Ubalozi wa Marekani umezumgumzia kifo Ashly Robinson (31), aliyefariki dunia April 9, 2026

Ubalozi wa Marekani umezumgumzia kifo Ashly Robinson (31), aliyefariki dunia April 9, 2026

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251

Ubalozi wa Marekani Nchini Tanzania, umezumgumzia kifo cha Mwanamitandao ya kijamii kutoka Miami, Ashly Robinson (31), aliyefariki dunia April 9, 2026, kwa mujibu wa Jeshi la Polisi akiwa Visiwani Zanzibar,

Kauli ya Ubalozi huo, inatokana na maswali yaliyoulizwa na AyoTV, iliyotaka kufahamu kwa kina juu ya taratibu ambazo Ubalozi huo unafanya pindi raia wa taifa lao anapofariki nje ya Marekani, ambapo Msemaji wa Ubalozi huo Nchini Tanzania amejibu kupitia barua Pepe na kusema;

“Raia wa Marekani akifariki dunia nje ya Nchi, Ubalozi wa Marekani
hutoa msaada wa Kibalozi kwa Wanasheria, mwakilishi, Jamaa wa karibu, na Familia.

“Wakati Raia wa Marekani akifariki katika Nchi ya kigeni, mamlaka za ndani wana jukumu kuchunguza chanzo cha kifo na kutoa taarifa au matokeo ya uchunguzi huo,”.

“Tunaweza kuthibitisha kifo cha Raia wa Marekani kilichotokea
Zanzibar, Tanzania tarehe 9 Aprili 2026, na tunatoa rambi rambi zetu za dhati kwa familia na wapendwa
juu ya kuondokewa kwa Ndugu yao,”.

“Kwa heshima ya faragha ya
familia na wapendwa katika wakati huu mgumu, sisi hatuna maoni zaidi.”

Katika tukio hilo, mamlaka za Zanzibar zinamshikilia mchumba wake, Joe McCann, kwa ajili ya uchunguzi zaidi.


Pia soma:Polisi inamshikilia Joe McCann, Mchumba wa marehemu Ashly Robinson maarufu kama "Ashlee kwa mahojiano
 
Mnawachosha tu Wazanzibar kukomalia uchunguzi zaidi wakati walikuwa wafunge jalada mapema waendelee kujilia urojo tu.
Kitaeleweka tu, ama sivyo mfereji wa Zanzibar unafungwa.
 
Sawa.

Lakini Msukuma wa NASA 😂😂😂
Hongera sana mkuu na asante kwa kutuwakilisha vema.

images.jpg



Nyau de adriz
 
Lazima mchumba wake kausika mana wenyewe wapo wa2

uyo Mzungu kauwa Dada yetu mweusi mwenzetu!!!

lazima tubaki nae kwa miaka 10 ivi.

Familia yake Dada yetu ipo njiani inakuja tutaaakisha anajutia maisha yake yote!!!!

uyu Mbuzi wa kizungu kafia kwenye uko wa kina Lema!!! Shubamit
 
Naingia kwenye mada moja kwa moja bila kuwachosha. Taarifa kutoka rubaa za kimataifa zinasambaa kwamba nchi ya Marekani, chini ya utawala wa Rais Donald Trump, ipo mbioni kuiwekea vikwazo nchi ya Tanzania kufuatia kifo cha raia wa Marekani aliyeuliwa na watu wasiojulikana hivi karibuni akiwa katika ziara ya kitalii huko Zanzibar.

Inasemekana vikwazo hivyo vitajumuisha vikwazo vya kusafiri na vya kiuchumi pia. Miongoni mwa watu wanaolengwa kuwekewa vikwazo vya usafiri ni Rais Samia Suluhu pamoja na baadhi ya mawaziri, akiwemo Waziri wa Mambo ya ndani na IGP. Sababu za kulengwa hawa viongozi ni kushindwa kwao kutoa ulinzi kwa raia huyo wa Marekani na pia kutoa majibu yasiyoridhisha kufuatia kifo cha mwanadada huyo, ambaye alikuwa maarufu katika masuala ya mitandaoni.

Akiongea kuhusu tukio hilo, mwanadiplomasia kutoka Marekani, ambaye hakutaka kutambulika, alisema na ninamnukuu: "An attack to one American is an attacker to the entire sovereignty of the USA. In this case, no stone will be left unturned. All people involved in one way or another must suffer the consequences of their deeds or negligence. We can also take further actions as we did to Iran and elsewhere" Mwisho wa kunukuu.

MAONI YANGU
Siku zote nchi ya Marekani ipo mstari wa mbele kulinda maslahi ya nchi na watu wake. Hakuna mmarekani anayeweza kufa kizembe kwenye nchi ya kigeni halafu Marekani wasijibu, tena vikali. Sote ni mashahidi katika hili. Tumeshuhudia maelfu ya watanzania wanatekwa na kuuliwa kama kuku bila kuchukua hatua. Ngoja sasa Marekani wakawafundishe viongozi wa Tanzania jinsi ya kutetea maslahi ya nchi na raia wake. Nadhani hili litakuwa funzo kubwa sana kwa watawala wetu na vyombo vyetu vya ulinzi na usalama wa raia, hasa jeshi la polisi.

Nawasilisha.
 
Actions always have consequences, especially when you disrespect laws and public order in another country. Accountability isn’t optional.

She should lead a responsible lifestyle
 
Kama amejiua mwenyewe au kauliwa na huyo boyfriend wake Tanzania inahusika vipi? Wafanye uchunguzi kwanza
 
Actions always have consequences, especially when you disrespect laws and public order in another country. Accountability isn’t optional.

She should lead a responsible lifestyle
Exactly. What goes around comes around. This time she will learn a lesson for failing to protect the lives of her citizens as well as those from abroad. No mercy for her. Let every devil get his due.
 
Kama amejiua mwenyewe au kauliwa na huyo boyfriend wake Tanzania inahusika vipi? Wafanye uchunguzi kwanza
Wakiwekewa vikwazo ndipo wataharakisha uchunguzi na pia kutoa majibu ya kuridhisha. Tuwaache wafu wawazike wafu wao mkuu.
 
Mtu wa maana sana huyu baba....🤣
 

Attachments

  • VID-20260303-WA0025.mp4
    3.2 MB
Back
Top Bottom