Ubaguzi wa kisiasa anaouonesha Magufuli hadi CCM wenyewe wanamshangaa

Ubaguzi wa kisiasa anaouonesha Magufuli hadi CCM wenyewe wanamshangaa

Sasa hivi ukiigusa CCM makachero wake watakuvamia kama unauza mifuko ya Nylon [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mkuu tindo hamchoki kunung'unika, kulalama, kushutumu, kulaumu, kujisheua na kulialia kutafuta huruma ya jamii ndani na nje?

Lini mtaanzisha mada za kukijenga chama chenu kwa hoja zinazogusa jamii kwa ujumla badala ya hizo mnazodhani zinawajenga viongozi wenu, kumbe zinawadidimiza kama siyo kuwabomoa?

Kuna lipi upinzani umelifanyia Taifa hili japo kidogo, ikizingatiwa wana madiwani, wabunge kadhaa na wanaongoza Halmashauri za majiji ya TANZANIA?
Ulikuwa unataka wawanunulie ndege na kuwajengea SGR? Mbona wewe ni mpumbavu kiasi hiki? Mbaya zaidi hujijui kuwa wewe ni mpuuzi
 
Kabla Nyerere hajawa rais wakati yuko Tanu akipamana na wakoloni, alijenga madaraja na barabara ngapi mpaka wananchi wakamuamini wakampa nchi? Mkapa na Kikwete kuna miundombinu walijenga wakiwa madarakani, je wamejenga barabara za urefu gani baada ya kutoka madarakani, ili tujue ukiwa nje ya madaraka unaweza kujenga kitu cha maana?

Baada ya vyanzo vingi vya halmashauri kuchukuliwa na serikali kuu, hakuna chochote cha maana halmashauri zinaeweza kufanya, zaidi ya kusubiri pesa serekali kuu, na hizo hela zikienda kwenye halmashauri, ndio hiyo inaitwa kasi ya serikali ya Magufuli. Hilli wala halihitaji Elimu ya chuo kikuu kulifahamu.

Hatushutumu bali tunaweka wazi ukweli. Kuna tofauti ya kulalamika, kunung'unika nk. Sisi tunasema wazi serikali hii ya awamu ya tano, ina viongozi wenye ulevi na matumizi mabaya ya madaraka.
Mkuu umemaliza. Kama hatakuelewa tena basi atakuwa na mtindio wa ubungo
 
Zimetoka nyingi ila wanaccm wameridhika na mgombea wao
Chadema walivyomchagua tena Mbowe mlisema chadema hakuna demokrasia mwenyekiti ni dikteta na hakuna wa kumpinga. Haya tuelezeni basi ninyi imekuwaje mkulu kajiprintia fomu yake mwenyewe na hakuna aliefungua mdomo kuhoji? Hiyo demokrasia mnayoihubiri iko wapi?
 
Kumbuka Mbowe amekuwa akigombea kwa miaka 25
Chadema walivyomchagua tena Mbowe mlisema chadema hakuna demokrasia mwenyekiti ni dikteta na hakuna wa kumpinga. Haya tuelezeni basi ninyi imekuwaje mkulu kajiprintia fomu yake mwenyewe na hakuna aliefungua mdomo kuhoji? Hiyo demokrasia mnayoihubiri iko wapi?
 
Ulikuwa unataka wawanunulie ndege na kuwajengea SGR? Mbona wewe ni mpumbavu kiasi hiki? Mbaya zaidi hujijui kuwa wewe ni mpuuzi

Naweza kuwa mpumbavu na mpuuzi kama unavyotaka iwe, lakini kumbuka nchi hii si ya CCM wala chama chochote cha siasa (Mbatia kuzindua kampeni Marangu TTC leo), ambavyo kimsingi huwajenga wanasiasa kuliko wanachama na Watanzania kwa ujumla

Mtanzania mwenye kujitambua, asiye mpumbavu na mpuuzi, kama mimi, lakini mwerevu kama wewe, Mkuu MKANDAHARI, maendeleo yanayogusa maisha yake ya msingi (elimu, afya, maji, nishati na miundombinu bora na imara) hataacha kumchagua kiongozi anayefanikisha hayo.

