Hapa sijamuelewa Rais wangu kabisa! kusema Wananchi wa NANGURUKU, wamekosa STENDI kwa sababu tu wamekosea kuchagua MBUNGE, yaani kama wangemchagua MBUNGE kutoka CCM wangepata STENDI, kwa kuwa wanemchagua kutoka UPINZANI hawawezi kupata STENDI kutokana na yeye bali MBUNGE wao.
Najiuliza, STENDI inayojengwa MBEZI DAR ES SALAAM, anayeijenga ni MBUNGE wa KIBAMBA, au Serikali ya MAGUFULI? STENDI ya Nanenane MBEYA! ilijengwa na Mbunge huyu SUGU? STENDI inayojengwa ARUSHA, muhusika ni GODBLESS LEMA, au Serikali ya MAGUFULI?
HII dhana ya Maendeleo hayana CHAMA imeshakufa? na Je! MAGUFULI ana uhakika gani hao wanaomuomba kama walimchagua BWEGE? JE! NANGURUKU hakuna wanachama wa CCM?
Mbona UBUNGO inajengwa FLY OVER, na Mbunge wake ni kutoka CHADEMA?
Credit: Abeid Suleiman