#COVID19 Ubalozi wa Marekani, watoa tahadhari dhidi ya ongezeko kubwa la ugonjwa wa Covid-19

#COVID19 Ubalozi wa Marekani, watoa tahadhari dhidi ya ongezeko kubwa la ugonjwa wa Covid-19

Huwa napenda kukufwatilia but kuna komenti huwa unatyanka kweli kweli, mfano hii hapa👇👇👇
Hebu watupumzishe! Wameshindwa kuzuia vifo100 vya kupigwa risasi kila siku halafu hapa wanataka kutuongopea wanajali uhai wetuwetu.

Tuko zetu busy na kazi huku tukichukua tahadhari na kumwomba Mungu sana.
 
Huyu balozi katumwa na mabeberu eee, sisi hatuna COVID hapa, sisi tuna magonjwa ya mfumo wa upumuaji yaani nyumonia....
Ambayo nayo inapona kwa miti shamba kwa asililia 99.999999%

Kuhusu kufa kwani watu wameanza kufa leo?

Watanzania chapeni kazi!!
 
Hawaaminiki kwangu kama wasivyotuamini sie.. corona yao, vyombo vyao, teknolojia yao, wataalam wa kwao na wanaamua taarifa zao zipi zifikie walimwengu

Ila tusipuuze tahadhali Mama D....We have families to feed
 
Jambo jema kivipi mkuu? Huoni wanaingilia mambo yetu ya ndani ilihali kwao ndio moto unawaka zaidi?
Wakuingilie mambo yako ya ndani una kipi wewe hata net za wajawazito wanakupa msaada. Embu ondoa kelele hapa? Ati mambo ya ndani ? Kataa basi na ARV wanazokupa.na zile chanjo za wajawazito na watoto tengenezeni za miti shamba
 
Ila tusipuuze tahadhali Mama D....We have families to feed
Tahadhari tunachukua popote tulipo, kifo kinatisha, kinaweza kuwa chanzo cha umaskini kwa familia zetu lakini tuutafute ukweli wa madawa tunayopewa.

Usisahau mwanzo kabisa walishapendekeza kwamba majaribio yafanyike afrika kwa kigezo wanatupenda na kutuhurumia sana kwakuwa hatuna health facilities za kutosha.

Sasa na sisi tuwaambie tuu kwamba Afrika haijaathirika kama USA EU na Asia, waanze kuokoa idadi kubwa ya watu wao wanaokufa Upendo wa kweli huanzia nyumbani

Hakuna upendo wa kuwapa watoto wa jirani chakula wakati watoto wako wanakufa njaa
 
Tumeshindwa kutoa tahadhari wacha mataifa yenye nguvu wafanye hiyo.

Kutukuwepo kwa dawa na chanjo ya uhakika ni jambo moja, na kutoa tahadhari juu ya uwepo wa ugonjwa ni jambo lingine. Hivyo, kutokuwepo kwa chanjo ya uhakika na dawa ya ugonjwa huu hakutoia uhalali wa kufuchwa takwimu za ugonjwa pamoja na halihalisi ya maambukizi kwa umma.
Who cares, those masters of your are dying like flies.
 
Wewe ni kichaa unayetakiwa kuvishwa nguo huku ukiwaita wale wazima wanaokusitiri vichaa
Pole lakini
Vichaa wanajulikana nchi hii wapo sehemu gani kama siyo lumumba
 
Watupumzishe!!!!!!
Wacha tufanye taratibu zinavyoagiza huku tukimwomba Mungu
Tusisahau malimao, Tangawizi, pilipili na kupiga nyungu
Hivyo vyote unavifanya kwa tatizo gani wakati mmesema kuwa corona hakuna?
 
Hivyo vyote unavifanya kwa tatizo gani wakati mmesema kuwa corona hakuna?
Nani kasema corona hakuna😅😅 kwani Mungu alikupatia masikio ya nini? Si angekupea macho na vidole vya kutype tuu🙄🙄🙄

 
Huyu balozi katumwa na mabeberu eee, sisi hatuna COVID hapa, sisi tuna magonjwa ya mfumo wa upumuaji yaani nyumonia....
Ambayo nayo inapona kwa miti shamba kwa asililia 99.999999%

Kuhusu kufa kwani watu wameanza kufa leo?

Watanzania chapeni kazi!!
Nasema uongo jamani?
 
Back
Top Bottom