NIKUSAMEHE TU KWA KUTUMIA LUGHA AMBAYO HUTUMIWA NA MATEJA
 
Julai 18 kila mwaka ni Siku ya Kimataifa ya Nelson Mandela, na pia ni siku ya kuzaliwa kwa mwanasiasa huyo mkongwe wa Afrika Kusini, aliyepigania kuondoa aina zote za ubaguzi wa rangi na kuleta usawa kwenye nchi yake.

Mwaka huu ni wa 101 tangu kuzaliwa kwa Mandela. Wengi tunafahamu historia yake na jinsi alivyojitoa kuikomboa nchi yake kutoka kwenye ubaguzi wa rangi. Alifungwa jela katika gereza la Robbin Island kwa miaka 27 kutokana na harakati zake za kupigania usawa na kuondoa ubaguzi wa rangi. Mei 10 mwaka 1994, Mandela aliapishwa kuwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, na alidumu madarakani kwa awamu moja tu, kama alivyosema awali, na nafasi yake kuchukuliwa na Thabo Mbeki Juni mwaka 1999.

Mandela alitunukiwa tuzo ya amani ya Nobeli mwaka 1993, pamoja na rais wa zamani wa Afrika Kusini F.W. de Klerk, ambaye aliondoa zuio la chama cha ANC na kumuachia huru Nelson Mandela kutoka kifungoni. Kwa pamoja walishirikiana kuliondoa taifa hilo kutoka katika utawala wa kibaguzi na kuwa nchi ya kidemokrasia.

Hivi sasa dunia bado inakabiliwa na ubaguzi wa rangi, ukosefu wa usawa, na hata chuki dhidi ya raia wa kigeni bado zinaonekana nchini Afrika Kusini. Kutokana na mambo hayo, tunabaki kujiuliza, ni wapi tumekosea? Kwa nini mambo haya bado yanaendelea mpaka zama hizi?

Mwezi Mei nchini Marekani kuliibuka vurugu kubwa baada ya askari polisi mzungu kumkandamiza kwa goti Mmarekani mwenye asili ya Afrika George Floyd kwa zaidi ya dakika nane, na kusababisha kifo chake. Maandamano ya kudai haki kwa watu weusi nchini Marekani yamefanyika kuanzia wakati huo, na Nchi nyingine za Ulaya nazo kuunga mkono maandamano hayo.

Haya yote yanaonyesha kuwa bado jamii haijaamua kimsingi kuondokana na dhana ya ubaguzi wa rangi, bado kuna watu wanaojiona ni bora kuliko wengine, na wanastahili kupewa heshima kuliko wengine. Lakini binadamu wote ni sawa, haijalishi rangi ya ngozi yako.

Watunga sera wanapaswa kusimamia haki sawa kwa wote, bila kujali rangi, dini wala kabila. Elimu pia inapaswa kutolewa kwa wanafunzi kuanzia shule za msingi ili kuweka msingi imara utakaowajenga katika siku za baadaye, kuwa haijalishi rangi ya ngozi, watu wote ni sawa na wana haki sawa katika sekta zote.

Wakati tunapoadhimisha Siku ya Kimataifa ya Nelson Mandela, tunapaswa kusimamia kimsingi yale ambayo Madiba aliyasimamia na kupigania katika maisha yake, haki, usawa, kuondoa ubaguzi wa rangi, na kuishi kwa amani na watu wote.
 
Hapa sijamuelewa Rais wangu kabisa! kusema Wananchi wa NANGURUKU, wamekosa STENDI kwa sababu tu wamekosea kuchagua MBUNGE, yaani kama wangemchagua MBUNGE kutoka CCM wangepata STENDI, kwa kuwa wanemchagua kutoka UPINZANI hawawezi kupata STENDI kutokana na yeye bali MBUNGE wao.

Najiuliza, STENDI inayojengwa MBEZI DAR ES SALAAM, anayeijenga ni MBUNGE wa KIBAMBA, au Serikali ya MAGUFULI? STENDI ya Nanenane MBEYA! ilijengwa na Mbunge huyu SUGU? STENDI inayojengwa ARUSHA, muhusika ni GODBLESS LEMA, au Serikali ya MAGUFULI?

HII dhana ya Maendeleo hayana CHAMA imeshakufa? na Je! MAGUFULI ana uhakika gani hao wanaomuomba kama walimchagua BWEGE? JE! NANGURUKU hakuna wanachama wa CCM?

Mbona UBUNGO inajengwa FLY OVER, na Mbunge wake ni kutoka CHADEMA?

Credit: Abeid Suleiman
 
Back
Top Bottom