Ubaguzi wa kisiasa anaouonesha Magufuli hadi CCM wenyewe wanamshangaa

Ubaguzi wa kisiasa anaouonesha Magufuli hadi CCM wenyewe wanamshangaa

Umesikia na si ni walamba viatu kama Dr slaa kwa njaa xake.
Bora ungekuwa mlamba viatu! Hakuna hasara kubwa hapa duniani kama mtu kuwa ndegative.... you just end up dealing with the marginals maisha yako yote mpaka cku unaenda kaburini. Tatizo kubwa sasa ni kwamba negativity huwa inakuwa na pronounced effect kubwa zaidi kwa wasiokuwa negative, na inawa-affect zaidi wao kuliko mhusika mwenyewe. Nilishasema kuwa ukikuta mtu negative ana kitu positive, ujue kapora kwa nguvu au kwa njia zingine anazozijua yeye!
 
Inaonekana hujui unaloongea nadhani, nenda Sudan ukaangalie kama Elbashir naye hujafanya miradi ya maendeleo. Hivi unadhani unaweza ukawa kiongozi wa nchi na usitekeleze mradi wowote wa maendeleo? Kama miradi ya maendeleo ndio inaonyesha kujitokea, basi wazungu waliojenga reli, tena zaidi ya moja, ranchi, mashule, hospitali nk, hao walijitolea sana. Inaonekana hujui tofauti ya wajibu na kujitolea. Leo hii Mkapa, Kikwete au Mwinyi wakitekeleza mradi wa maendeleo ndio watakuwa wamejitolea maana hawako madarakani.

Nenda Ethiopia hapo, utawala uliopita umefanya miradi mikubwa ya maendeleo, wana shirika kubwa la ndege nk. Je utawala wao ulikuwa unawafanya nini wananchi wak? Kiongozi mpya wa Ethiopia alipoingia juzi madarakani si ndio karudisha uhuru wa wananchi wake.
Maendeleo yote tuyayaona South Africa yaliletwa na makaburu lakini akina Mandela nawenzake walikubali wafie jela kuliko kuwa chini ya utawala dhalimu wa makaburu.
 
Kwani hapa Tanzania tunatawaliwa na dikteta mpaka useme hamna uhuru? Hii nchi inatawaliwa kwa misingi ya Katiba na sheria za nchi. Kuleta maendeleo lazima kuendane na utawala wa sheria, ndio maana upo hapo unatoa maoni yako bila bugudha.
Kusema wakoloni walileta maendeleo hii pia inadhihirisha upofu wako wa kisiasa na kukariri upuuzi wa Tundu Lissu. Mkoloni alijenga reli na barabara ili ainyonye nchi yetu. Mapato yote yalienda kwao huko ulaya. Sasa hivi mapato yote yanabaki hapa Tanzania. Kwa hiyo acha kukariri siasa za kitoto.

Huwezi kuona tatizo maana ww ni mfaidika wa utawala huu, hivyo sitegemei maoni tofauti na haya toka kwako. Hilo la kusema utawala wa sheria, nilikuambia toka juzi uwepo wa sheria ni jambo moja, na utekelezaji ni jambo jingine. Na hakuna nchi isiyo na sheria, ila ni sheria za aina gani hapo ndio hoja ilipo. Maoni ninatoa, ila ninatolea wapi? Hivi unadhani kwenye nchi zenye udictator watu hawatoi maoni yao? Wanatoa sana, ila usalama wao ni jambo jingine.

Hao wakoloni walitumia mapato kujenga hiyo miradi, sio kwamba walitoa kwenye mishahara yao. Kama wazungu walijenga reli, viwanja vya ndege, mashule nk, bado hata wao walitumia mapato kujenga miradi. Hao wazungu unaolia waliondoka miaka 60 iliyopita, mbona bado sisi ni masikini?
 
Sitaki niandike mistari mingi kama ulivyotiririka.
Jibu swali moja tu. Hao wakoloni walipoondoka hapa Tz mwaka 1961 waliacha barabara ngapi za rami ambazo ni barababara kuu?
 
Sitaki niandike mistari mingi kama ulivyotiririka.
Hao wakoloni walipoondoka hapa Tz mwaka 1961 waliacha barabara ngapi za rami ambazo ni barababara kuu? Hao wakoloni hayo mapato waliyotumia kujenga hizo reli ilikuwa ni kwa manufaa ya Watanzania? Hao wakoloni walipoondoka hapa Tanzania waliacha shule ngapi za sekondari? Waliacha hospitl ngapi mkoa na wilaya? tindo
 
Team Mwenyekiti kwa sasa meno yote 32 nje...kasheshe ni kwa hawa wenzangu mie ni shughuli pevu kupenyapo.
 
Sitaki niandike mistari mingi kama ulivyotiririka.
Jibu swali moja tu. Hao wakoloni walipoondoka hapa Tz mwaka 1961 waliacha barabara ngapi za rami ambazo ni barababara kuu?

Kwa taarifa yako, watu watakaokuwepo mwaka 2070 watajiuliza Magufuli aliacha barabara ngapi za lami, na madaraja kiasi gani. Maana wakati huo yatakuwa mengi kuliko sasa. Nadhani swali lako majibu yake yako humo.
 
