Ubaguzi wa rangi(racism) dhidi ya mtu mweusi upo na hautakaa uishe duniani

Ubaguzi wa rangi(racism) dhidi ya mtu mweusi upo na hautakaa uishe duniani

lbaraka

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2014
Posts
393
Reaction score
248
Habari wakuu,
Napenda kuliongelea suala la ubaguzi wa rangi unaopigiwa kelele kwa sasa duniani. Kwanza kabisa tuelewe kwamba haya mambo hayajaanza leo. Yana historia ndefu sana kuanzia enzi za Nuhu na watoto wake watatu.

Hamu, yule aliemchungulia baba yake, alilaaniwa kwamba atakuwa mtumwa (slave) wa ndugu zake (Shem na Japhet) siku zote. Na yule Ham ni baba wa waafrika genealogically. Hilo ni la kwanza.

Pili, hawa wazungu wanaoandamana ni wanafiki tu. Hakuna mzungu ambae anapenda kumtumikia mtu mweusi hata siku moja. Wanajifanya kuwa politically correct tu. Ukiangalia kwenye soka la Russia, Portugal, Italy na Spain, wachezaji weusi kama akina Dany Alves, Moussa Marega, Yaya Toure, Moise Kean, Mario Baloteli na wengine wengi, wanabaguliwa waziwazi, wengine wakitupiwa ndizi na mayai uwanjani, lakini serikali zao au vyama vya soka havichukui hatua zozote za maana.

Tena kwa Marekani, just imagine kama asingekuwepo yule binti aliechukua ile video ya mauaji ya George Floyd, tungeyaona mabaya yote yale? Ni wangapi wanaouawa vile na hatuoni? Mengi sana wanafanyiwa watu weusi ila hayaonekani. Majuzi tu yupo black boy mwingine anaeitwa Ahmaud Arbery, alieuawa na polisi mzungu wakati akifanya mazoezi binafsi tu.

Ndio mana hata Obama mwenyewe ni black ila hakufanya chochote maana hii inshu ni ngumu na ni ya kihistoria sana. Vita vyake havitakoma kamwe.
 
kuna mitaa kama harlem kule kipindi cha nyuma mtu mweupe alikuwa hapiti!hii tunaiitaje?!racism au revenge???wamarekani wazungu wale wazawa wa mitaa hiyo ndo utawaona.ila bado kwa marekani ubaguzi unaonekana sana sababu wana moral authority.

kuna nchi zina ubaguzi na huskii tena ule ubaguzi wa kichefuchefu!!!hasa nchi za kiarabu sisi tuliowahi kwenda kusalimia ndugu huko tuliyaona.

india kaskazini hapana mchezo ule sio ubaguzi ni vita ukionekana.afadhali nchi za south india mfano hydrebad,chennai nk zina ahueni sababu wale wahindi pia weusi tii
 
Ubaguzi Ulaya na sehemu nyingine duniani ni 5% au 10% Tu ila waafrika wenyewe tunabaguana zaidi ya 75% huu ni ujinga
 
lbaraka,
Polisi brutally is not about race,
VIP south Africa mwafrika kuuwa mwafrika mwenzake unasemaje hapo
 
Polisi brutally is not about race,
VIP south Africa mwafrika kuuwa mwafrika mwenzake unasemaje hapo
Of course police brutally is all about race. But sometimes not. Racism ni term pana sana. Inaanza kidogo kidogo baadae watu huua wengine. Mimi niliongelea kwenye mrengo wa Marekani na Ulaya ambako kuna mixed races. Wewe angalia mauaji ya kukusudia ya polisi, wanaouawa wengi ni watu weusi. Kwanini? Hilo si bahati mbaya. Ni kwa sababu ya ubaguzi tu. Wewe unadhani hii kaulimbiu ya #blacklivesmatter imetoka wapi mkuu? It's all about racism!

Kuhusu mauaji yaliyotokea majuzi South Africa, ile haikuwa racism. Ile ni xenophobia. Jaribu kusoma tofauti ya hayo maneno mawili kwny kamusi utauona utofauti. Although kwa kiswahili ni kama sawa but ni terms tofauti kabisa.
 
Habari yote hii ya Floyed ilipamgwa
..

Kuipunguza Covid 19...

Sahivi habari ni hiyo tuhh
.. No more corona. Na watu wamejikuta wamepona tu.
 
