Jiwe gizani, hebu chimbua kidogo bwashee!
Ngoja nielezee kidogo..
1. warombo shida yetu kubwa japo siku hizi imepungia sana ni matambiko. Yaan kwa mizimu tuu? Halooo.. acha kabisa. Sema imepungua kiasi kikubwa. Na wakibosho bado wameshikilia mila hata some parts za kibosho. Pia ushamba bado upo upo kwa warombo. Huwa ni wapole ila wana gubuu. Ubabe nadhani ni kama asili na confidence ambayo tayari sisi wanawake wa kichagga ilishajijenga toka enzi. Warombo ni mabuldoza. Wanafanya kazi aisee. Wanawake wa kirombo wanapiga kazi si mchezo. Kama kuna wanawake wanafanya kazi uchaggan basu warombo.
2. Wamarangu.. hata uniue sitokaa wala kutamani olewa na wamarangu. Yaani kati ya sisi wachagga, hakuna sub tribe wana tabia za ajabu kama wamarangu. Wamejaa nyodo, dharau, wanajisikia, uchonganishi etc. Yaan naona kama wamachame wanapakaziwa. Yaan wanawake wao [emoji119][emoji119]
Wana wivu balaa. Roho za wivuuu. Ni wavivuu[emoji23] huwa wanapenda kujibrag sana. Na vile wamejaliwa karangi basi ndo wanajikuta ilee keki yani. Hela yenyewe hawana. Halaf ni opportunists balaa. Ila wanajipendaa. Wanapendeza haswaa. Hawa wanaelewana na wamachame kwa kias fulan maana kishule wao walienda enda wa mwanzo unlike uchaggani kungine.
3. Wakibosho.
Ile clip ya USIMLETE ni wakibosho wale. [emoji23][emoji23] sitataja wanakoishi. Katika sisi wachagga, uuuwui, hakuna wachagga wakorofi kama wakibosho. Siyo wanaume si wanawake. Yaani mwanamke akikuambia "Macha nataka saa ya rollex" basi ukaitafute ulete. Kama utaiba haya, maana wakibosho kwa ujambazi[emoji23][emoji23][emoji119][emoji119] yaan hela yao inatafutwa kibabe.
Enzi hizo walikua wanaruka na magodoro magorofani Arusha. Yaan hawa ndo wazee wa show. Na hata bifu lao na wamachame ni kutokana na Historia. Hawapatani. Hata nyumba haziangalii upande mmoja. Na hili ni kwenye jamii za uchaggani lipo sana. Yaani kina koo na koo hazioani kwahiyo lisiwashangaze sana. Ila wakibosho na warombo wanaelewana maana asilimia kubwa ni wafanyabiashara. Hata mahotel mengi makubwa utakuta yanamilikiwa na wakibosho. Akakuambia ngikupa kiandu kimbia ufeee. Hawanaga mzahaaa.
4. Wamachame.
Honestly nawapenda sana wamachame[emoji23][emoji23] na kuna muda kbs nadanganya ndo kwetu. Wamachame hasa wanaume huwa ni wastaarabu mno. Mno mno. Wanawake wao wana ubabe. Hiwa si washari ila mpaka uwachokoze. Na wana balaa zitoo ukiwaingilia. Na majority kama sikosei ni magiant sana. Wana miili. Kiboko ya wamachame huwa ni wakibosho[emoji23][emoji23] yaan waliwachinja kweli enzi za kina Mangi Sina. Kiukweli waliopaswa utwa wapalestina ni wakibosho.
Sema MASAMA alipotaja Gilberty akidhania babake ndo angemkubalia kwmaba si sehem ya Machame ndipo alipoharibu kabisa. Masama kwa Mullah camp pale sasa ndo kuna Uislam haswaa. Yaan ule Uislam wenyewe. Machame kuna Ulutheri na Uislam tuu. Yaani pale Masama ndo wale walioanza kuvaa Pedo wale. Wale wanaoruka wanageuka hewani[emoji23][emoji23] ukitaka balaa na fujo nenda mitaa ya Masama.
5. Old Moshi.
Huku huwaga wamejaa wasomi. Halafu hawanaga muda na mtu. Kwa kina mama Anna Mkapa huko. Ila ndo kuna Uru kishumundu vile eh?[emoji23][emoji23] hawa huwaga wako kivyao ila ndo wabishi balaa. Wanawake wao hawatakagi ujinga.
All in all, wanawake wa Machame ni wazuri sana na wana upendo sana. Wanajua kupambana. Kuachana siwezi sema mwanamke ndo sababu ama lah kwani hata mwanaume anaweza pia kua chanzo. Binafsi enzi za shule nilikua napenda kuitwa mmachame ili tuu nisiletewe mazoea[emoji23][emoji23]
"All in all" (in baba levo's voice)
Karibuni sana Rombo kuoa achaneni na baba Gilberty. Wao wakibosho wana mabifu na wamachame tuwaelewe.
Na Gilberty alijua kabisa hapa kuna shida ndo maana alikua hataji mchumbake nani wakati wenzake wanataja baba akafatilia kwa unakini intelijensia yale mpaka kufikia USIMLETE..