kirengased
JF-Expert Member
- Jan 10, 2016
- 6,348
- 7,058
Salaam,
Wandugu, binafsi nimesikitishwa sana kwa kauli za kibaguzi zilizotolewa na mgombea mmoja wakati akimnadi Diwani wa chama chake asiyekubaliwa na wananchi.
Kwa kauli yake mgombea huyo wa Rais alitisha wananchi kwa kuwaambia wasipompa Diwani huyo ushindi wasimuulize yeye kuhusu maendeleo.
Isivyoeleweka Mgombea Urais huyo amekuwa akisema maendeleo hayana chama lakini anatoa mfano wa jinsi walivyoistopisha barabara ya lami kusudi isiingie eneo linaloongozwa na Wapinzani.
Unaposema hadharani huwezi kufanya kazi na Wapinzani maana yake una ubaguzi wa kiitikadi.
Pamoja na maendeleo tunayotafuta lazima tujue umoja wetu, haki na kuheshimiana ndiyo nguzo kuu za amani na utangamano.
Ni aibu kwa kiongozi mkubwa kutoa kauli za kivitisho ili kulazimisha yeye ama chama chake kuchaguliwa!
Ni muhimu tukakemea vitendo hivi visivyotuunganisha na kuuinua utaifa wetu na uzalendo Wetu.