Ubaguzi wa polisi dhidi ya Waafrika nchini Marekani haujabadilika

Ubaguzi wa polisi dhidi ya Waafrika nchini Marekani haujabadilika

Yoyo Zhou

Senior Member
Joined
Jun 16, 2020
Posts
199
Reaction score
322
mmexport1748482727341.jpg
Tarehe 25 Mei inatimia miaka mitano tangu Mmarekani mwenye asili ya Afrika George Floyd auawe na polisi kwa kukabwa na goti.

Tukio hili lilisababisha maandamano makubwa kote Marekani na hata katika nchi nyingine duniani. Hata hivyo, sasa miaka mitano imepita, ubaguzi wa polisi dhidi ya Waafrika nchini Marekani haujabadilika hata kidogo.


Maelfu ya watu nchini Marekani siku hiyo waliandamana ili kumkumbuka Floyd, na kulaani utawala wa Trump kwa kupindua mageuzi ya polisi na hatua za kuhimiza usawa wa rangi.


Katika miaka mitano iliyopita, mashirikisho ya Wamarekani wenye asili ya Afrika, makundi ya haki za kiraia, maafisa wa majimbo na kaunti, na hata maafisa wa serikali kuu nchini Marekani wameendelea kutoa wito wa kutokomeza ubaguzi wa rangi na matumizi mabaya ya nguvu ya polisi. Hata hivyo, ikilinganishwa na miaka mitano iliyopita, hakujawa na mabadiliko makubwa katika suala la ubaguzi wa rangi au vitendo vya kinguvu kupita kiasi vya polisi, na matukio ya polisi kuwauwa Waafrika pia hayajapungua.


Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na tovuti ya Ramani ya Umabavu wa Polisi nchini Marekani, mwaka 2020, idadi ya watu waliouawa na polisi nchini Marekani ilikuwa 1,160, na kufikia mwaka 2024, idadi hiyo iliongezeka hadi 1,260. Wamarekani wenye asili ya Afrika bado ndio kundi linalokabiliwa zaidi na dhuluma za polisi.


Wamarekani wenye asili ya Afrika wanachukua asilimia 12 ya watu wote nchini Marekani, lakini mwaka 2020, Wamarekani wenye asili ya Afrika walifikia asilimia 25 ya Wamarekani wote waliouawa na polisi, na mwaka 2024, kiwango hiki bado kilikuwa takriban asilimia 25.


Kwa maoni ya Wamarekani wenye asili ya Afrika nchini Marekani, ubaguzi wa rangi dhidi yao bado ni mbaya sana.


Kulingana na matokeo ya kura za maoni zilizotolewa hivi karibuni na Shirika la Pew, asilimia 67 ya Wamarekani wenye asili ya Afrika wana mashaka kuhusu iwapo Marekani inaweza kutimiza usawa wa rangi. Wakati huo huo, asilimia 72 ya watu wanaona kwamba ufuatiliaji wa usawa wa rangi haujaleta mabadiliko halisi kwa Wamarekani wenye asili ya Afrika nchini Marekani.



Miaka mitano ni muda wa kutosha kwa mtoto mchanga kukua na kuwa mtoto aliyeelimika shuleni, lakini hautoshi kwa Marekani, ambayo ni nchi yenye nguvu kubwa zaidi duniani, kujifunza maadili ya msingi ya haki na usawa.


Wakati watu wanakusanyika katika mitaa ya Minneapolis mwaka baada ya mwaka, hawamuombolezi Floyd pekee, bali pia wanashtaki ubaguzi wa rangi ambao hauwezi kutokomezwa daima nchini Marekani.
 
Zamani nilikuwa naona wamarekani weusi wanaonewa sana na police

Lakini ukikaa katika jicho la haki na kisheria

Wamarekani weusi wengi sana ni wavunjifu wa sheria tena kwa kiwango cha juu sana

Kuna jamaa mmoja JF husema

I see mediocrity when i see nigga all over the world

Wamarekani weusi wengi ni wajinga sana
 
Kifo cha Yule mwamba kiliniuma Sana...Toka hiyo siku sikuipenda nchi ya Marekani.
Na mpaka Jamaa anafariki hata sikuamini asee....
Ngoja niende tweeter nikuone tena kifo kile.
 
