Ubalozi wa Marekani kuwaondoa raia wake Tanzania kwasababu ya Corona na kuwarudisha kwao

Ubalozi wa Marekani kuwaondoa raia wake Tanzania kwasababu ya Corona na kuwarudisha kwao

Hapo sijui nichangie nin?
Kwanin isiwe Kenya na Tz?
Hawa mabeberu ni wivu tunapiga kazi kuleta maendeleo yetu ,SGR, stickers na flyover
Watz tupige kazi tusitishwe na mafua
 
Hii inamanisha Marekani ni salama ata kama ina visa zaidi ya buku mbili, kuliko Tanzania ambayo ina visa 13
 
Kuna mijitu inatamani isikie Tanzania inaongoza kwa maambukizi na vifo kwa huu ugonjwa wa mabeberu kwa kweli mtasubiri sana kwa hili.
 
Kusafirisha maiti ni gharama kubwa heri warudi sasa wakafie kwao!
 
Hao walikua wanasubiriwa waupate.
Hospital ndio ingekua kizaazaa.
 
Hiyo anataka kwenda kuwaua tu raia zake huko Marekani.

Ni heri awapime na kuwa isolate hapa hapa Tanzania kipindi hiki kuliko kuwapelekea Marekani.
Tanzania salama? Watanzania wangapi wamepimwa kubaini kiwango cha maambukizi nchini?
 
Kweli kabisa. Mtu akili yake imefungwa kiasi kwamba anathubutu kusema Marekani hakuna corona!! Kauli za Marekani zinatolewa kukidhi maslahi yao fulani tu. Jee, kuna yo yote aliyesikia balozi za Marekani nchini Uchina au Italia zikisema raia wake waondoke huko? Tanzania iko chini sana kwenye orodha ya nchi zilizoathirika na ugonjwa huu. Sasa iweje ndiyo iwe nchi ya kwanza kutajwa kujihami na ugonjwa kama siyo sababu nyingine wanazozifahamu wenyewe
tu.
Takwimu zetu sio za kweli, halafu tupo Kisiasa zaidi hatua madhubuti hazichukuliwi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani WHO, dunia inatangaza kila siku halafu anatokea mtu mmoja kutoka Tanzania anakubali Corona haipo Marekani, acheni kusujudia watu kila saa kwenye kila kitu mzee, tuliza akili.

Au taarifa zinazotolewa na Trump mwenyewe kuhusu hali ya Corona nchini mwake huwa hauzisikii, basi tufanye ile siyo Corona bali ni homa ya Dengue
We are too careless to control it. Mabasi, masoko. Kumbi, nk. Kama vile bado kabisa. Ukizuka mitaani utakuwa moto wa nyika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakija hao..nahisi watakuja na kichupa Cha Covid 19..wakifika airport wanakifungua..so tusishangae maambukizi kuongezeka baada ya watu wao kuondoka
 
Labda wamebashiri taharuki ya raia kunyanyapaliwa hasa ugonjwa ukishika kasi
 
Hivi upstair kwako kuko vizuri kweli?
Marekani ndio inaongoza kwa kuwa na case nyingi sasa hivi.

Nikupe ukweli:
Marekani anaona Serikali yetu haipo serious.
Inadanganya data na hakuna step yoyote inayochukuliwa.
Kwa hio wameshaona kuwa hili dude litakuja kuua watu hapa hadi kila mtu atashangaa
Hata swine flue ya 2009 walisema Africa inaficha data mwisho wa siku hatukuathirika kama walivyoathirika wao.
 
Hata ungekua wewe utabaki katika nchi hii ya mficha maradhi??

Subirini tutakavyoanza kudondoka kama kuku wa kideli
Mkuu bora watuambie ukweli tu, na prediction yake siku zijazo watuambie ili tujipange kama kufanya saving na mambo mengine yatakayo tusaidia kukabiliana nayo siku ambazo corona itaweka kambi tz
 
Lazma Kuna vitu umeongezea hapa na umesahau kusema ndivyo ulivotafsiri wewe, haiwezekani wamarekani wawafukuzie raia wao sehemu yenye vifo karibia 2000 kutoka sehemu yenye maambuki ya watu 13 tu na wanaendelea vizur!!

Lazma Kuna kitu kinafichwa ama na sirikali ya Tanzania au USA!!
akili zingine za kijinga sana. Marekani haisemi kwamba kwao hakuna Corona. Wanachosema watu wao warudi kwao ambako itakuwa rahisi kuwahudumia.

wanaogopa mipaka ikifungwa na hali ikawa mbaya kwao wakiwa Tanzania itakuwa mgumu kuwasaidia.

wakati wa majanga unataka familia yako irudi nyumbani kwako ambako unaweza kuwasaidia.

Hivyo ndivyo nchi zinazojali watu wake hufanya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Slow slow alisema wapinzani ni corona.... Ngoja tuwaondoe tubaki salama
 
Back
Top Bottom