Ubalozi wa Marekani kuwaondoa raia wake Tanzania kwasababu ya Corona na kuwarudisha kwao

Hapo sijui nichangie nin?
Kwanin isiwe Kenya na Tz?
Hawa mabeberu ni wivu tunapiga kazi kuleta maendeleo yetu ,SGR, stickers na flyover
Watz tupige kazi tusitishwe na mafua
 
Hii inamanisha Marekani ni salama ata kama ina visa zaidi ya buku mbili, kuliko Tanzania ambayo ina visa 13
 
Kuna mijitu inatamani isikie Tanzania inaongoza kwa maambukizi na vifo kwa huu ugonjwa wa mabeberu kwa kweli mtasubiri sana kwa hili.
 
Kusafirisha maiti ni gharama kubwa heri warudi sasa wakafie kwao!
 
Hao walikua wanasubiriwa waupate.
Hospital ndio ingekua kizaazaa.
 
Hiyo anataka kwenda kuwaua tu raia zake huko Marekani.

Ni heri awapime na kuwa isolate hapa hapa Tanzania kipindi hiki kuliko kuwapelekea Marekani.
Tanzania salama? Watanzania wangapi wamepimwa kubaini kiwango cha maambukizi nchini?
 
Takwimu zetu sio za kweli, halafu tupo Kisiasa zaidi hatua madhubuti hazichukuliwi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We are too careless to control it. Mabasi, masoko. Kumbi, nk. Kama vile bado kabisa. Ukizuka mitaani utakuwa moto wa nyika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakija hao..nahisi watakuja na kichupa Cha Covid 19..wakifika airport wanakifungua..so tusishangae maambukizi kuongezeka baada ya watu wao kuondoka
 
Labda wamebashiri taharuki ya raia kunyanyapaliwa hasa ugonjwa ukishika kasi
 
Hata swine flue ya 2009 walisema Africa inaficha data mwisho wa siku hatukuathirika kama walivyoathirika wao.
 
Hata ungekua wewe utabaki katika nchi hii ya mficha maradhi??

Subirini tutakavyoanza kudondoka kama kuku wa kideli
Mkuu bora watuambie ukweli tu, na prediction yake siku zijazo watuambie ili tujipange kama kufanya saving na mambo mengine yatakayo tusaidia kukabiliana nayo siku ambazo corona itaweka kambi tz
 
Lazma Kuna vitu umeongezea hapa na umesahau kusema ndivyo ulivotafsiri wewe, haiwezekani wamarekani wawafukuzie raia wao sehemu yenye vifo karibia 2000 kutoka sehemu yenye maambuki ya watu 13 tu na wanaendelea vizur!!

Lazma Kuna kitu kinafichwa ama na sirikali ya Tanzania au USA!!
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Slow slow alisema wapinzani ni corona.... Ngoja tuwaondoe tubaki salama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…