Angekuwa mwarabu yule Polisi walokole wangejaa kwenye Uzi kuwalaumu kwa Ubaguzi wao na meneno yote yangewatoka
Sasa

tatizo Mzungu na Mzungu walishapigwaga changa kuwa anafanana na Mungu wao !!!!!

Wapo tayali wamtupie lawama mweusi mwenzetu !!!
ili tu MZUNGU abaki Salama

Awa
ndio Kondooo waliopotea tangu na tangu ,,
 
View attachment 3349314Tarehe 25 Mei inatimia miaka mitano tangu Mmarekani mwenye asili ya Afrika George Floyd auawe na polisi kwa kukabwa na goti. Tukio hili lilisababisha maandamano makubwa kote Marekani na hata katika nchi nyingine duniani. Hata hivyo, sasa miaka mitano imepita, ubaguzi wa polisi dhidi ya Waafrika nchini Marekani haujabadilika hata kidogo.
Maelfu ya watu nchini Marekani siku hiyo waliandamana ili kumkumbuka Floyd, na kulaani utawala wa Trump kwa kupindua mageuzi ya polisi na hatua za kuhimiza usawa wa rangi.
Katika miaka mitano iliyopita, mashirikisho ya Wamarekani wenye asili ya Afrika, makundi ya haki za kiraia, maafisa wa majimbo na kaunti, na hata maafisa wa serikali kuu nchini Marekani wameendelea kutoa wito wa kutokomeza ubaguzi wa rangi na matumizi mabaya ya nguvu ya polisi. Hata hivyo, ikilinganishwa na miaka mitano iliyopita, hakujawa na mabadiliko makubwa katika suala la ubaguzi wa rangi au vitendo vya kinguvu kupita kiasi vya polisi, na matukio ya polisi kuwauwa Waafrika pia hayajapungua. Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na tovuti ya Ramani ya Umabavu wa Polisi nchini Marekani, mwaka 2020, idadi ya watu waliouawa na polisi nchini Marekani ilikuwa 1,160, na kufikia mwaka 2024, idadi hiyo iliongezeka hadi 1,260. Wamarekani wenye asili ya Afrika bado ndio kundi linalokabiliwa zaidi na dhuluma za polisi. Wamarekani wenye asili ya Afrika wanachukua asilimia 12 ya watu wote nchini Marekani, lakini mwaka 2020, Wamarekani wenye asili ya Afrika walifikia asilimia 25 ya Wamarekani wote waliouawa na polisi, na mwaka 2024, kiwango hiki bado kilikuwa takriban asilimia 25.
Kwa maoni ya Wamarekani wenye asili ya Afrika nchini Marekani, ubaguzi wa rangi dhidi yao bado ni mbaya sana. Kulingana na matokeo ya kura za maoni zilizotolewa hivi karibuni na Shirika la Pew, asilimia 67 ya Wamarekani wenye asili ya Afrika wana mashaka kuhusu iwapo Marekani inaweza kutimiza usawa wa rangi. Wakati huo huo, asilimia 72 ya watu wanaona kwamba ufuatiliaji wa usawa wa rangi haujaleta mabadiliko halisi kwa Wamarekani wenye asili ya Afrika nchini Marekani.
Miaka mitano ni muda wa kutosha kwa mtoto mchanga kukua na kuwa mtoto aliyeelimika shuleni, lakini hautoshi kwa Marekani, ambayo ni nchi yenye nguvu kubwa zaidi duniani, kujifunza maadili ya msingi ya haki na usawa. Wakati watu wanakusanyika katika mitaa ya Minneapolis mwaka baada ya mwaka, hawamuombolezi Floyd pekee, bali pia wanashtaki ubaguzi wa rangi ambao hauwezi kutokomezwa daima nchini Marekani.
Hao maniga nao wana tabia za hovyo hivi walitokea nchi zipi.
 
