Kama Balozi na Kaimu hawapo haina maana Ubalozi umefungwa mpaka warudi. Ofisi ya Serikali haitembei na mfanyakazi yeyote wa ofisi hiyo hata asiporudi kabisa shughuli zote zitaendelea kama kawaida. Wajinga wengi, pamoja na wewe, wanafikiri Tanzania ni mfano mzuri wa kuigwa katika kuendesha mambo ambapo mtu mmoja anaamua kila kitu na asipokuwapo basi hakuna chochote kinachofanyika mpaka arudi. Balozi za wenzetu hazitekelezi kazi zao kwa kutegemea mkuu ameamkaje kila siku, wait hata asipoamka mambo yao yataenda Kama kawaidà. Wafanyakazi wote was Ubalozi wowote ni wakazi wa nchi ilipo ofisi yao na mengi yanayotokea kwenye nchi walipo yanawagusa kwa namna moja au nyingine. Kukiwa hakuna mafuta au sukari nao wanaadhirika.