Of course police brutally is all about race. But sometimes not. Racism ni term pana sana. Inaanza kidogo kidogo baadae watu huua wengine. Mimi niliongelea kwenye mrengo wa Marekani na Ulaya ambako kuna mixed races. Wewe angalia mauaji ya kukusudia ya polisi, wanaouawa wengi ni watu weusi. Kwanini? Hilo si bahati mbaya. Ni kwa sababu ya ubaguzi tu.
Wewe unadhani hii kaulimbiu ya #blacklivesmatter imetoka wapi mkuu? It's all about racism!

Kuhusu mauaji yaliyotokea majuzi South Africa, ile haikuwa racism. Ile ni xenophobia. Jaribu kusoma tofauti ya hayo maneno mawili kwny kamusi utauona utofauti. Although kwa kiswahili ni kama sawa but ni terms tofauti kabisa.
Vipi Vita ya wenyewe kwa Africa sababu ya tofauti za kiitakadi
tanzania-police-brutality.jpg
kenya-violence-police_0.jpg
Kikaoni.jpg
ETGD4eHWoAIgxpL.jpg
police-brutality-kenya.jpg
_111686113_saspol2afp.jpg
daudi-mwangosi-remains.jpg
kenyaviolence1_051816051717.jpg
brtsap.jpg
zimbabwe-police(2).jpg
Screen-Shot-2015-03-13-at-10.03.02-PM-1024x650-1024x650(1).png
Police-1.jpg
396D7A51-FC7A-430A-B9F9-ECEF0C8C1319.jpg
e552Rpx9j8573b81671a00002f00c28b8c.jpeg
cop(1).jpg
Police-kick-child.jpg
Ug+police.jpg
31kenya.3.jpg
 
Mkuu mimi sikatai point yako moja kwa moja. Ni kweli hii si racism(according to your attachments). Ndo mana kama umesoma vizuri hapo juu nlipokujibu umeona nimeandika police brutally is racism but sometimes NOT. Wanaposema #blacklivesmatter wana maana kwamba uonevu wa polisi kwao kama watu weusi ni too much
 
Sawa na wazidi kutubagua, ili tuzidi kuwa Black Africans asilia, na tunazaana kwa kasi kuliko weupe wote Duniani, km alisema Magu tufanye tu! tuone watabagua nani! uzao wa wakoloni ni katoto kamoja tu ktk familia
 
Hawa jamaa zetu Wazungu wanatuogopa sana, ndhani kuna kitu ndani yetu kinawaumiza mno, ila sisi hatujajua! au wametuzuia kujua.
 
Ubaguzi Ulaya na sehemu nyingine duniani ni 5% au 10% Tu ila waafrika wenyewe tunabaguana zaidi ya 75% huu ni ujinga
Ata wazungu wenyewe wanabagua , iyo ndiyo sifa ya mwanadamu, anajiangalia yeye kwanza Kabla ajamuangalia mwingine !
 
Kuna wabaguzi kama watu weusi ?Weusi tunaongoza kwa ubaguzi ndo maana huwa tunaamini tunabaguliwa maana sisi tunabagua wenzetu. Leo nimeona video mbabu wa kizungu kaanguka kwenye maandamano. Polisi walikuwa wanampita tu. Nikajisemea huyu babu angekuwa mweusi,reactions za kubaguliwa zingejaa mitandaoni.
 
Mkuu mimi sikatai point yako moja kwa moja. Ni kweli hii si racism(according to your attachments). Ndo mana kama umesoma vizuri hapo juu nlipokujibu umeona nimeandika police brutally is racism but sometimes NOT. Wanaposema #blacklivesmatter wana maana kwamba uonevu wa polisi kwao kama watu weusi ni too much
Hakuna usawa kwa mwenye nacho na asiyo nacho. Tuache kujidanganya waafrika. Kinachofanya tunabaguliwa ni hii hali yetu ya umaskini na utegemezi kwa mambo mengi. Hili lipo mapka kwenye familia zetu. Kwenye familia hakuna usawa kati ya kaka maskini na mdogo wake tajiri. Ni lazima yule maskini, japo ni mkubwa aataangaliwa kwa jicho la dharau hata japo kwa kiasi kidogo.... na hapo ndipo ubaguzi huanza.
 
Back
Top Bottom