Zamani nilikuwa naona wamarekani weusi wanaonewa sana na police

Lakini ukikaa katika jicho la haki na kisheria

Wamarekani weusi wengi sana ni wavunjifu wa sheria tena kwa kiwango cha juu sana

Kuna jamaa mmoja JF husema

I see mediocrity when i see nigga all over the world

Wamarekani weusi wengi ni wajinga sana
Ni km wakenya, hakuna mijitu inajiona inajua lakini ya hovyo km wakenya ndivyo maniga yalivyo
 
Kifo cha Yule mwamba kiliniuma Sana...Toka hiyo siku sikuipenda nchi ya Marekani.
Na mpaka Jamaa anafariki hata sikuamini asee....
Ngoja niende tweeter nikuone tena kifo kile.
Polisi wa Marekani hacheki na kima siyo hawa wa kwetu na bado mnawapigia kelele
 
Zamani nilikuwa naona wamarekani weusi wanaonewa sana na police

Lakini ukikaa katika jicho la haki na kisheria

Wamarekani weusi wengi sana ni wavunjifu wa sheria tena kwa kiwango cha juu sana

Kuna jamaa mmoja JF husema

I see mediocrity when i see nigga all over the world

Wamarekani weusi wengi ni wajinga sana
Kuna ukweli kwenye hili, kila nikifuatilia hawa wanaouawa na polisi sikuti kwenye CV zao kama walikuwa walimu , wahasibu au wafanyakazi viwandani; bali utasomewa kitini cha matatizo lukuki ya kisheria
Hiyo Floyd mwenyewe aliwahi kumshikia mwanamke mwenye mimba bunduki na ana kesi nyingine za ukibaka lukuki, zaidi ya hapo wamarekani weusi waliamua kuandamana kwa mtu ambaye kusema kweli ukisoma historia yake unaweza kusema mwisho wake ilikua Kifo kwa mikono ya polsi
Yaani hamnaga mtu hao watu weusi wamewahi kumtetea akawa hana makando kando yake kwenye maisha yake
 
Hata huku Africa tunauana Sana, swali kwanini waafrika tuko hivyo, rejea mdude na kibao ni laana au nini
Mzungu aliposema mwafrika (mtu mweusi) hawezi kujitawala hakukosea. Wewe angalia nchi zote zenye watu weusi, hata zilizopo mabara mengine unakuta zina matatizo. eg Haiti. Halafu ukija Afrika, zile nchi zenye wazungu kama Afrika Kusini zina maendeleo. Hii ni ajali? Hapana. Mbaya zaidi ni kuwa huwa hatutaki kukubali kuwa tuna matatizo jambo ambalo ni baya sana kwenye kuleta mabadiliko. Ukitaka kuondoa tatizo lolote ni lazima ukiri kwanza una tatizo.
 
Zamani nilikuwa naona wamarekani weusi wanaonewa sana na police

Lakini ukikaa katika jicho la haki na kisheria

Wamarekani weusi wengi sana ni wavunjifu wa sheria tena kwa kiwango cha juu sana

Kuna jamaa mmoja JF husema

I see mediocrity when i see nigga all over the world

Wamarekani weusi wengi ni wajinga sana
Dudubaya kasema hilo, kiujumla jitu jeusi ni takataka.
Kuna mpopo aliletwa nimfundishe kazi, week 1 tu kaanza yeye kunifundisha tena kazi.
Aliondokea mlango alioingia nao kimya kimya.
 
Dudubaya kasema hilo, kiujumla jitu jeusi ni takataka.
Kuna mpopo aliletwa nimfundishe kazi, week 1 tu kaanza yeye kunifundisha tena kazi.
Aliondokea mlango alioingia nao kimya kimya.
Hapo wewe una rangi gani mwenzetu?

Maana si kwa misemo hiyo kuhusu weusi
 
Ukiangalia tu movie na music wao utajua wale ndugu zetu ni watu wa aina gani.
Background za vijana wengi weusi wengi zinahusika na uhalifu uhalifu kukaa jela nk.

Inaonekana sisi watu weusi bado tuna kiwewe sana cha ukoloni na bado excuse yetu kubwa ni ukoloni.

Natafuta nchi moja inayokaliwa naweusi tupu halafu iwe na maendeleo makubwa.
SA pale tunaona yanayoendelea hata baada ya nchi kujengwa na kaburu lakini weusi ndio wanaiharibu sasa.

Watu weusi duniani kote tunahitaji kujitafakari sana tukitaka kujenga heshima.
 
Back
Top Bottom