-1A7A-4426-A0F6-D537001FCA3A.jpeg
 
Izo ni kauli za ki siasa kwani mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro si alikua Mpinzani. Mbona Kuna mbaka manaibu waziri na nafasi nyingine mbalimbali serikalini wakitokea upinzani?
Na wakiteuliwa bado wanabaki kuwa Wapinzani?
 
Na wakiteuliwa bado wanabaki kuwa Wapinzani?
Tumia akili kidogo, utakua vipi ndani ya serikali ya Chama A ukatekeleza sera za Chama B. Kinachotakiwa ni mchango wako katika maendeleo ya Taifa bila kujali Chama ulichokua kwakua vyama vinapita Ila Taifa lipo tu.
 
Izo ni kauli za ki siasa kwani mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro si alikua Mpinzani. Mbona Kuna mbaka manaibu waziri na nafasi nyingine mbalimbali serikalini wakitokea upinzani?
Usiseme za kisiasa. Angalia anaezitoa ni nani. Rais wa nchi. Halafu baadae anakuja kusema maendeleo hayana vyama.
 
Ni kauli mbovu kutolewa na mtu ambaye kwa kumujibu wa katiba yetu bado pia ana act kama Rais.
 
Hizo ni kauli za ki siasa kwani mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro si alikua Mpinzani. Mbona Kuna mbaka manaibu waziri na nafasi nyingine mbalimbali serikalini wakitokea upinzani?
Magufuli ni mkabila mkubwa na ni hatari kwa mshikamano wetu.
 
Salaam,

Wandugu, binafsi nimesikitishwa sana kwa kauli za kibaguzi zilizotolewa na mgombea mmoja wakati akimnadi Diwani wa chama chake asiyekubaliwa na wananchi.

Kwa kauli yake mgombea huyo wa Rais alitisha wananchi kwa kuwaambia wasipompa Diwani huyo ushindi wasimuulize yeye kuhusu maendeleo.

Isivyoeleweka Mgombea Urais huyo amekuwa akisema maendeleo hayana chama lakini anatoa mfano wa jinsi walivyoistopisha barabara ya lami kusudi isiingie eneo linaloongozwa na Wapinzani.

Unaposema hadharani huwezi kufanya kazi na Wapinzani maana yake una ubaguzi wa kiitikadi.

Pamoja na maendeleo tunayotafuta lazima tujue umoja wetu, haki na kuheshimiana ndiyo nguzo kuu za amani na utangamano.

Ni aibu kwa kiongozi mkubwa kutoa kauli za kivitisho ili kulazimisha yeye ama chama chake kuchaguliwa!

Ni muhimu tukakemea vitendo hivi visivyotuunganisha na kuuinua utaifa wetu na uzalendo Wetu.
Watu wataelewana tu huku mtaani kwa hizi chuki zinazoendelea kujengwa na waheshimiwa.
Siitofautishi hii hali na mtu anaekuchomea moto shamba lako kosha akupa msaada wa kilo mbili za dona na maharage pasipo chumvi mkaa nk.
 
Magu ni mkabila mkubwa na ni hatari kwa mshikamano wetu.
La ukabila sasa linatetewa kwa nguvu zote... ukizikumbuka kauli "rais hawezi kutoka kaskazini... huyu sio mwenzotu na sasa kabila kubwa haliwezi tawaliwa na makabila madogo!!"
Kuna mahala tumefika na huenda ndio jahazi linazama sasa la si hivyo basi tunaelekea wakenya walikotoka.
 
Back
Top Bottom