Kama yameachwa na mtanzania tena mzalendo haina tabu. Nashangaa wewe kusifia reli iliyojengwa na mkoloni aliyekuwa anatunyonya kwa kila namna.
 
Kwani kawe alumni ,bia yetu ,Ussr wanasemaje

Sasa si afute hivi vyama vingine ili tuwe wakomunisti

Maana inaonekana havina maana

Futeni vyama vyote vya upinzani tuanze moja mbaki CCM tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimesikia shangwe alizopata Prof Jay...Jamaa walitamani wampore MIC ila ndiyo hivyo tena.WanaKilosa wapo Baaado Muacheni aendelee kutuwakilisha.Kuna watu wanakera tuu,sasa Lijualikali alikuwa hana hata cha kuongea yupo yupo tuu
Nimeangalia kipande cha video sehemu anayoongea Mh. Joseph Haule,kwa kweli nimepata uhakika kuwa Watanzania wengi wanajua nani ni kiongozi wao wa kweli na mtetezi wao hasa. Kushangiliwa kule kuna maana kubwa sana,kwamba upinzani unaaminiwa na Watanzania,na kwamba kukiwa na tume huru,uchaguzi huru na wa haki,hakika CCM itakuwa kwaheri.
Keep it up the good work upinzani na Mungu Mwenyezi awatangulie.
 
Tumekua tukisikia kwamba mkuu wa nchi ni mbaguzi hasa linapokuja swala la mitazamo ya kisiasa, kitu ambacho si kuzuri na hakifai kwa mkuu wa nchi.

Tofauti na viongozi wengine, hata marais waliopita, Mheshimiwa hapa amefeli na inaonyesha anafanya makusudi.

Jana akiwa Msoga, diwani wa hilo eneo aliitwa atoe kero. Mh akadhani ni diwani toka chama cha Chadema kwa sababu hakuvaa sare ya CCM, akaamuru anyang'anywe mic na maneno makali juu lakini baada ya kuuliza chama gani akaambiwa ni wa CCM, mara moja akaamuru arudishiwe mic na aendelee kuongea.

Leo tarehe 29 June 2020 akiwa Kilosa akaanza kumponda mbunge wa eneo na kusema wananchi wa eneo hilo wanachagua kwa jazba akiamini mbunge wa eneo hilo ni wa Chadema. Anaongeza kwa kusema yeye angekua mbunge wa eneo hilo angekua amemaliza changamoto zote ila kwa sababu wananchi wanachagua kwa jazba na wanachagua wabunge sio, ndio maana bado changamoto zipo.

Baadaye akauliza mbunge wa hapo anaitwa nani na wa chama gani? Wananchi wakamtaja na kumwambia anatoka chama chamapinduzi. Bila hata aibu akaanza kumsifia na kuahidi kuzimaliza changamoto hizo akisadiwa na waziri husika.

Wananchi wa Tanzania sio watoto wanajua na wanaelewa vizuri, wao wanapendana bola kujali vyama, dini wala kabila lakini bado kuna viongozi karne hii wanasimamia ubaguzi.

Naamini mh Rais ana nia njema na Tanzania, lakini bado ana nafasi ya kuondoa hurka hii ya ubaguzi hata kama chadema walimpa wakati mgumu 2015.

Rais ndio kiungo pekee cha kuwaunganisha Watanzania.

Sio sababu ya yeye kuendelea kubagua vyama vya upinzani hali kazi zake alizo zifanya zinaonekana.

Haya mambo madogodogo yanamuondolea kitu fulani kama kiongozi.

Tuungane kuupinga ubaguzi. Na asilazimishe vyama vya upinzania kupata ajenda.

View attachment 1493226

Prof Jay
View attachment 1493227
Hili lilituumiza sana watu wa Kimara,Mbezi,Kibamba kwa kuvunjiwa nyumba zetu bilabila kisa tu,,,tulichagua CHADEMA kuwa wabunge wa Jimbo la Kibamba na Ubungo. Maumivu na Mateso yetu hayatosahaulika kwa vizazi vyetu vyote hadi utimilifu wa dahari!
 
Acha chuki na hasira. Hata treni ya Sgr utaipanda wewe na jamaa zako. Mbona mlikodi Bombardier kwenda na kurudi mpaka Mwanza.

Hata treni ya Mkoloni tunapanda mpaka leo. Kumbe tulikodi Bombardier, nilidhani ni bure. Kwa taarifa yako, hata precision air na fast jet kabla ya figisu tulizipanda sana.
 
Amewahi sema jimbo la upinzani hapeleki fedha.

Jimbo la tundu lissu hakupeleka chochote hadi walipo mfuta lissu ubunge.
Hili lilituumiza sana watu wa Kimara,Mbezi,Kibamba kwa kuvunjiwa nyumba zetu bilabila kisa tu,,,tulichagua CHADEMA kuwa wabunge wa Jimbo la Kibamba na Ubungo. Maumivu na Mateso yetu hayatosahaulika kwa vizazi vyetu vyote hadi utimilifu wa dahari!
 
IMG_20200624_174951.jpg

Ndio moods mkerejetwa wa kijani Sasa hii picha au katuni nikiyoposti ina shida gani hebu nielimishe nijue ,umekazana kublock hivi Mimi au mtu mwingine yoyote tunaweza kufanana mawazo na yako unavyotaka niandike au nifanane na wewe.
 
Back
Top Bottom